Mmoja wa majambazi aliyepigwa risasi na raia mmoja kutoka Afrika kusini eneo la Mgodi huo
Tukio hilo limetokea muda mfupi baada ya gari lililokuwa likisafirisha dhahabu kutoka mgodini kufika uwanja wa ndege wa mgodi huo wakatI ndege hiyo aina ya Jet{Air Tanzania} ilipokuwa kwenye harakati za kuruka na kuondoka Uwanjani hapo na kusafirisha dhahabu hiyo kuipeleka jijini Dar Es Salaam na ndipo yalipoanza kuishambulia.
Hata hivyo kati ya majambazi hayo manne yalikimbia baada ya mmoja wao kuwa kupigwa risasi na mzungu mmoja raia wa Afrika ya Kusini aliyetambulika kwa jina la Engenas Van der ambaye naye alipigwa risasi na mkono wake wa kushoto majambazi hayo kabla ya polisi kufika mgodini hapo kusaidia ambapo walikuta majambazi hayo yamekwisha mimina zaidi ya risasi 60 hewani zilizopelekea ndege hiyo kutobolewa ubavuni na nyuma.
Baada ya majambazi kuanza kurusha risasi za moto hewani walinzi wa mgodi walitimka kwenye eneo hilo hadi polisi walipofika eneo la tukio baada ya dakika 40.
Kabla ya kuanza kwa majibizano na walinzi majambazi hayo yalirusha bomu kwa lengo la kutaka kuilipua ndege hiyo,bomu ambalo lilikomea nje ya uzio wa Uwanja huo umbali wa mita 10 ambapo pia halikuwafanikiwa kulipuka.
Majambazi hayo ambayo yanasadikika kuwa ni raia kutoka nchini Burundi yalikuwa yamejihifadhi porini hadi gari hilo lilipowasili kwenye Uwanja huo na kutokea na ndipo mapambano na walinzi wa kampuni ya G4S waliokuwa wakisindikiza gari hilo ambapo hata hivyo hawakuhimili mapambano hayo na kutimka mbio kuokoa maisha yao.
Katika tukio hilo lililotokea jana Saa 5 asubuhi jambazi mmoja ambalo halikufahamika jina lake liliuawa baada ya kupigwa risasi Shingoni na mzungu huyo kabla ya polisi kufika eneo hilo lililogeuka Uwanja wa vita.
na bunduki aina ya smg yenye namba UA 89381997 iliyotengenezwa mwaka1997 na ilikuwa na risasi 62,bastola yenye namba N004847aina ya Chines na mabomu manne ya kurushwa kwa kwa mkono.
Kwa mujibu wa ukaguzi wa polisi inadaiwa kuwa dhahabu iliyokuwa imetarajiwa kusafirishwa ni box 16 zenye uzito wa kilogramu 400,taarifa ambayo imetofautiana na idara ya madini ya ambayo inaeleza kuwa katika ukaguzi wao siku moja kabla ya tukio waliweza kubaini mabox 25 ambapo kwenye kila box moja kulikuwa na tofari moja lenye kilo kuanzia 5-30 na ndiyo yaliyopaswa kusafirishwa na si yaliyokutwa leo eneo la tukio.
Ofisa mahusiano wa mgodi huo Joseph Mangilima alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo alisema hawezi kusema lolote kwa kuwa tayari jeshi la polisi lilikuwa kwenye upelelezi wa tukio.
No comments:
Post a Comment