MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Thursday, October 3, 2013

TAMASHA LA UTAMADUNI KUFANYIKA DEC 14 WILAYANI HANDENI MKOANI TANGA


 
 RAHA Company and Entertainmen wameanda Tamasha la Utamaduni linalotaraji kufanyika Wialyani Handeni mkoani Tanga mwezi Desemba mwaka huu.
 
 Akizungumza mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana amewaomba wadau mbalimbali wa masuala ya Utamaduni na michezo kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha Tamasha hilo ambalo ni kwanza kufanyika katika Wilaya ya Handeni.
 
Mratibu wa Tamasha la Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga, Kambi Mbwana, pichani.

 
Akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo, Mbwana alisema endapo wadau wote, wakiwamo wafanyabiashara na wamiliki wa kampuni, taasisi za serikali watashirikiana katika hilo, mambo yatakuwa mazuri.

Alisema hali hiyo inamfanya aone haja ya kuwataka watu hao washirikiane kwa pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tamasha la utamaduni na michezo Handeni linafanyika kwa mafanikio na kuweka historia mpya.

“Watu wote wana umuhimu katika kufanikisha kwa tamasha hili, hivyo kila mmoja kwa nafasi yake tunaomba msaada wake hata wa kimawazo, ukizingatia kuwa kinachofanyika kwa sasa ni kuachiana majukumu tu.

“Tunawaomba wote wenye moyo wa kufanikisha wazo hili tushirikiane nao kwa namna moja ama nyingine, hasa kwa kuona wenye kampuni zao, mashirika na taasisi za serikali pia kutudhamini katika hili,” alisema Mbwana.

Kwa mujibu wa Mbwana, kufanyika kwa tamasha hilo kutakuwa ni sehemu nzuri ya kuwakutanisha wadau, wananchi wa Handeni na Tanzania kwa ujumla kwa ajili ya kujadiliana changamoto zinazowakabili kwa maendeleo yao.

Tamasha hilo la Utamaduni linaandaliwa chini ya Raha Company and Entertainment huku likifanyika kwa mara ya kwanza katika wilaya hiyo inayoongozwa na Mkuu wake wa Wilaya Muhingo Rweyemamu, wakati mbunge ni Dk Abdallah Omari Kigoda ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara.


No comments:

Post a Comment