Wachezaji wa kimataifa wa Tanzania wanaochezea TP
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Mbwana Samata na Thomas
Ulimwengu wanatarajiwa kuwasili Jumamosi mchana (Mei 17 mwaka huu) kujiunga na
Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya Zimbabwe (Mighty Warriors).
Washambuliaji hao watatokea moja kwa moja Sudan ambapo
kesho (Mei 16 mwaka huu) TP Mazembe itacheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika
dhidi ya timu ya huko.
Ujio wa washambuliaji hao utafanya wachezaji wote
kutoka nje walioitwa na Kocha Mart Nooij kuwa wamepatikana kwa ajili ya mechi
hiyo ya mchujo ya Kombe la Afrika ambalo fainali zake zitachezwa mwakani nchini
Morocco. Mchezaji mwingine wan je ambaye tayari ameripoti Stars ni Mwinyi
Kazimoto anayecheza nchini Qatar.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
linamshukuru Mmliki wa TP Mazembe ambaye pia ni Gavana wa Jimbo la Katanga,
Moise Katumbi kwa kuwaruhusu wachezaji hao kujiunga na Taifa Stars kwa vile
mechi dhidi ya Zimbabwe ipo nje ya kalenda ya FIFA.
Naye Kocha Nooij atakuwa na mkutano na waandishi wa
habari kesho (Mei 16 mwaka huu). Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi
kwenye kambi ya Taifa Stars iliyopo katika hoteli ya Accomondia.
Wakati huo huo, Zimbabwe inawasili usiku wa kuamkia
Jumamosi (Mei 17 mwaka huu) ikiwa na msafara wa watu 27. Timu hiyo itatua saa
7.30 usiku kwa ndege ya Ethiopian Airlines na itafikia hoteli ya Sapphire Court
iliyopo Mtaa wa Lindi, Dar es Salaam.
Zimbabwe itafanya mazoezi siku hiyo jioni kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa Jumapili saa 10
kamili jioni kwenye uwanja huo huo.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment