MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Thursday, July 25, 2013

BENKI YA DUNIA YAIPA CHANGAMOTO AFRIKA


Benki ya  Dunia imetoa changamoto kwa nchi za Afrika  kuhimiza maendeleo endelevu ya  ardhi  ili kupunguza umaskini na kujiletea maendeleo.
Ripoti ya Benki hiyo iliyotolewa Julai 22, 2013  imeeleza kuwa ingawa nchi za Afrika ina karibu nusu ya eneo la ardhi nzuri  ambayo haijaendelezwa kwa kilimo, bara hilo limeshindwa  kuiendeleza ardhi hiyoinayokadiriwa kuwa hekta milioni  202 kujikwamua katika umaskini, kuleta maendeleo ya uchumi,kuongeza nafasi za kazi na kulleta mafanikio kwa jumla.
Ripoti hiyo inayoitwa  “Kutumia ardhi ya Afrika kwa mafanikio ya pamoja,”  inaeleza kuwa  nchi za Afrika najamii zake zinaweza kabisa kuondoa tatizo la uporaji wa ardhi, kuzalisha mazao ya chakula na kubadilisha  taratibu za usimamizi na umiliki  wa ardhi katika mwongo ujao.Afrika,
Ripoti  hiyo imeeleza, ina kiwango kikukbwa cha umaskini ambapo asilimia  47.5 ya watu wake wana kipato chini ya  dola za Marekani $1.25 kwa siku..

“Licha ya kuwa na ardhi kubwa na utajiri wa madini, Afrika bado ni maskini ,”  anasema  Makhtar Diop, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika.
“Kuboresha usimamiaji wa ardhi ni muhimu kwa maendeleo ya haraka na kutoa nafasi  zaidi kwa waafrika , wakiwemo wanawake ambao ni asilimia 70 ya wakulima wa Afrika ambao wanakwazwa  kumiliki ardhi na sheria za kimila..Hali hii haikubaliki na lazima ibadilike ili waafrika waweze kunufaika na ardhi yao.”

Ripoti hiyo imeeleza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya ardhi ya ardhi haijarasimishwa, hivyo kuwa na hatari kubwa ya uporaji na kuchukuliwa kwa malipo ya chini ya fidia.
Hata hivyo kumekuwa na matumaini ya maboresho  chini ya mipango inayoendelezwa katika nchi za   Ghana, Malawi, Msumbiji,, Tanzania, na Uganda ambapo  mpango wa kutumia  ardhi kwa mafanikio ya pamoja  unaweza kuleta mapinduzi  ya  uzalishaji wa kilimo na uporaji wa ardhi na  kuondoa umaskini wa kutupea Afrika..

Mpango wa kuleta mabadiliko

Ripoti hiyo inapendekeza kuwa Afrika inaweza kufanikiwa kuendeleza ardhi yake  katika kipindi cha muongo ujao kwa::

· Kuwa na mabadiliko  na uwekezaji kurasimisha ardhi  na  maeneo muhimu yanayomilikiwa na watu binafsi.
· Kusimamia taratibu za umiliki za maeneo yaliyovamiwa  na kujengwa  bila mpangilio mijini ambapo wanaishi zaidi ya  watu asilimila 60 barani Afrika.  .
· Kukabiliana na udhaifu wa utawala na rushwa katika mfumo wa  usimamizi wa ardhi katika nchi za Afrika ambao  kwa kawaida unapendelea wakubwa na kuathiri maslahi ya wananchi walio maskini.
· Serikali za Afrika kuwa na dhamira  ya kisiasa  kuhimiza  mabadiliko haya ya ardhi kuvutia raslimali na uwezekezaji wa jamii ya kimataifa. .

Ripoti  hiyo inasema kuwa mpango huo utagharimu  nchi za Afrika  na  washirika wa maendeleo , ikiwemo sekta bianfsi kiasi cha  dola za Marekani bilioni 4.5 

No comments:

Post a Comment