MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Friday, March 11, 2016

LOWASSA AMJULIA HALI MAALIM SEIF

 Aliyekuwa mgombe urais kupitia Chadema, Edward Lowassa akimsalimia, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF Seif Sharif Hamad katika Hotel ya Serena , Dar es Salaam. Picha na Amanitanzania blog

Aliyekuwa mgombea urasi kupitia chama cha Chadema akiwakilisha UKAWA, katika Uchaguzi Mkuu 2015, Edward Lowassa leo amemtembelea  na kumjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad katika Hotel ya Serena, Dar es Salaam

Akizungumza baada ya kutembelewa na Lowassa Maali Seif Sharif Hamad alisema hali yake inazidi kuimarika na kwamba anaendelea vizuri kwa hiyo wananchi wasiwe na wasiwasi

Alipoulizwa na waandishi wa habari kama kuna chochote walichojadili kuhusu uchaguzi wa zanzibar alipotembelewa na Rais John Magufuli  na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein yeye alisema hakuna walichozungumza kuhusu uchaguzi wa Zanzibar isipokuwa walikuja kumuona tu

No comments:

Post a Comment