Kilimanjaro Stars wakishangilia wakati wa mchezo wa robofainali dhidi ya Rwanda katika mchezo wa Chalenji uliochezwa Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda. Kilimanjaro Stars ilishinda 2-0
Kesho tarehe 6 Desemba, kutakuwa na michezo miwili ya nusu fainali ya michuano ya Chalenji 2012 inayofanyika katika Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Nambole nchini Uganda
Nusu Fainali ya kwanza itaanza saa kumi kamili kwa kuzikutanisha Zanzibar Heroes vs Kenya ambapo mtanange huo unatarajia kuwa mkali na hali ya juuu kutokana na timu zenyewe kuwa na morali wa hali ya juu, Zanzibar kwa kufikia hatua hiyo ya nusu fainali iliweza kuiondosha Burundi katika mchezo wa robo fainali kwa jumla ya mabao 6-5 kwa njia ya matuta baada ya kwenda sulu bini sulu katika muda wa dakika tisini
Vilevile kutakuwa na nusufainali ya pili itakayozikutanisha, Kilimanjaro Stars na wenyeji Uganda, mtanange utakaoanza kwenye muda wa saa moja kamili katika Uwanja huohuo wa Nelson Mandela
No comments:
Post a Comment