Afisa Elimu mkoa wa Dar
es Salaam Raymond Mapunda (kushoto) akimkabidhi hivi karibuni katika ukumbi wa
Karimjee zawadi ya redio (music sytem) Winfrida Leonard kutoka shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA
– Nakayama iliyopo Rufiji mkoani Pwani ambaye alishika nafasi ya tatu katika
mashindano ya kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa
Tanzania. Mashindano hayo yaliandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania
waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) ambapo jumla ya wanafunzi 32 kutoka
shule nane walishiriki.
Faiza Ussi kutoka shule ya Sekondari ya
Sunni Madressa ya mjini Zanzibar alifurahia zawadi ya laptop aliyopewa hivi
karibuni katika ukumbi wa Karimjee mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika
mashindano ya kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa
Tanzania. Mashindano hayo yaliandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania
waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) ambapo jumla ya wanafunzi 32 kutoka
shule nane walishiriki
Washindi
kumi walioshiriki shindano la kuandika
insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja
wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) wakiwa katika picha ya pamoja hivi karibuni
katika ukumbi wa Karimjee na baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla
hiyo. Wanafunzi 32 kutoka shule
nane walishiriki katika mashindano hayo
yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza ambapo mshindi wa kwanza alipata laptop
yenye thamani ya dola 600 za kimarekani
No comments:
Post a Comment