Ndugu zanguni
Kwanza kabisa napenda
kuelezea masikitiko yangu juu ya tukio lililomkuta Mwandishi mwenzangu
veteran wa tasnia hii Kassim Mikongoro. Nampa pole sana kwa sababu
yaliyomkuta katika ghasia za Mtwara sio tu yamempa hasara ya Mali bali
pia yamemuathiri kisaikolojia yeye na familia yake. Niwe mkweli hata
mimi nimeathirika kisaikolojia kutokana na tukio lilimkuta Kassim. Na
kwa mara nyingine Pole sana Kassim.
Haya yamemkuta Kassim
lakini mimi naamini yanaweza kumkuta mwandishi wa habari mwingine
yeyote, nasema hivi kwa sababu nina shauku ya kuamsha mjadala
utakaosaidia kuangalia mustakabali wa waandishi wa habari katika
usalama wao na familia zao. Najua kwa yaliyomkuta Kassim kila mtu
anaweza kusema la kwake lakini ni vizuri kukumbushana kuwa tukiweka
kando hisia hizo zote Kassim ni mwandishi wa habari kama alivyo
mwandishi wa habari mwingine yeyote.
Nionavyo mimi swali hili
tunapaswa kujiuliza sote wadau, nikiwa na maana waandishi wa habari
wenyewe, wamiliki wa vyombo vya habari, wahariri wa habari, mamlaka za
kiserikali na wananchi ambao tunawahudumia. Kwa namna yoyote ile si
haki kuwashambulia waandishi wa habari, tena wasihukumiwe kienyeji
namna hiyo. Tukifikia hapo na kwa kuwa Mhimili wetu sio rasmi basi
naona huku mbeleni itakua kila asiyeridhishwa na kazi zetu anatuadhibu
kwa namna alivyoadhibiwa Kassim. Atabaki nani?
Ni vizuri tulijadili
hili kwa weledi na busara na wananchi wajue tuna maana gani. Mimi ni
miongoni mwa waandishi wa habari walikutana na mikutuo ya kutishiwa,
wakati mwingine kushambuliwa na hata kupigwa kutokana na kazi ya
uandishi wa habari. Nakumbuka wakati nasoma chuo kikuu Mwalimu wangu
aliwahi kuniambia kuwa siku zote Ukiandika habari hasa yenye sifa na
mvuto wa kuwa habari wapo utakaowafurahisha na wapo utakaowakwaza.
Nilivutiwa sana na somo hili na nikajiridhisha pasipo mashaka kuwa
kumbe kwa waandishi wa habari kukwaza watu kila siku ni sehemu ya
maisha yetu katika kazi hii. Matharani ukiandika habari juu ya mpango
mzuri wa kuwawezesha wakulima kuzalisha chakula cha kutosha kwa namna
yoyote utakua umewafurahisha wakulima lakini pia utakua umewakwaza
wafanyabiashara ambao biashara zao zinategemea wakulima wakose chakula
cha kutosha ili wao waingize chakula kutoka nje ya nchi na wapate
mapesa lkuki ya faida. Hali kadharika ukiandika habari inayohimiza nchi
kuishi kwa amani utakua umewafurahisha wanaopenda amani na utakua
umewakwaza wanaotamani amani ipotee ili mipango yao ifanikiwe. Ipo
mifano mingi. Yaliponikuta ya kushambuliwa wakati nikifanya kazi ya
kuripoti hali ya vituo vya kura kuwa shwari baada ya zoezi la upigaji
kura ilihali kuna watu walitaka kusiwe na amani kengele iligonga kuwa
hizi ndio changamoto za uandishi wa habari.
Sasa mimi najiuliza
swali hivi kama kila mtu ambaye hafurahishwi na habari zetu atachukua
jukumu la kutushambulia kama ilivyokua kwa Kassim Mikongoro, atabaki
nani?
Saa chache baada ya
nyumba ya Kassim Mikongoro kuchomwa moto, nimeongea nae kwa njia ya
simu, nilishindwa kujizuia na machozi yamenitoka pale kaka yangu huyu
ambaye ametumikia kazi hii kwa karibu miaka 40 tena kwa habari,
vipindi, makala na ripoti nyingine mbalimbali za kuelimisha wananchi
juu ya maendeleo yao ya Kilimo, ustawi wa jamii nakadharika
aliponiambia kuwa yaliyomkuta yamesababisha aanze kufikiria kuanza
maisha upya kwa sababu kila kitu kimeteketea kwa moto na nilipokua
nikizungumza nae ameniambia amebakiwa na pensi na shati moja tu
alivyovaa. Imeniuma saaaana saaaana.
Ikaniuma zaidi
aliponithibishia kuwa kwa kuwa alijua kuwa ajenda ya gesi imekaa
vibaya, katika ripoti zake aliepuka kujihusisha na habari zinazohusiana
na gesi. Kwa kuwa alijua hatakua salama endapo atajihusisha na jambo
hili. Sijajua waliomhukumu walitumia vigezo gani na wamemhukumu kwa
kosa gani Kassim, mtu ambaye amekua mstari wa mbele kuwapigania
wakulima wa korosho wa Mtwara, kupigania hali mbaya ya miundombinu ya
Mtwara, aliyetengeneza makala kadhaa za kutangaza fursa za Mtwara,
ambaye amekua tayari kufanya kazi Mtwara mahali ambako waandishi wa
habari wengi hukataa kupangwa huku kufanya kazi kutokana na changamoto
za maisha za Mtwara. Siwezi kusema yote hapa. Ila itoshe kusema POLE
SANA KASSIM MIKONGORO.
Anyway wadau tuliangalie hili.
Na kwa wakati huu naomba
tusisite kumchangia mwenzetu Kassim Mikongolo ili maisha yake
yaendelee, tumchangie fedha Jamani na napendekeza tuwe na utamaduni huu
ili tutiane moyo kwa kuwa usalama wa waandishi wa habari katika nchi
yetu umejaa maswali mengi. Na tukumbuke nchi yetu inatajwa kushika
nafasi ya tatu barani Africa kwa waandishi wa habari kuwa hatarini
Pole sana Kassim, nipo na wewe katika wakati huu Mgumu and Please be strong brother.
No comments:
Post a Comment