Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Amina Masenza alishangaa kuona hali aliyoikuta
ndani ya Bweni la kulala wanafunzi wavulana shuleni hapo.
Sehemu ya Bweni la wanafunzi wa kiume wakiwa wamehifadhi matandiko yao ambalo ni darasa.
Wanafunzi
zaidi ya 119 wa sekondari ya Mount Zion wakiwa wamebanana darasani na
imedaiwa kulipa gharama ya ada ya Shilingi milioni 1 kwa mwaka lakini
wengi wao hukalia viti na ndoo za plastiki darasani
wanafunzi wakiwa wamekalishwa chini vichakani huku mmoja wa walimu
akiwalinda kabla ya kukutwa na viongozi walioambatana na Mkuu wa Wilaya
ya Ilemela kuwakuta mafichoni
wanafunzi wakiwa wamekalishwa chini vichakani huku mmoja wa walimu
akiwalinda kabla ya kukutwa na viongozi walioambatana na Mkuu wa Wilaya
ya Ilemela kuwakuta mafichoni
Moja ya vyumba vya Bweni la kulala wasichana katika sekondari ya Mount
Zion iliyopo Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza kamainavyoonekana.
SEKONDARI ya Mount Zion (Bweni) ya
binafisi iliyopo Manispaa na Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza imefungwa na
kuzuiliwa kuendelea kutoa huduma ya kitaaluma baada ya Mkuu wa Wilaya Ilemela kwa kushirikiana na Idara za Elimu na
Afya kufanya ukaguzi na kubaini mazingira ya shule hiyo kuwa hatarishi.
Ziara ya kustitukiza iliyofanywa na
Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Amina Masenza aliongozana na wajumbe wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama kufanya ukaguzi katika shule hiyo na
kubaini wanafunzi kuishi katika mazingira hatarishi huku uongozi wa shule hiyo
ukiwaficha baadhi ya wanafunzi zaidi ya 50 wa bweni vichakani kukwepa
ukaguzi.
Hatua hiyo inafuatia kuwepo taarifa
zilizotolewa kwa Mkuu huyo na baadhi ya wasamaria wema jambo iliyomlazimu
ujumbe huo kufika shuleni hapo ili kujionea hali halisi na kukutana na uongozi
wa shule hiyo,tangu kutakiwa kuboresha kasoro na mapungufu yaliyoonekana baada
ya ukaguzi wa awali uliofanywa na Idara ya Afya ya Manispaa hiyo Februari 13
mwaka huu na kutakiwa kutekelezwa haraka.
Uongozi wa sekondari hiyo pamoja na
kuomba kupatiwa muda wa wiki mbili ili kufanyia marekebisho kasoro na mapungufu
yaliyokutwa baada ya ukaguzi wa awali na kugundulika kutokuwa na vyoo na mfumo
wa maji taka,mabweni maalumu kwa wavulana na wasichana,vyumba vya madarasa
kupunguza mrundikano,sehemu ya kutayarishia vyakula, majengo ya utawala shemu za kufulia
nguo,eneo la viwanja vya michezo mbalimbali na usalama.
“Shule hii haina Stoo na Jiko la
kutayarishia vyakula kwa wanafunzi kwani hupikiwa nje kwenye mabanda na hata ukumbi
(Bwalo) la kulia chakula hali inayosababisha wanafunzi kwenda kulia vyakula
wanakolala na kwenye miti iliyopo ndani ya eneo la shule nyakati za
mchana,hakuna mabweni ya kulala wanafunzi wasichana yakiwa hayana hata vitanda
na kulazimika kulala kwenye baadhi ya vyumba vya madarasa na hata wavulana pia”alisema
Afisa Afya wa Manispaa wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya na ujumbe wake.
Aidha alieleza pia kuwa ,shule hiyo
haina hata eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya ufuaji nguo (Laundry),haina
viwanja vya michezo kabisa (Playing grounds),usalama haupo kutokana na
kutokuwepo uzio na sanduku la huduma ya kwanza pamoja na vifaa vya zimamoto
(Fire Extinguishers),vyumba vya madarasa ni saba kwa wanafunzi 515 wakati
ilisajiliwa ikiwa na madarsa hayo kuhudumia wanafunzi 160 tu
Afisa Afya wa Manispaa ya Ilemela
Daniel Batare alieleza kwamba pamoja na kuwepo mapungufu hayo bado shule hiyo yenye
kidato cha kwanza hadi cha nne haina vyumba vikubwa vya madarasa na wanafunzi
kukaa bila kufuata mpangilio wa 45 kwa darasa na kulazimika kukaa 119 darasa
moja A,B na C kutokana madarasa mengine kutokamilika hali ambayo inaweza
kusababisha kukumbwa na magonjwa ya mlipuko.
“Tatizo la Bweni ambalo limeonekana kuwa kubwa
katika shule hiyo ambapo wanafunzi wote 515 ni wa bweni huku wavulana 240
hulala kwa mgawanyo ambapo 120 wamekuwa wakilala chumba kimoja cha darasa
kilichogeuzwa bweni na wengine 120 wakilala kwenye nyumba iliyokodishwa vikiwa
mita 2 kwa 3 vilivyopo jirani na shule hiyo wakihifadhi masanduku ya bati
wanayotunzia vifaa vyao”alieleza Afisa huyo
Alieleza kuwa wanafunzi wasichana
275 wanalala kwenye vyumba vidogo vinane vya ukubwa wa mita 2 kwa 3 ambapo kila
chumba kimoja hulala wasichana 34 ambacho ni hatari kwa usalama wa wanafunzi
hao na kukiwa hakuna vitanda na wakilazimika kuweka magodoro yaliyo chakaa
chini huku sakafu yake ikiwa imebomoka hali ya usafi ikiwa ni finyu pamoja na
kukutwa wadudu kama panya,mende na kunguni wakiwa kwenye vyumba hivyo.
“Umejionea Shule hii haina hata
jengo la utawala (Administration Block) na badala yake hutumia chumba kimoja
cha ofisi ya mkuu wa shule,hakuna ofisi ya walimu kazi zao hufanyia kwenye varanda
na madarasa,pia hakuna hifadhi ya vitabu (Library)
.
Akisoma
Ilani ya Kisheria ya kusitisha shughuli za utoaji elimu kwa shule hiyo mbele ya
Mkuu wa wilaya, Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Ilemela Batane amesema kuwa
kupitia ukaguzi wa kiafya uliofanyika tarehe 13/02/2013 na kufanywa na maofisa
Afya kutoka manispaa na kata husika madhaifu mengi yalibainika na hayajafanyiwa
kazi kama ilivyoshauriwa suala ambalo ni kinyume cha sheria ya Afya ya jamii
no. 1 ya mwaka 2009.
.
Mkuu wa Wilaya Masenza baada ya
kupewa taarifa hiyo na maafisa wa afya na elimu wa Manispaa ya Ilemela wakati
alipofanya ziara ya kushitukiza shuleni hapo kwa lengo la kujionea hali halisi
ikiwa ni pamoja na kujionea mazingira wanayoishi wanafunzi wa bweni na
msongamano uliopo ndani ya vyumba vya madarasa na mabweni ya kulala endapo
uongozi wa shule hiyo ulifanya marekebisho na kutekeleza kama ilivyoshauriwa na
wataalamu Idara husika.
Kufatia hatua hiyo akizungumza na
uongozi wa shule hiyo chini ya Mkurugenzi na mmiliki wa shule hiyo Dkt.Andrew Masambala
na mbele ya wanafunzi,Masenza alisema nimesikitishwa na hali niliyoikuta na
viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ni mbaya na hivyo amefika
kujionea na kwa mazingira nasikitika kuona uongozi kushindwa kufuata taratibu
na mashariti ya uanzishaji wa shule na hata zile za mazingira na afya.
“Naagiza Idara zote husika kuifungia
mara moja shule hii na siko tayari nikiendelea kuwaona watoto wakiishi
mazingira kama ya wahamiaji halamu wanaokuwa wameingia nchini kwa njia za panya
na kuhifadhiwa kwa kufichwa vichakani na wakilala kwa mbanano huku wadudu
wakiwang’ata na wengine kupata maradhi na ugonjwa wa maralia hivyo natangaza
rasimi kuifunga shule hii”alisisitiza.
No comments:
Post a Comment