MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Thursday, November 30, 2017

Kampuini ya Airtel Tanzania yakabidhi simu kwa jeshi la zimamoto kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano kwa Jeshi hilo



Kamishna Generali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akizungumza wakati wa mkutano na  waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  baada ya kupokea msaada wa simu za mkononi kutoka Kampuni ya Airtel Tanzania zitakazotumika kuimarisha mawasiliano ndani ya jeshi hilo kupitia namba ya dharura 114. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano.



Kamishna Generali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akipokea baadhi ya simu za mkononi ambazo zimetolewa na Airtel Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano kupitia namba ya dharura 114 ndani ya jeshi hilo. Simu hizo zitasaidia wananchi wote kutoka mitandao yote watakapopiga katika namba ya dharura 114 na kuhudumiwa kwa haraka. Habari na Picha kwa hisani ya Airtel Tanzania

Kampuni ya Airtel Tanzania imekabidhi msaada wa simu kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambazo zitatumika kwa ajili ya kurahisisha na kuimarisha mawasiliano ya namba ya dharura 114 wakati wa kuripoti dharura za moto na majanga mbalimbali nchini.
Simu hizo zimetolewa kwa mikoa maalumu ya Jeshi la Zimamoto ambapo wateja wa Airtel watapiga bure ili kupata huduma za jeshi hilo.
Akikabidhi simu hizo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya alisema wao kama Airtel wanatambua umuhimu wa Jeshi hilo na wanaamini kuwa wananchi sasa wataweza kupata huduma za Jeshi hilo kwa urahisi kupitia namba hiyo ya dharura.
“Airtel tunatambua umuhimu wa jeshi la zimamoto na uokoaji katika jamii,hivyo tunaamini utoaji wa taarifa za majanga kwa wakati muafaka unarahisisha shughuli za uokoaji na kuzuia kwa kiwango kikubwa hasara ambayo inaweza kusababishwa na majanga hayo katika jamii.
 Alisema kupitia namba hii ya dharura ya 114 na kwa uwezeshaji wa kuitumia kwa urahisi na uhakika, Jeshi la Zimamoto litaweza kuwahudumia wananchi kwa haraka wakati wa moto na majanga yanapotokea.
Alisema Airtel itaendelea kushirikiana na Jeshi hilo ili kuhakikisha mawasiliano yanafanyika kwa urahisi na haraka ili kulisaidia jeshi la zima moto kuweza kuwafikia wananchi wengi Zaidi kote nchini na kuepusha hasara zinazoweza kutokea wakati wa majanga ya moto na kadhalika.
“Tunataka kuwahakikishia wateja wetu wote kuwa mtandao wa Airtel uko imara kwa kuwa hivi karibuni tumeboresha zaidi mtandao kwa kutumia teknolojia mpya ya U900 katika baadhi ya mikoa ikiwemo hii inayofaidika na huduma ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, hivyo basi tunawaomba muitumie namba hiyo ya dharura vizuri huku pia mkifaidi huduma zetu bora za Airtel ,” alisema.  
Mikoa iliyopokea simu hizo ni pamoja na Ilala, Kinondoni, Temeke, Pwani, Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Mwanza, Mara, Shinyanga, Tabora, Simiyu, Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Rukwa, Ruvuma, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Tanga, Mtwara, Lindi, Singida na Bagamoyo.



No comments:

Post a Comment