Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lamadi
kwenye Viwanja vya Kisesa wilaya ya Busega mkoa wa Simiyu na kuwaambia
wananchi kuwa muda wa walimu kuendelea kupata tabu umeisha na kuagiza
mamlaka husika kutatua kero na madai ya walimu ndani ya miezi sita na
kama wameshIndwa wajiuzulu kupisha watu wengine.
Kikundi cha Ngoma cha Mwanalyaku Dance Group kikionyesha uwezo wake wa
kucheza ngoma ya bugobogobo ikiwa sehemu ya utangulizi kabla ya kuanza
kwa mkutano wa hadhara wa CCM uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM,
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lamadi
wilayani Busega kwenye Mkutano wa hadhara na kuwaambia wananchi wawe
makini na makanjanja wa kisiasa ambao kwa sasa wamefunga ndoa batili
kutaka kuvuruga mchakato wa kupata Katiba mpya.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya akizungumza katika Mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye viwanja vya Kisesa, Lamadi na kumuambia Katibu Mkuu
wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana maji bado ni tatizo kwa wakazi wa wilaya
yake.
Kikundi cha Kwaya cha akina mama kinachofahamamika kwa jina la Chui
kutoka Nyamajashi kikitumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye viwanja vya Kisesa,Lamadi wilaya ya Busega.
No comments:
Post a Comment