Balozi
Gomile-Chidyaonga ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Malawi nchini
Tanzania mwaka 2011, alikuwa Naibu Balozi wa nchi hiyo Uingereza alifikwa na
mauti baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Msiba huo ni mkubwa
katika fani ya mpira wa miguu nchini kwani, Balozi Gomile-Chidyaonga ndiye
aliyefanikisha ujio wa timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) ambayo Mei 4 mwaka
huu ilicheza mechi ya kirafiki na Taifa Stars jijini Mbeya.
TFF tunatoa pole
kwa familia ya marehemu Balozi Gomile-Chidyaonga, Ubalozi wa Malawi nchini na
Chama cha Mpira wa Miguu Malawi (FAM), na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Bwana alitoa, Bwana
ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina.
No comments:
Post a Comment