Kiwanda cha Dar
Brew, kimezindua aina mpya ya Bia ijulikanayo kama “Chibuku Super”. Bia hii
inayopatikana katika chupa nzuri naya kuvutia ya plastiki, isiyorudishwa (take
away) ina ujazo wa lita moja na itauzwa kwa bei ya shilingi 1,200/- tu kwa
chupa. Uzinduzi huo uliojawa na burudani zisizo kifani, ilihudhuriwa na
wafanyakazi wa kiwanda hicho, wauzaji wa jumla na rejareja na wageni wengi
waalikwa.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya kiwanda hicho
kilichopo eneo la Ubungo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi mkuu wa Dar Brew Bw.
Kirowi Suma alisema; Leo ni siku ya furaha kubwa sana kwetu Dar Brew na kwa
watumiaji wote wa Bia, kwani tumeweza kuzindua Bia hii mpya ya “Chibuku Super”
ambayo inatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika soko la Bia hapa nchini. Bia
hii imetengenezwa kwa utaalam wa hali ya juu na kwa kutumia mitambo ya kisasa
kabisa, hivyo kuwahakikishia wanywaji Ubora wa hali ya juu. Alisema Suma
Bw. Suma
alisema, Bia hii inatengenezwa kwa kutumia malighafi za hapa nyumbani, ikiwemo
nafaka ya mtama bora toka kwenye ardhi yetu, haya yote yanatupa kila sababu
sisi watanzania kujivunia kilicho chetu na kukumbuka Asili yetu, kwani hii ni
Bia yetu ya asili. Chibuku Super ina kilevi cha asilimia 4, kinachokufanya
uweze kuitumia kwa muda mrefu ukiwa na marafiki, lakini pia inakupa lishe nzuri
kutokana na virutubisho vinavyopatikana katika nafaka zinazotumika kutengeneza
bia hii. Kwa sasa Bia hii itaanza kupatikana katika mikoa ya Dar es salaam,
Pwani, Morogoro na Dodoma, kisha itaenea nchi nzima.
Akizungumzia juu
ya usambazaji wa Bia hii, meneja mauzo wa Dar Brew Bw. Saidi Mremi amesema; Baada
ya uzinduzi huu unaofanyika leo, Bia hii ya Chibuku Super itaanza kupatikana
kesho katika Baa zote, Super Markets, na sehemu nyinginezo zinazouza vileo.
Tunatarajia wateja na wapenzi wa bia wataifurahia bia hii mpya itakayouzwa kwa
bei ya shilingi 1,200/- tu kwa chupa yenye ujazo wa lita moja.
Na kwa wauzaji
wa jumla, tunatarajia watahamasika kuuza bia ya Chibuku Super kwani ina faida
nzuri na haina usumbufu wa kununua chupa, kwani chupa zake hazirudishwi (Take
away), alisema Mremi
Tuna imani kubwa
wapenzi wa Bia wataipokea bia hii mpya kwa Shangwe na furaha kubwa, na pia
watatumia Bia hii kuonesha kuwa wanajali Asili yao. Alimaliza Mremi.
No comments:
Post a Comment