Ni
Mwanamke wa Kwanza kushika wadhfa huo katika Sekta ya anga.
Kampuni ya precision Air, imemtangaza Sauda
S. Rajab kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa kampuni hiyo, ambaye anajiunga na kampuni
hiyo kuanzia machi mosi mwaka huu. Akiwa amelitumikia Shirika la Kenyan Airways
kwa miaka 23 akiwa ameshika nafasi mbalimbali katika shirika hilo na sasa akiwa
kama Meneja Mkuu kitengo cha mizigo. (Cargo)
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya Precision Air,
Michael Shirima, amesema, kuwa Sauda Rajab, ataleta mtazamo
mpya wa kiutawala kwa Precision Air kukua zaidi na kujenga ushindani kwa
kampuni kubwa za usafiri wa anga duniani.
“Anao uwezo wa
kujenga katika msingi ambao tayari Kioko na wafanyakazi wengine wameweza
kuujenga.,” alisema Shirima.
“Sauda Ameahidi kutimiza majukumu
yake vyema baada ya kutembelea katika vitengo mbalimbali na kuahidi kuwa
atatimiza majukumu yake ipasavyo kwa kuongeza tija zaidi katika utendaji na
utawala,” alisema.
Kioko amestaafu akiwa
ameitumikia kampuni kwa miaka 10 tangu alipojiunga na Precision Air na kuijenga
kampuni na kuipa mafanikio makubwa
“Tangu alipojiunga na
kampuni mwaka 2003 kampuni ilikuwa ikimiliki ndege mbili aina ya ATR 42 na
ndege nyingine ndogo. Katika kipindi cha uongozi wake hadi sasa kampuni ina
ndege tisa na nyingine Mpya ikiwemo 1ATR 42-300, 7ATRs 42-500, 2ATRs 42-600 na
Boeing mbili 737-300 na kufikisha idadi ya ndege 12 ambazo zimeiongezea uwezo
wa kiutendaji kampuni na kuwa pekee inayofanya safari zake katika sehemu nyingi
za nchi.” Alisema Shirima
“Idadi ya wateja ilikuwa kutoka 200,000
na hadi kutarajiwa kufikia milioni moja Mwaka huu na kuongezeka kwa mapato
kutoka bilioni 20 mwaka 2004 hadi Bilioni 163 mwaka 2011/2.” Alisema.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kioko amesema “Mafanikio
ya Precision Air hayajafikiwa kutokana na jitihada zake mwenyewe ila ni pamoja
na wateja na wafanyakazi wa wote wa Precision Air ambao wamekuwa wakiunga mkono
huduma mbalimbali za kampuni hiyo.
“napenda kuwaita familia ya Precision Air. Ninaamini
wataendeleza ushirikiano huu kwa Sauda.”
Shirima amesema kuwa, hakika Mkurugenzi huyo anayemaliza
muda wake ameifikisha Precision katika sehemu kubwa ambayo kila mtu anajivunia
na hata ukweli unajidhihirisha kutokana na nafasi ambayo shirika hilo linayo
kwa sasa.
“Tumejivunia sana kuwa na mtu kama Kioko kwa kile ambacho
ametufanyia sisi kama Precision Air.
Kwa upande wake, Bi Sauda amesema kuwa amevutiwa na
kujiunga na kampuni ambayo imekuzwa na wazawa na yuko tayari kuisogeza mbele
zaidi.
“Ninafurahia kupata nafasi hii, Ninatarajia kupata
ushirikiano mzuri katika kufikia majukumu haya mapya.”
Sauda alihitimisha kwa kusema kuwa moja ya Changamoto
ambazo atazipa kipaumbele katika uongozi wake ni suala la usafirishaji na
upakiaji wa miziko katika sekta ya anga kwa nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara
na Afrika kwa ujumla kwa kuandaa mpango maalum wa kuwezesha kukabiliana na
changamoto hiyo.
No comments:
Post a Comment