Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma , George Yambesi akifungua mafunzo kwa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara .
Sehemu ya washiriki wa mafunzo wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma George Yambesi.
Mmoja kati ya washiriki, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimajanro Dk. Faisal Issa akizungumza kuhusu mafunzo hayo, na kutoa shukrani.
Makatibu Tawala wa Mikoa na
Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wametakiwa kuhakikisha matatizo ya
mishahara kwa watumishi yanamalizika mara moja
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuhusu Mfumo Shirikishi wa Taarifa za
Kiutumishi na Mishahara (HCMIS). Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Mejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi alisema malalamiko ya watumishi
kuhusu malipo ya stahili zao kwa wakati yamepungua, pia kudhibiti eneo la
mikopo kwa watumishi kwa kuhakikisha makato kwa ajili ya mikopo hiyo hayavuki
theluthi mbili za mishahara yao.
“Mtakua mmetoa mchango
mkubwa katika eneo hili kama kila mtumishi atakuwa na taarifa sahihi kwa
kutumia mfumo huu ili taarifa hizo ziweze kutumiwa kufanya maamuzi sahihi
katika eneo la usimamizi na matumizi bora ya watumishi” Ka Yambesi
alisema na kuongeza mafunzo hayo yamelenga ufahamu wa mfumo, mahitaji maalum
kwa uendeshaji na usimamizi katika ngazi ya waajiri.
Mafunzo hayo yalikuwa mahususi kwa Makatibu Tawala na wakurugenzi
Yambesi aliainisha kuwa
lengo la mafunzo hayo ni kutekeleza au kufanya maamuzi ya kiutumishi kwa weledi
unaotakiwa na kwa kufanya hivyo washiriki hao wa mafunzo watakuwa wameshiriki
kutoa mchango wao katika mabadiliko yanayoendelea kwa maendeleo na ustawi wa
Taifa kupitia huduma mbalimbali zinazotolewa.
Katibu Mkuu aliwaelekeza
baada ya kuelewa mfumo wa HCMIS unavyofanya kazi na taarifa muhimu zinazoweza
kutolewa na mfumo huo watafakari namna ya kuufikisha mfumo huo katika maeneo
yao ya huduma mfano katika sekta za Elimu, Afya, Kilimo na Mifugo.
Yambesi aliongeza pia ni
vizuri kutafakari namna mfumo huo utakavyoweza kutumika kuimarisha usimamizi
katika maeneo mengine ya malipo ya stahili za watumishi kama vile madai ya
likizo, matibabu na mafunzo ambayo yanaendelea kukua bila udhibiti wa kutosha
hivyo mfumo kutumika kupata sulushisho kwa madai mengi ya watumishi
yanayojitokeza.
Kwa kutumia mfumo huu
mtaweza kufanya maamuzi mbalimbali na kusimamia watumishi walio chini yenu kwa
kuimarisha uwajibikaji na kupunguza muda mwingi mliokuwa mnatumia kupata
taarifa za kiutumishi kwa ajili ya kufanya maamuzi, pia kuwa na taarifa sahihi
na kwa wakati kuhusiana na utekelezaji wa maagizo mnayotoa.
Mfumo wa HCMIS ulianzishwa
mwaka 2010 ukiwa na lengo la kuimarisha usimamizi wa rasilimaliwatu na mishahara
katika utumishi wa Umma kwa kuhakikisha watumishi wanaingizwa kwenye orodha ya
malipo ya mishara (Payroll) kwa wakati,
mishahara na cheo cha mtumishi kinabadilishwa kwa wakati anapopandishwa cheo,
kuepuka malimbikizo makubwa ya muda mrefu ya mishahara ya watumishi, watumishi
wanaondolewa kwenye orodha ya malipo kwa wakati, na pia serikali inakuwa na
taarifa sahihi za watumishi na kuzitumia kufanya mipangilio ya rasilimali na
mishahara.
No comments:
Post a Comment