MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Monday, July 14, 2014

NAIBU WAZIRI WA MAJI AMOS MAKALLA ASITISHA SHUGHULIZA UFYATUAJI WA MATOFALI KWENYE VIWANDA VIWILI JIJINI DARE ES SALAAM BAADA YA KUBAINIKA VIWANDA HIVYO KUTUMIA MAJI YA WIZI KUTOKA DAWASCO

Naibu Waziri Wa Maji, Amos Makalla, akizungumza eneo la Kimara, DaresSalaam baada ya kukamatwa kwa wezi wa Maji wanayoyatumia kufyatulia Tofali.
Naibu Waziri Amos Makalla,  akizungumza eneo ambalo lilibainika kuna Bomba limekatwa na kutumika kuiba Maji kutoka kwenye Bomba Kuu la Dawasco

 VIWANDA VIWILI VYA KUFYATU TOFALI VYAPIGWA STOP





Naibu Waziri wa Maji, Amos  Makalla amesitisha shughuli za ufyatuaji Tofali kwa viwanda viwili jijini , DaresSalaam baada ya kubainika vinatumia Maji ya wizi


Makala aliagiza shughuli hizo kustishwa mara moja  katika Viwanda  vya  Kampuni ya Ujenzi ya Solution cha Kimara jijini, DaresSalaam kilichokuwa kinazalisha matofari1000 kwa siku na kile kilichopo karibu na Ofisi zaWizara ya Maji kijulikanacho kwa jina la Moto Company


 Naibu waziri alivibaini viwanda hivyo kwamba vinatumia Maji ya Wizi ya Dawasco wakati wa ziara ya siku tatu aliyoianza leo ya kutembelea Vyanzo vya Maji na kukagua Matenki ya kuhifadhia Maji na miradi inayomilikiwa na Dawasa


Makalla alisema Shughuli zote za ufyatuaji Tofali lazima zisimame kutokana na wamilikikutumia Maji yasiyolipiwa na kuunganishwa kienyeji kitendo ambacho ni wizi na wanafaa kuchukuliwa hatua za kisheria

No comments:

Post a Comment