Alikuwa ni mchezaji wa Kimatifa aliyesajiliwa kutoka Rwanda, Kavubagu aliyewainua mashabiki wa Yanga katika daki ya tano ya mchezo huo kwa kuiandikia bao la kwanza timu yake
Katika mchezo huo kipindi cha kwanza timu ya Simba ilikosa penalti baada ya Mshambuliaji wa timu hiyo Mrisho Ngassa, kuangushwa katik eneo la hatari, penalti hiyo ilipigwa na Musa Mude aliyeipiga kiuchovu ambapo golikipa wa timu ya Yanga, Bartez(Ali Mustapha) aliudaka kiulaini kabisa.
Kipindi cha pili ni yanga tena ndiyo walioendelea na Shamrashara baada ya mchezaji wa kimataifa tena kutoka nchini Uganda, anayejulikana kwao kwa jina la Diego (Hamis Kiiza) alipowanyanyua mashabiki hao kwa kupachika bao la kichwa kutokana na mpira wa adhabu uliorushwa na Beki wa Kimataifa Mbuyu Twite na kuwagonga wachezaji wa Yanga na kumkuta mfungaji aliyeupiga kwa kichwa bila kigugumizi na kutinga wavuni ukimwacha Kaseja hana la kufanya zaidi ya kuusindikiza wavuni
No comments:
Post a Comment