MAELFU ya Wakazi wa mkoa wa Mtwara leo wameandamana kutoka kijiji cha Mtawanya umbali wa kilomita
Tisa hadi Mtwara mjini barabara ya kwenda Msimbati eneo ambalo gesi
asilia inavunwa wakipinga uwamuzi wa serikali wa kusafirishwa gesi kwa
njia ya bomba kutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam.
Maandamano hayo ambayo yaliudhuriwa
na wananchi kutoka baadhi ya wilaya za mkoa wa Mtwara, zikiwemo
Tandahimba na Newala yamefanyika kwa hali ya amani na utulivu huku
yakisindikizwa na ulinzi mkali wa polisi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na
waratibu wa maandamano hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Joseph Simbakali
alipaswa kuwa mgeni rasmi hata hivyo alikataa na badala yake
yalipokelewa na mwenyekiti wa umoja wa vyama vya siasa Hussen Mussa
Amiri.
Vyama vilivyounda umoja huo ni
Chadema, NCCR-Mageuzi, SAU, TLP, APPT Maendeleo, ADC, UDP na DP, vikiwa
na kaulimbiu ya gesi kwanza vyama baadaye, hapa hakitoki kitu.
Soko kuu la mjini hapa, lilifungwa
kwa mda hadi maandamano hayo yalipotia nanga, kutoa fursa kwa
wafanyabiashara hao kushiriki katika maandamano hayo ambayo
yalisababisha barabara kufungwa kwa mda.
Mabango yalitumika zaidi kuwasilisha
ujumbe wa wananchi hao wa kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam ambapo
baadhi yalisomeka "Bandari Bangamoyo, Viwanda Bagamoyo, Gesi Bagamonyo,
Mtwara wapuuzi?....Gesi haitoki hata kama hatujasoma......gesi kwanza
vyama baadae, hapa hakitoki kitu....kusini tumezarauliwa vya kutosha
sasa baasi" yalisomeka baadhi ya mabango.
Akisoma tamko la vyama vya siasa vya
upinzani vilivyoungana kupinga gesi kwenda Dar es Salaam katibu wa umoja
huo, Seleman Litope kwa mda mrefu kusini imekuwa zikiondolewa fursa
mbalimbali za maendleo, akitolea mfano wa kung'olewa kwa reli, ukosefu
wa usimamizi mzuri wa zao la korosho, ukosefu wa miundombinu ya
barabara, kuodnolewa kwa mradi wa maendeleo ya ukanada wa Mtwara (Mtwara
coridor ) na kuondolewa kwa gesi.
Alisema hali hiyo imesababisha mikoa
ya kusini kuwa nyuma kimaendeleo na kwamba hawako tayari kuona historia
ikijirudia na kwamba umoja wao wa vyama Nane vya siasa unalenga
kuhakikisha rasilimali yao hiyo haitoki kwenda kokote kabla ya
kuwanufaisha.
"Ujenzi usitishwe...serikali hadi leo
haiko wazi namna gani wakazi wa Mtwara watanufaika na gesi hiyo wakati
rais ameshazindua ujenzi wa bomba kwenda Dar es Salaam...uwamzi wa
kupeleka gesi Dar es Salaam unapingana na tamko la Rais Jakaya Kikwete
alilolitoa kwenye ziara yake mkoani Mtwara 2009 kwamba mkoa wa Mtwara
ujiandaye kuwa ukanda wa viwanda" alisema Litope
Taarifa hiyo imebainisha kuwa "Tuna
hofu kutokana na ilivyokuwepo kwa wakazi wa Songongo (Lindi) kubaki
masikini wakati gesi inazalishwa hapo, yasije yakatukuta sisi hivyo ni
lazima tusimamie rasilimali hii ili iweze kuleta maendeleo”
Tamko hilo lenye kurasa mbili likiwa
na maadhimio tisa linahoji kwanini mitambo ya kuzalisha umeme isijengwe
Mtwar wakati eneo kwa ajili ya ujenzi huo linapatikana.
Aidha waandamanaji hao wamemuomba
Rais Kikwete kumuondoa madarakani Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Joseph
Simbakalia kwa madai amewatusi wananchi wa mkoa huo kwa kuwaita wapuuzi
kutokana na madai yao ya kupinga gesi kwenda Dar es Salaam.
“Tunamuomba Rasi Jakaya Mrisho
Kikwete amuondoe katika nafasi ya Ukuu wa mkoa ndugu
Joseph sombakalia na kutuletea mwingine kwa sababu ametutukana
hadharani, tumeshindwa kuvumilia, HATUMTAKI” ilisema sehemu ya tamko
hilo.
Picha zote hizo ni wanannchi wakiwa kwenye maandamano leo
No comments:
Post a Comment