MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Thursday, February 6, 2014

WAFANYAKAZI WA TRL WATAKA SERIKALI IWAPANDISHIE MSHAHARA

WAFANYAKAZI wa Shirika la Reli Tanzania (TRL)   wameitaka serikali   kuwapandishia mishahara kutoka 205000  ya sasa hadi 300,000 ifikapo february 28 mwaka huu, kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (Trawu), Shehe Shughuli, wakati wa mkutano na viongozi wa TRL waluiokuwa wamekuja kujibu maswali kuhusu namna ya kuongeza mishahara hadi kufikia kima cha chinin cha serikali.

 Akijibu maswali hayo Naibu Mkurugenzi wa TRL, Mhandisi, Elias Mshana, alisema suala hilo wameshalishughulikia katika ngazi kuu na serikali imeahidi kutimiza katika bajeti ijayo ya mwaka 2014 na 2015.

Mhandisi Mshana, alisema TRL haina uwezo wa kuwalipa wafanyakazi kiasi ambacho wanakihitaji lakini wameomba fungu serikalini kwasababu kima cha chini cha serikali ni shilingi 240,000 na Taasisi hiyo inatambaulika kam a ni ya serikali hivyo wameamua kuomba shilingi 300,000.

“Awali serikali ilitangaza kima cha chini cha wafanyakazi kuwa ni 240000 lakini TRL bado wafanyakazi walikuwa hawajaongezewa mshahara hivyo kuwafanya wasue sue na kunung’unika lakini katika bajeti ijayo tushakubaliana na serikali tutawaongezea,” alisema Mshana
Mwenyekiti wa Trawu alimjibu Mshana kwamba wafanyakazi hawapo tayari kusubiri hadi bajeti ijayo wakati serikali imetangaza kuongezewa mshahara kabla ya bajeti hiyo.
“Wafanyakazi tunakufa njaa hatuwezi kusubiri hiyo bajeti mwisho wa mwezi huu tunaomba mshahara uwe umershapanda la sivyo tutajua la kufanya, tumechoka kudharauliwa na serikali,” alisema mmoja wa wafanyakazi hao



No comments:

Post a Comment