Kwenye jengo hili tunaweza kusema hivyo maana ni kwamba sehemu hii inatumiwa na watu ambao baadaye tukiwa na uhai wanaweza kuwa watu muhimu sana kwa Taifa hili la Tanzania hata katika nchi nyingine za Afrika na Duniani
Nasema hivyo kwa maana moja tu kwamba ni sehemu ambayo baadhi ya vijana, watoto wetu wanapata kujifunza masomo ya ziada kwa maana nyingine Tution, yaani ni baada ya kusoma masomo ya kawaida Darasani na kuongezea pale ambapo labda Mwalimu hakuelweka vizuri, hapo ndipo mwanafunzi anaweza kupata fursa zaidi ya kuuliza
Haya mazingira si ya Shule ya Msingi hapana hii ni sehemu tu mtu kaamua kuanzisha ili aweze kutoa mchango wake kwa wanafunzi kwa malipo
Mazingira haya yapo karibu na Shule ya Msingi Mchikichini Ilala Dar es Salaam, lakini cha kushangaza ni kwamba maeneo hayo yamegeuka siyo sehemu ya kujifunza masomo bali kuna vitendo viovu vinaendela ambavyo vinaweza kusababisha vijana wetu wanaokuwa na malengo ya kujifunza na kutumbukia katika mambo ambayo hayaendani na kile kilichowapeleka
sehemu hiyo wanakutana watu mbalimbali ambao si wanafunzi, na wenye shughuri mablimbali kwa siyo rahisi mwanafunzi akatekeleza vizuri kile kilichompeleka pale huku kukiwa na muingiliano wa wtu mablimbali.
No comments:
Post a Comment