MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Tuesday, September 9, 2014

RAIS AKAGUA VIFAA VYA KUBAINI WENYE EBOLA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE DAR ES SALAAM

Rais Jakaya  Kikwete akipata maelezo ya jinsi vifaa maalumu vinavyofanya kazi ya kutambua wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo ya namna ya kuhudumia abiria wakati wa ukaguzi wa wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi madaktari na wauguzi walivyo jiandaa kufanya ukaguzi wa abiria na kutambua wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wauguzi waliovalia mavazi maalumu tayari kutoa huduma kwa  abiria  atayekutwa na ugonjwa wa ebola  mara atapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam

Baadhi ya wahudumu waliovalia mavazi maalumu wa  wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaangalia wahudumu waliopata mafunzo maalumu ya kumhudumia mgonjwa wa ebola wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam leo

No comments:

Post a Comment