MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Sunday, January 15, 2012

Msiba wa Marehemu, Regia Mtema(aliyekuwa Mbunge wa Viti maalum)

 Spika wa Bunge Anne Makinda akiwafarija ndugu wa Marehemu Regia Mtema aliyekuwa Mbunge wa Viti maalum mkoani Morogoro kupitia CHADEMA aliyefariki kwa ajali ya gari eneo la Ruvu Darajani mkoani Pwani siku ya Jumamosi saa tano akitoka Chalinze. Mwili wa marehemu unatarajia kusafirishwa kwenda Ifakara kwa mazishi yatakayofanyika jumatano. Kabla ya kusafirishwa Mwili utaagwa kiserikali katika  Ukumbi wa Karimjee siku ya Jumanne
 Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akitia saini kitabu cha maombolezo
 Rais Jakaya kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo
 Ndugu wa Marehemu Regia wakiwa wenye majonzi
 Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (katikati) Mbunge wa Msoma Mjini, Vicent Nyerere (kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama hicho, John Heche wakiwa kwenye Msiba
 Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akihojiwa na waandishi wa habari kwenye msiba kuhusiana na msiba huo
Spika Anne Makinda akihojiwa na waandishi wa habari

No comments:

Post a Comment