Baadhi ya wafanyakazi wa Mifuko ya Jamii wakiwa na watoto wenye ulemavu wa akili wa kituo cha Miyuji wakati walipokwenda kutoa msaada wa mabati na mbao zilizotolewa na Mifuko hiyo kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa moja ya chumba cha Darasa cha Kituo hicho.
Wakimama waliolazwa katika wodi ya wazazi ya Chikande iliyopo katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma wakisalimiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Mifuko ya Jamii wakati wa kukabidhi msaada ya magodoro 30 na mashuka 100 iliyotolewa na Mifuko hiyo
Baadhi ya wafanyakazi wa mifuko ya Jamii wakikabidhi msaada wa mashuka na magodoro kwa wodi ya wazazi ya Chikande iliyopo katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano SSRA, Sarah Kibonde akiwa na mtoto aliyezaliwa katika Wodi ya wazazi ya Chikande iliyopo katika Hospitali kuu ya Mkoa wa Dodoma muda mfupi baada ya kukabidhi msaada wa Magodoro na Mashuka kwa wodi hiyo
Watoto wanaolelewa katika kituo cha wenye ulemavu wa akili cha Miyuji kilichopo mkoani Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mifuko ya Jamii, GEPF, LAPF, NSSF, PPF, NHIF na SSRA ambao ndiyo wasimamizi wa mifuko hiyo baada ya kutoa msaada wa mbao na bati kwa ajili ya umaliziaji wa moja ya chumba cha Darasa kinachojengwa katika Kituo hicho
No comments:
Post a Comment