Kocha Mkuu wa timu ya The Express ya Uganda, Mosese Basena akifurahia baada ya kuwaona waandishi kutoka nchini Tanzania
Kocha Mkuu wa The Express ya Uganda, Moses Basena (katikati), Mike Mkunza kutoka Exerctive Solution, Timzo Kalugila kutoka gazeti la Super Star wakifurahi jambo walipokutana ndani ya Uwanja unaomilikiwa na timu hiyo kabla ya kuanza kwa mazoezi ya Kilimanjaro Stars ya kujianda na mchezo dhidi ya timu ya Burundi unaochezwa leo latika Uwanja wa Nelson Mandela ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya Tusker Challenge Cup 2012 inayoendelea nchini Uganda
Huu ni Uwanja unaomilikiwa na timu ya The Express ya Uganda ambapo timu ya Kilimanjaro Stars iliutumia kufanyia mazoezi ikiwa ni maandalizi ya mchezo dhidi ya Burundi unaochezwa leo katika mwendelezo wa michuano ya Tusker Challenge Cup 2012 inayoendea katika Uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda
Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Moses Basena ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa timu ya Express ya Uganda, akizungumza na baadhi ya wachezaji wa Kilimanjaro Stars walipokutana kwenye Uwanja unaomilikiwa na timu hiyo kabla ya kuanza kwa mazoezi ikiwa ni maandalizi ya mchezo dhidi ya timu ya Burundi unaochezwa leo katika Uwanja wa Nelson Mandela ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya Tusker Challenge Cup 2012.
katika mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa kuanzia muda wa saa kumi nambili za jioni timu ya Kilimanjaro Stars itabidi icheze mchezo wa kasi kutoka na timu hiyo ya Burundi nayo inacheza mchezo kasi sana
Wakati wa mazoezi ya Kilimanjaro Stars, Kocha Mkuu, Kim Poulsen aliwapa mazoezi wachezaji ya kutoa pasi kwa haraka na kutafuta nafasi ambapo kila mcheza aliweza kufanya mazoezi hayo katika Uwanja huo.
Kilimanjaro Stars inaingia Uwanjani leo ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wa kwanza goli 2-0 dhidi ya timu ya Sudani magoli yaliyofungwa na John Boko (Adebayo)
katika mchezo wa leo Kilimanjaro Stars itaendelea kuwakosa wachezaji wake wanaochezea timu ya TPP Mazembe , Mbwana Samata na Tomas Ulimwengu ambao mpaka sasa hawajaweza kuungana na timu
No comments:
Post a Comment