MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Wednesday, January 2, 2013

Waziri Muhongo aelezea kuhusu Gesi ya Mtwara

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam kuhusiana na Gesi inayochimbwa mkoani Mtwara ikiwa ni pamoja na maandamano  ya amani yaliyofanyika ya kupinga Bomba la Gesi kujengwa mkoani humo kupelekwa Dar es Salaam.

Akizungumza katika Mkutano huo Waziri alisema Nchi hii raslimali zote zinazopatikana zinatumika kuleta maendeleo kote nchini, hakuna hata siku moja  ilishatokea kuwa  rasilimali ikipatika sehemu fulani watatumia watu wanaoishi huko ambako rasilamili hiyo ilikopatikana

Hapa alitolewa mfano wa Mlima Kilimanjaro, akisema kuwa Pesa inayopatikana kwenye kivutio cha Mlima huo zinatumika kuleta maendeleo sehemu yoyote katika nchi hii akiongezea kwa kusema kuwa hiyo ndiyo sera ya Taifa hili na si vinginevyo kama watu wanavyodhania.

akizungumzia kuhusu kushirkishwa kwa wananchi alisema si kweli kama baadhi ya watu wanavyosema hatujawahi kuwashirikisha wananchi katika mradi huu wa Gesi, alisea kuwa wakati wa uzinduzi wa Mradi huu walichukuliwa wabunge wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini iliyovunjwa pamoja na wabunge wa Mikoa ya kusini kwenda kushuhudia uzinduzi huo na kuwapeleka baadhi ya wabunge katika nchi za Norway na kwingineko kujifunza namna Gesi hiyo itakavyowanufaisha wakazi wa maeneo ya mradi huo
  Kuhusu kuwashirikisha wananchi, Waziri alisema wameshirikishwa kikamilifu katika mradi huo na kuwaelezea jinsi watakavyonufaika katika mradi huo ni pamoja na Nyumba zao zote kuwekewa Umeme kwa gharama nafuu.


No comments:

Post a Comment