Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha ujenzi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha ujenzi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River
Viongozi wakuu wa nchi wanachama
wa Jumuiya ya Afrika mashariki Jumatano Novemba 28, 2012 wamefungua rasmi wa
barabara ya Arusha – Namanga kwa upande wa Tanzania, na Namanga– Athi River kwa
upande wa Kenya, kama sehemu ya mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi unaofanyika
Nairobi, Kenya.
Barabara ya Arusha – Namanga
– Athi River yenye urefu wa kilometa
104.4 kwa upande wa Tanzania ilikuwa ni mojawapo ya shughuli za uzinduzi rasmi
wa Makao Makuu Mapya za Jumuiya uliofanyika mapema siku hiyo hiyo jijini Arusha,
kabla ya viongozi hao kuelekea Athi River kwa ufunguzi wa barabara hiyo.
Ujenzi wa barabara ya Tanga–Horohoro, yenye urefu wa kilomita 66
pia nao umekamilika na tayari imeanza kurahishisha
usafiri na usafirishaji baina ya Tanzania na Kenya na nchi nyingine wanachama.
Barabara nyingine zilizopo katika mtandao wa barabara wa Jumuiya
zinazoendelea kujengwa kwa upande wa Tanzania, ni pamoja na zile za mtandao wa
Dar es Salaam-Isaka-Lusahunga na Mutukula hadi Masaka; Lusahunga-Nyakasanza
hadi Rusumo, na Rusumo-Kigali hadi Gisenyi.
Nyingine ni Biharamulo - Mwanza - Musoma - Sirari - Lodwar –
Lokichogio; Tunduma - Sumbawanga - Kigoma - Manyovu (Mugina) - Rumonge -
Bujumbura - Ruhwa (Bugarama) – Karongi hadi Gisenyi, pamoja na ile ya Tunduma -
Iringa – Dodoma - Arusha - Namanga hadi Moyale.
Ujenzi wa barabara hizi utarahisisha usafiri na usafirishaji wa
bidhaa na huduma baina ya nchi wanachama, na hivyo kupunguza gharama za
uzalishaji na vilevile gharama za kufanya biashara katika nchi za Jumuiya na
hivyo kuvutia uwekezaji.
No comments:
Post a Comment