MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Wednesday, March 20, 2013

TUME YA KUCHUNGUZA CHANZO CHA KUSHUKA KWA KIWANGO CHA UFAULU WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2012 YAABAINI MATATIZO

Profesa Sifuni Mchome

 Uhaba wa walimu, vitabu, umbali zilipo baadhi ya Shule, majengo ni baadhi ya vitu ilivyovibaini Tume ya kuchunguza chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012
 akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam ,mwenyekiti wa Tume hiyo alisema hayo ni mambo ya mwanzo yaliyobainika baada ya kufanya uchunguzi katika Shule zilizopo jijini Dar es Salaam, aliongeza kwa kusema kuwa wamezungumza na wadau mbalimbali wa elimu, ikiwa ni pamoja na walimu wa Shule za Sekondari binafsi, wamiliki wa Shule hizo na wengine wengi na baadhi wanachi wa kawaida

Alisema wanaendelea katika mikoa mingine watakapo maliza watatoa ripoti kamili, alisema ripoti hii ya mwanzo ni kwa Dar es Salaam tu

No comments:

Post a Comment