Kuanzia tarehe 26 Juni hadi 3
Julai, Rais Obama na Mkewe wanatarajia kutembelea nchi za Senegal, Afrika ya
Kusini na Tanzania. Katika ziara yake hiyo, Rais atawekea mkazo umuhimu ambao
Marekani inauweka katika ushirikiano wetu wa kina na unaoendelea kuimarika na
nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia mipango mbalimbali ikiwemo
ile ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, uwekezaji na biashara, uimarishaji wa
taasisi za kidemokrasia na uwekezaji katika kizazi kipya cha viongozi wa
Kiafrika.
Rais atakutana na viongozi
mbalimbali wa kiserikali, sekta binafsi na jumuiya huru ya kiraia ikiwemo
vijana ili kujadili ubia wetu wa kimkakati katika ushirikano wetu rasmi na
masuala mengine ya kimataifa. Ziara hii itadhihirisha dhamira ya dhati ya Rais
ya kupanua na kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na watu wa nchi za Afrika
Kusini mwa Jangwa la Sahara katika kuimarisha amani na ustawi katika kanda hii
na duniani kote kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment