MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Sunday, December 23, 2012

Waziri wa Habari atembelea Kituo Cha Shirika la Utangazaji Mwanza

 Mhandisi Zablon Mafuru (kushoto) ambaye ni mkuu wa Kituo cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mwanza  akimuonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kulia) hivi karibuni mtambo wa Radio Tanzania wa masafa marefu (Medium Wave) unaorusha matangazo yake katika mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Shinyanga, Kigoma , Siminyu  na nchi jirani za Uganda na Rwanda uliopo Ilemela jijini Mwanza.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kushoto) akiangalia mtambo wa kurushia matangazo ya redio kwa  masafa mafupi  (Short Wave) na Televisheni wa Shirika la Habari la Tanzania (TBC) hivi karibuni uliopo eneo la Nyashana jijini Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana  James Kajugusi. 
 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kushoto) akikagua kiwanja cha Shirika la Habari la Tanzania (TBC) kilichopo  eneo la Kapripointi jijini Mwanza. Kulia ni Eston Sanga ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa Shirika hilo.
 

No comments:

Post a Comment