Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole Zaina Mkieli, Mama wa aliyekuwa msanii
wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina
la Sharo Milionea, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi kwenye mazishi
ya msanii huyo, leo kwenye Kijiji cha Lusanga, Muheza Tanga. Picha na
Bashir Nkoromo
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (Watatu kulia, waliobeba
jeneza) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msanii wa
muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la
Sharo Milionea, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi, kwenye mazishi ya
msanii huyo, leo kwenye Kijiji cha Lusanga, Muheza Tanga
Nape Nnauye akitoa pole za Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipokiwakilisha
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki
wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo
Milionea,leo kwenye Kijiji cha Lusanga, Muheza Tanga.
waombolezaji wakitupia mchanga kaburini,
Waombolezaji wakimsaidia mwenzao aliyepoteza fahamu mwakati wa
mazishi
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na
filamu Tanzania, Hussein Ramadhani, maarufu Saharo Milionea, likiwasili
nyumbani kwao, Lusanga, Muheza mkoani Tanga, wakati wa mazishi leo
Mzee Kingi Majuto akitupa mchanga kaburini kumzika Sharo Milionea
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na Rais wa Bongo
Movies Simon Mwakifyamba na Ofisa Habari wa Airtel Jackson Mbando
Mwana FA akitoa salam kwa niaba ya Wanamuziki wa Bongofleva, wakati wa mazishi hayo
Baadhi ya wasanii wa muziki wa bongo fleva na filam Tanzania, wakiwa kwenye mazishi ya Sharo milionea
Mkuu wa wilaya ya Muheza, Subra Mgalu akisoma salam za Shirika la Fursa
Sawa kwa Wote (EOTF) la Mama Anna Mkapa, kwenye msiba huo.
Vijana wakiwa wamepanda mnazi kwa ajili ya kushuhudia mazishi ya aliyekuwa msanii wa
muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la
Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha Lusanga, Muheza Tanga.
No comments:
Post a Comment