MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Thursday, January 26, 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa, katika mkutano uliofanyika siku ya jumatano na kuhudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu, Asha-Rose Migiro, Katika Katibu Mkuu alianisha Mpango Kazi wa miaka mitano pamoja na vipaumbele vitano. baadhi ya vipaumbele hivyo, ni pamoja na uwezeshaji wa wanawake ili waweze kushika nafasi za uongozi za kisiasa halikadhalika kuwawezesha kiuchumi pamoja na kushughulika masuala ya vijana.Kuzihamasisha nchi kupinga kwa nguvu zote ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Kusimamia maendeleo endelevu na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia, mabadiliko ya tabia nchi, kuimarisha utoaji wa huduma za dharura na misaada ya kibinadamu, kuzisaidia nchi ambazo zimetoka katika migogoro na kusimamia suala zima la upokonyaji wa silaha. Mara baada ya mazungumzo yake na Mabalozi, Ban Ki Moon alikutana na waandishi wa Habari ambapo pia alielezea vipaumbele hivyo na pia kutangaza mabadiliko makubwa ya safu ya uongozi katika Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa. Akielezea mabadiliko hayo, Ban Ki Moom aliwaambia waandishi kwamba, Naibu Katibu Mkuu Migiro pamoja na Msimamizi Mkuu wa Ofisi yake, Vijay Nambier wamewasilisha kwake ombi la kuachia nafasi zao ili kumpisha kuunda safu mpya ya wasaidizi wake. Katika mabadiliko hayo wapo pia maafisa waandamizi kutoka Idara na Mifuko ya Umoja wa Mataifa, ambao nao pia wataachia nafasi zao. wengi wao ni wale ambao wamefanya kazi na Katibu Mkuu katika miaka mitano ya kwanza ya uongozi wake.




No comments:

Post a Comment