MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Tuesday, July 15, 2014

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUMALIZA TATIZO LA MAJI KOTE NCHINI

 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushoto) akizungumza na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, wakati wa kukagua Matanki ya kuhifadhia Maji eneo la Kimara Jijini, Dar es Salaam, hata hivyo matanki hayo yatabomolewa na kujengwa upya katika miradi ya Maji inayoendelea kujengwa.


 Naibnu Waziri wa Maji, Amos Makalla akitoka katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kibamba, Dar es Salaam jana

 SERIKALI KUMALIZA TATIZO LA MAJI

Serikali imesema itahakikisha miradi ya Maji inayojengwa kutoka Ruvu na chini yote ina kamilika septemba mwakani

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla katika siku yake ya pili ya ziara ya kukagua miardi ya na Maji na Vyanzo vyake vinavyomilikiwa na Shirika la Maji Taka na Safi Dar es Salaam (Dawasa)

Awali akiwa katika Shule ya Msingi Mavurunza iliyopo kata ya Mavurunza katika Jimbo la Ubungo, nusura Mkutano wa hadhara uvunjike kwa kile kilichoonekana ni ushabiki wa kisiasa kati  ya wanachama wa Chama  Cha Mapinduzi (CCM) na wa Chama Cha Demokrasi na Maerndeleo (CHADEMA) waliokuwa wanabishana wakati viongozi wakizungumza akiwemo Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika

Makalla aliendelea kwa kusema, Serikali imekwishatenga pesa kwa ajili ya miradi hiyo ambayo miradi yote hiyo itagharimu sh milioni Bilioni 397

 Alisema kama miradi hiyo itakamilika lazima tatizo la maji kwa wakazi wa Jimbo la Ubungo na Dar es Salaam kwa ujumla litapungua kwa kiasi kikbwa sana kama siyo kumalizika kabisa

Naye Mbunge wa Ubungo   John Mnyika aliwasihi wananchi kwamba miradi hii inayotekelezwa ni ya wananchi wote wala haiangalii  kichama wala kisiasa.

Naibu Waziri wa Maji kesho ataendelea na ziara yake kwa siku ya tatu kwa kuendelea na kukagua miradi mablimbali ya Maji inayojengwa jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment