MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Friday, April 25, 2014

MSEMAJI WA TIMU YA COAST UNION YA TANGA AACHI NGAZI

MIMI Hafidh Athumani Kido, nikiwa na akili timamu natangaza kutojihusisha na shughuli zote za Coastal Union, hasa usemaji wa klabu hiyo.
Miongoni mwa sababu nyingi zilizonifanya kutangaza uamuzi huo ni sintofahamu iliyozuka ndani ya klabu yetu, kwa taaluma yangu ya uandishi wa habari lazima niwe na msimamo juu ya mambo yanayoendelea kwenye jamii.
Ili niendelee kufanya kazi na klabu hii kwa wakati huu wa misuguano, lazima niwe na upande; kwa maana upande unaounga mkono uongozi ama upande usiokuwa na Imani na uongozi. Lakini mimi nimeamua kutounga mkono upande wowote.
Kwa hivyo basi, ili niwe katika mstari sahihi nimeamua kukaa pembeni nifanye shughuli zangu za uanahabari kwa furaha na amani.

Bado ni mwanachama halali wa Coastal Union Sports Club,  namba yangu ya kadi ni 0013. Nitaendelea kutoa ushauri na kuishabikia klabu

No comments:

Post a Comment