MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Thursday, April 17, 2014

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI BUNGE KATIKA KIVUKO CHA MV KIGAMBONI


Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe wakizungumza na watoto Samir Juma (fulana nyekundu) na Salum Chumu wakiwa katika Kivuko cha MV Magogoni wakivuka kuelekea Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 17, 2014. Watoto hao ambao wanasoma darasa la awali katika shule ya msingi ya Bunge, walipata bahati ya kuketi na viongozi hao waliokuwa wakielekea kuhani msiba wa kada wa CCM Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada



Rais Dk Jakaya  Kikwete akifurahi na watoto Samir Juma (fulana nyekundu) na Salum Chumu wakiwa katika pantoni la MV Magogoni wakivuka kuelekea Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 17, 2014.

Rais  Jakaya  Kikwete akitoa  heshima za mwisho kwa mwili wa kada wa CCM na Mwenyekiti wa Washirika kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada jijini Dar es salaam leo April 17, 2014.

No comments:

Post a Comment