Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Mvomero (CCM), Amos
Makala, amezindua vituo vya kuchota maji katika vijiji vya cha Mgogo, Kata ya
Sungaji, Kijiji cha Mlali na Kipera vilivyopo katika jimbo hilo lililopo mkoani
Morogoro
Makalla alizindu vituo hivyo akiwa katika ziara ya siku tano
katika jimbo iliyolenga kuhamasisha shughuri za maendeleo ya wananchi wa vijiji
vya Tarafa ya Mlali, Turiani na Mvomero
Mbali na hayo Naibu Waziri, Amos Makalla aliweza kukabidhi misaada
mbakimbali kwa kutoa misaada ya kifedha
kwa vikundi vya akina mama wajasiliamali, vijana , taasisi za dini na
ujenzi wa Ofisi za Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kata na Matawi ya
wananchi ya vijiji hivyo.
Pia misada mingi aliyoikabidhi kwa wananchi hao ya kifedha ilielekezwa kwenye sekta ya
elimu katika kusaidia uendelezaji wa ujenzi majengo ya vyumba
vya madarasa kwa Shule za awali na
mikondo ya darasa la kwanza kwenye vijiji vilivyopo kwenye
Tarafa hizo kufuatia wananchi kuonesha nguvu zao wakiwa na lengo la kuwaondolea
adha watoto wao wanaotembela umbali mrefu kwenda shule.
Pia akiwa katika Mji Mdogo
wa Dawaka aliweza kukabidhi msaada wa vyakula wa tende katoni 50 na mchele
tani 1.5 kwa ajili ya waumini wa dini ya kiislamu ambao wapo kwenye mfungo wa
mwezi mtukufu wa Ramadhan wilaya huo.
Makalla alifanya ziara hiyo ya siku tano kuanzia tarehe 3 hadi 7 kwenye jimbo la Mvomero ikiwa ni
mfululizo wa ziara zake katika jimbo hilo kwa ajili ya kuzungungumza na
wananchi wa jimbo hilo
No comments:
Post a Comment