MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Wednesday, April 23, 2014

MASHINDANO YA 16 YA MPIRA WA KIKAPU (BASKETBALL) KUFANYIKA DAR

Mashindano ya 16 ya Mpira wa Kikapu kwa Majiji ya Afrika Kanda ya Tano na Majiji alikwa kutoka Kanda zingine za Afrika yanatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Mashindano yatafanyika:-
Mwezi wa Tano (May)
Tarehe 6 hadi 11
Mwaka 2014

Majiji yanayotarajiwa kushiriki ni Dar es Salaam (wenyeji), Mwanza, Mbeya, Arusha na Tanga kutoka Tanzania.

Nairobi, Mombasa na Kisumu kutoka Kenya.

Kampala na Mukomo kutoka Uganda.

Bujumbura – Burundi na Kigali-Rwanda.

Mogadishu na Hargeisa kutoka Somalia.

Juba na Citizen kutoka Sudani ya Kusini.

Adis Ababa – Ethiopia na Cairo-Misri.

Mashindano ya 15 ya Majiji yalifanyika mwezi May mwaka jana (2013) jijini Kampala; ambapo Jiji la Mukono nchini Uganda lilitwaa ubingwa kwa wanaume na Nairobi walitwaa ubingwa kwa wanawake.

Ni matarajio ya Kamati ya uendeshaji ya Majiji (Intercity Coordinating Committee) na Bodi ya Intercity, kwamba Majiji yote matano ya Tanzania yatakuwa yanajiandaa vyema ili kushiriki na kuhakikisha kuwa ubingwa unabakia Tanzania.

Tunatoa wito kwa utawala wa Jiji la Dar es Salaam kushirikiana na uongozi wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam ili kuitumia fursa hii kulitangaza Jiji na kuwapatia wafanya biashara nafasi ya kuongeza uchumi wao. Pia Halmashauri zote tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni kushiriki katika kuziandaa timu za wanawake na wanaume za Jiji la Dar es Salaam kwa kiwango cha kutwaa ubingwa.

Ingefaa nafasi ya kwanza ya udhamini ichukuliwe na Jiji pamoja na Halmashauri zake tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni na kwa pamoja kuwaalika wafanyabiashara wa Jiji la Dar es Salaam kuwaunga mkono ili shindano liwe zuri na lenye mafanikio makubwa.

Tunatoa wito kwa Utawala wa Majiji ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Tanga kusaidia maandalizi ya timu zao kwa kushiriki moja kwa moja na kwa kushawishi wadhamini wengine kudhamini timu za majiji yao.

Imetolewa na kamati ya uendeshaji ya Majiji ya Africa Kanda ya Tano, Mchezo wa Mpira wa Kikiapu.



No comments:

Post a Comment