MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Thursday, October 16, 2014

TAARIFA YA UKAGUZI MAALUM WA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW (UKAGUZI WA IPTL)

Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inapenda kuujulisha Umma kuwa Ukaguzi Maalum wa akaunti ya Tegeta Escrow ambao unafahamika kama Ukaguzi wa IPTL unaendelea na unaongozwa na Hadidu za Rejea (ToR) zilizotolewa na kisha kuridhiwa na Ofisi ya Bunge na Wizara ya Nishati na Madini.

Ukaguzi wa akaunti ya Tegeta Escrow uliombwa na Katibu wa Bunge na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini. Ukaguzi huu unalenga kufanya uchunguzi wa kina ambao utatoa taarifa kamili yenye kuonesha hali halisi kuhusu miamala (transactions) kwenye akaunti maalum ya Tegeta Escrow kisha kutoa taarifa kuhusiana na ukaguzi huo.

Kwa kuwa Hadidu za Rejea pekee haziwezi kuonesha ukubwa wa kazi bali utekelezaji wa kazi yenyewe ndio unaoweza kutoa taswira halisi, ni vyema umma wa watanzania ukatambua kuwa Ukaguzi huu haujaweza kukamilika kwa kipindi kilichokadiriwa awali hivyo ukaguzi unaendelea kwa kuzingatia Hadidu za Rejea na kifungu cha 29 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya mwaka 2008.

Aidha, ongezeko la muda wa kukamilisha ukaguzi huu limetokana na uhitaji wa kukusanya maelezo yanayoendana na vielelezo vinavyojitosheleza ili kumsaidia mkaguzi kufikia malengo ya ukaguzi huo. 

Imetolewa,
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

No comments:

Post a Comment