MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Sunday, June 28, 2015

JANUARY MAKAMBA ADHAMINIWA NA WANACCM 600 MKOANI MANYARA


Mbunge wa Bumbuli na naibu waziri wa mawasilano, sayansi na teknolojia, January Makamba akisalimiana na wananchi na wananchama wa CCM mkoa wa Manyara waliojitokeza katika viwanja vya ofisi za CCM mkoa wa Manyara kumuunga mkono katika harakati zake za kusaka wadhamini mkoani hapo. 





Makamba akisalimiana na wananchi na wananchama wa CCM mkoa wa Manyara waliojitokeza katika viwanja vya ofisi za CCM mkoa wa Manyara kumuunga mkono katika harakati zake za kusaka wadhamini mkoani hapo. January amejizolea wadhamini 600 kutoka mkoa huo.




Mbunge wa Bumbuli na Naibu waziri wa mawasilano, sayansi na Teknolojia, January Makamba akimnyanyua juu mtoto kwa furaha aliyekuja kumsikiliza katika viwanja vya ofisi za CCM mkoa wa Mayara wakati alipowasili mkoani hapo kwa ajili kuomba udhamini wa wanachama kumuwezesha kuteuliwa na chama kugombea nafasi ya urais.


Mbunge wa Bumbuli na naibu waziri wa mawasilano, sayansi na teknolojia, January Makamba akiteta jambo na Katibu wa CCM mkoa wa Manyara, Mzee Ndekubale walipokuwa katika mkutano na wananchi pamoja na wanachama wa CCM mkoani Manyara.
 


 Mbunge wa Bumbuli na Naibu waziri wa Mawasilano, sayansi na Teknolojia, January Makamba akifurahia jambo kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Babati Mjini (kushoto) wakati wa mkutano na wanachama wa CCM mkoa wa Manyara. 
.
 Makamba akiwa na Mkewe Ramona, mkoani Manyara


January Makamba akihutubia wananchi na wanachama wa CCM mkoani Manyara waliojitokeza katika Viwanja vya CCM mkoani hapo . January yupo katika ziara yake ya kutafuta wadhamini ndani ya chama ambao watamuwezesha kuteuliwa kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM. Ambapo mkoani Manyara amepata wadhamini 630.


Mbunge wa Bumbuli na Naibu waziri wa mawasilano, sayansi na teknolojia, January Makamba akiagana na  wananchi pamoja na wanachama wa CCM mkoa wa Manyara  baada ya kumaliza kuzungumza nao na kupata wadhamini 630 mkoani humo

No comments:

Post a Comment