MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Monday, December 3, 2012

Kilimanjaro Stars yatinga Nusu Fainali ya Chalenji

Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, Mrisho Ngassa akishangilia kwa staili ya aina yake baada ya kumalizika kwa mchezo wa Robo Fainali ya kwanza dhidi ya Rwanda uliochezwa katika Uwanaj wa KCC uliopo Lugogo, nchini Uganda jana. Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya TBL iliweza kuibuka na ushindi wa goli 2-0. goli la  kwanza likiwekwa kimiani na Amri Kiemba kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Mwinyi Kazimoto aliyeambaa na mpira upande wa kushoto na kufanikiwa kwapita mabeki wa timu ya Rwanda na kutoa pasi iliyomkuta mfungaji, Goli la pili lilifungwa na John Boko baada ya kupiga shuti na kipa wa Uganda, Jean Claude Ndori kutuema mpira ndipo alipomalizia mpira huo na kutinga wavuni.

No comments:

Post a Comment