Na Anthony Siame
Waziri Mkuu Mizengo Pinda asema hafikirii kuwania Ubunge tena wala nafasi ya Urais mwaka 2015.
Pinda ameyasema hayo wakati alipowaita wahariri kutoka vyombo mablimbali vya habari Ofisini kwa Dar es Salaam.
Akizungumzia mambo mablimbali yanayolihusu Taifa ulifika wakati wa kuulizwa maswali kutoka kwa mmoja wa wahariri na mmiliki wa gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile alimuuliza swali Waziri Mkuu kwamba je mwaka 2015 hutawania Ubunge kama ulivyokwisha tueeleza kipindi kilichopita.
Baada ya kuulizwa sawli hilo kwanza alicheka na kusema kwamba sasa wewe wataka niseme, alianza kwa kusema kwamba yeye hawezi kubadilisha kauli yake ni wazi kwamba hatawania nafasi ya Ubunge tena maana kipindi cha miaka 15 kinamtosha sana
Na Vilevile aliongeza kuhusu swala la Urais alisema yeye hana nia hiyo maana kwanza amekaa Ikulu kwa muda mrefu hata kumzidi hayati Mwalimu Jk Nyerere, alisema maisha yake yote ametumiki Ikulu toka kipindi cha Nyerere, aliongeza kusema bahati aliyoipata ya kuwa Waziri Mkuu amelizika nayo na anamshukuru Mungu
Alisema Ikulu ni Mzigo mzito sana tofauti na watu wengine wanavyofikiria, wanaokimbilia Ikulu lazima watakuwa na manufaa wanayatafuta siyo swala la kuwatumikia wananchi na alisema kipindi kikifika wananchi ndiyo wataamua ni Rais wa namna gani wanamtaka
No comments:
Post a Comment