Kocha wa Taifa Stars, Mart
Nooij amesema wachezaji wake wako tayari kwa ajili ya mechi ya Kombe la Afrika
dhidi ya Zimbabwe (Mighty Warriors) itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo (Mei 16 mwaka huu), Nooij amesema kabla ya kuja
Tanzania alikuwa akifuatilia Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), hivyo anawafahamu
wachezaji wengi.
Amesema wachezaji wanaounda
kikosi chake ni wenye uzoefu na mechi za kimataifa, hivyo wapo tayari kwa ajili
ya mechi hiyo, kwani wamepata mechi za kirafiki na mazoezi ya kutosha kwenye
kambi iliyokuwa Tukuyu mkoani Mbeya ambapo kulikuwa na utulivu mkubwa.
Nooij amesema ujio wa
washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe
ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (RDC) kutaongeza morali ya kikosi chake.
Samata na Ulimwengu watawasili
nchini Jumamosi mchana, saa 7.30 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines
wakitokea Khartoum, Sudan ambapo leo (Mei 16 mwaka huu) wanacheza mechi ya Ligi
ya Mabingwa dhidi ya Al Hilal ya huko.
Wachezaji waliopo kambini kwa
sasa ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Said Moradi, Oscar Joshua, Kelvin
Yondani, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Himid Mao,
Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri Kiemba, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Simon
Msuva, Mrisho Ngasa, Khamis Mcha, Ramadhan Singano, John Bocco, Elias maguli na
Kelvin Friday.
Wakati huo huo, timu ya
Zimbabwe (Mighty Warriors) inawasili kesho alfajiri (Mei 17 mwaka huu) kwa
ndege ya Ethiopian Airlines ikiwa na msafara wa watu 27. Kesho saa 4 asubuhi
(Mei 17 mwaka huu) Kocha wa timu hiyo atakuwa na mkutano na waandishi wa habari
katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo
zinaanza kuuzwa kesho (Mei 17 mwaka huu) kwenye vituo vya Shule ya Sekondari
Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, OilCom Ubungo,
Uwanja wa Taifa, kituo cha mafuta Buguruni na Dar Live Mbagala. Viingilio ni
sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000 tu.
wakati huohu mmoja wa wadau wa mpira wa miguu nchini ameahidi kutoa Sh Milioni 5 kwa timu ya Taifa, Taifa Stas iwapo timu hiyo itaibuka mshindi dhidi ya timu ya Taifa ya Zimbabwe katika mchezo utaochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jumapili
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) linamshukuru mdau huyo, na linatoa mwito kwa wadau wengine
wajitokeze kutoa motisha kwa Taifa Stars.
Bonasi ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) kwa wachezaji wa Taifa Stars itatolewa kwa mujibu wa taratibu
zilizopo.
TFF YAOMBOLEZA
VIFO VYA WASHABIKI DR CONGO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi mwenzake wa
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- FECOFA, Omar Constant kutokana na vifo vya
washabiki.
Washabiki 12 walipoteza maisha
uwanjani wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya nchi hiyo kati ya TP Mazembe na AS Vita
iliyochezwa kwenye Uwanja wa Tata Raphael, jijini Kinshasa.
“Tumeguswa na msiba huo mzito,
tunatoa salamu za rambirambi kwako (Rais wa FECOFA), familia za marehemu pamoja
na wadau wote wa mpira wa miguu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo,”
imesema sehemu ya barua hiyo ya Rais Malinzi.
KOZI ZA UKOCHA
LESENI A, B KUFANYIKA JUNI
Kocha a ukocha wa mpira wa
miguu kwa ajili ya leseni A na B zinazotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) zitafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 2 mwaka
huu.
Ada kwa kozi zote ni sh. 300,000 ambapo wale
watakaofanya ya A (equivalent) itaanza Julai 21-26 mwaka huu. Washiriki wa kozi
hiyo ni wale wenye leseni B za ukocha za CAF.
Kwa wale watakaoshiriki kozi ya leseni B ambao
ni wale wenye leseni C watakuwa na vipindi viwili. Kipindi cha kwanza ni
kuanzia Juni 2-15 mwaka huu wakati cha pili kinaanza Juni 23 mwaka huu na
kumalizika Juni 28 mwaka huu.
Wakufunzi wanaotambuliwa na CAF watakaoendesha
kozi hiyo ni Sunday Kayuni na Salum Madadi kutoka Tanzania, na washiriki
watajigharamia kwa kila kitu. Baadaye CAF watatuma Mkufunzi mwingine kwa ajili
ya mitihani.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA
MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment