Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dk. Emmanuel Humba (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mwezeshaji wa Mfuko huo, Eugen Mikongoti wakati wa Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam. Mfuko huo utatimiza miaka kumi tangu kuanzishwa. ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Sherehe zitakazofanyika makao makuu ya Bima ya Afya
Mkurugenzi Mwezeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Eugen Mikongoti akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mfuko huo kutimiza miaka kumi tangu mwaka 2001 ambapo waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe zitakazofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Emmanuel Humba na kulia ni Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na uwekezaji Deusdedit Rutazah.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika Mkutano huo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Emmanuel Humba (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya mfuko huo kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake tarehe 19 mwezi huu ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe zitakazofanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa utafiti na Takwimu Michael Mhando akifuatiwa na Beatus Chijumba ambaye ni Mkurugenzi rasilimali watu na utawala.




No comments:
Post a Comment