Marehemu, Juma Kilowoko (SAJUKI) akiwa na mkewe Wastara Juma wakati wa kufunga Ndoa
wakiwa wamepozi katika picha na mkewe enzi za Uhaa wake
Ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa Msanii Sajuki wakiwa nyumbani kwao kwa marehemu Tabata Dar es Salaam
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri
wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella
Mukangara amewatumia salamu za
rambirambi, ndugu, jamaa na wasanii wote nchini kufuatia kifo cha msanii Juma
Kilowoko (SAJUKI) kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013 katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa
iliyotolewa leo, jijini Dar es salaam ,Wizara ya Habari, Vijana na Utamauni na
Michezo imepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha msanii huyo
na kuongeza kuwa kifo hicho ni pigo katika tasnia ya filamu hapa nchini.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo Kifo chake ni pengo kubwa kwa Serikali, wadau wa tasnia
ya filamu na michezo ya kuigiza nchini kwa ujumla.
“Nimepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha SAJUKI sina maneno ya kuelezea
masikitiko na huzuni nilinayo , kwani kifo chake ni pigo katika tasnia ya
filamu za michezo ya kuigiza” alisema Dkt Mukangara.
Dkt.
Mukungara amewataka ndugu, jamii na wasanii wote kuwa wavumilivu na watumilivu
wakati wote wa msiba na kumuombea marehemu makao mema kwa Mwenyezi Mungu.
Juma
Kilowoko (SAJUKI)ni mzaliwa wa mkoa wa Ruvuma. Sajuki alianza kujihusisha na
masuala ya maigizo alipojiunga na kikundi cha Kaole na baadaye filamu. Filamu
alizocheza ni pamoja na Revenge
ya Kampuni ya RJ .
Mwaka
2008 aliamua kuanza kutengeneza kazi zake mwenyewe ambapo filamu yake ya kwanza
iitwayo Two Brothers kwa kushirikiana na Shija Deogratious ilitoka. Sajuki baadaye aliamua kuanzisha kampuni yake iitwayo
WAJEY Production Company ambapo alitengeneza filamu nyingi zikiwemo Mboni
Yangu, Round, Briefcase , Kijacho, Kozopata, Mchanga na Keni, 077( Zero Seven
Seven).nk
Sajuki alifanikiwa kucheza michezo ya kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye majina hapa nchini. Sajuki amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na Uongozaji wa filamu.
Sajuki alifanikiwa kucheza michezo ya kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye majina hapa nchini. Sajuki amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na Uongozaji wa filamu.
Sajuki
alianza kuugua mwaka 2010 na hali ilizidi kudhoofu mwaka 2011,ambapo alikwenda
kutibiwa nchini India. Wadau wengi wa tasnia ya filamu walifanikiwa kutoa
michango mbalimbali iliyomwezesha Sajuki kupata matibabu yake. Alirudi na
kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo lilileta matumaini na furaha kwa watanzania; aliporejea tu aliweza
kutoa filamu iitwayo Kivuli huku filamu nyingine ikiwa katika hatua ya
utengenezaji.
Aidha
hali yake ilibadilika jambo lililolazimu alazwe katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili hadi umauti ulipomkuta usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013
Mungu ailaze roho ya
Marehemu mahali pema peponi Amen
No comments:
Post a Comment