MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Wednesday, June 4, 2014

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA, SAADA SALUM MKUYA YA BAJETI YA WIZARA HIYO KWA MWAKA 2041/15

1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea, kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2014/15.


2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya mwaka 2014/15. Aidha, natoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuniteua kuwa Waziri wa Fedha. Ninaahidi kwamba nitatekeleza jukumu hili kwa weledi na uadilifu. Vile vile, nawapongeza Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mhe. Adam Kighoma Ali Malima (Mb) kwa kuteuliwa kuwa Naibu Mawaziri wa Wizara ya Fedha. Kadhalika, namshukuru pia aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Janeth Zebedayo Mbene (Mb) kwa utendaji kazi wake mahiri na tunamuombea Mwenyezi Mungu ampe nguvu na afya njema katika kazi zake mpya Wizara ya Viwanda na Biashara. Nichukue pia fursa hii kumpongeza Bw.

2

Rished M. Bade kwa kuteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.

3. Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe mwenyewe, Naibu Spika pamoja na Wenyeviti wa Bunge kwa kuongoza vyema majadiliano ya Bunge la Bajeti.

4. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie nafasi hii kuishukuru kwa namna ya pekee Kamati ya Kudumu ya Uchumi, Viwanda na Biashara chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mbunge wa Kisesa) na Makamu wake Mhe. Dunstan Luka Kitandula (Mbunge wa Mkinga) kwa maoni, ushauri na mapendekezo waliyoyatoa kwa Wizara wakati wa kuchambua mapendekezo ya Bajeti ya Wizara ya Fedha. Aidha, nachukua nafasi hii kumshukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti Mhe. Andrew John Chenge (Mbunge wa Bariadi Magharibi) pamoja na Kamati nzima kwa ushauri wao. Katika uandaaji wa hotuba hii, Wizara imezingatia ushauri na mapendekezo ya Kamati hizo pamoja na ushauri na maoni ya hoja mbalimbali zilizotolewa wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara kwa mwaka 2013/14.

5. Mheshimiwa Spika, kama unavyofahamu, Wizara ilipata pigo kwa kuondokewa na kiongozi wetu mkuu Marehemu Dkt. William Augustao Mgimwa. Tunawashukuru Viongozi wa Serikali, Waheshimiwa Wabunge, Washirika wa Maendeleo, Taasisi mbalimbali pamoja na wananchi kwa ushirikiano waliotupa kipindi chote cha msiba. Tumeendelea kuenzi misingi imara aliyotujengea marehemu katika kutekeleza majukumu ya Wizara. Aidha, tunapenda kutoa pole kwa ndugu na

3

jamaa kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Chalinze Marehemu Saidi Ramadhani Bwanamdogo. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.

6. Mheshimiwa Spika, napenda kuwapongeza, Mhe. Yusuf Salim Hussein Mbunge wa Chambani, Mhe. Godfrey William Mgimwa (Mbunge wa Kalenga) na Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mbunge wa Chalinze) kwa kuchaguliwa kwao.

7. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Mhe. Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mpanda Mashariki kwa hotuba yake nzuri ambayo imetoa mwelekeo wa shughuli za Serikali kwa mwaka 2014/15.

8. Mheshimiwa Spika, katika hotuba yangu nitaanza kuelezea mapitio ya utekelezaji wa mipango ya Wizara katika mwaka 2013/14. Nitaelezea pia mikakati mbalimbali ambayo Wizara imeweka kwa mwaka 2014/15 ili kuendelea kuboresha utekelezaji wa majukumu yake ya msingi yakiwemo: usimamizi wa Bajeti ya Serikali; ukusanyaji mapato ya Serikali; usimamizi wa misaada na mikopo; ulipaji wa Deni la Taifa; usimamizi wa matumizi ya fedha za umma; usimamizi na udhibiti wa ununuzi wa umma; usimamizi wa utekelezaji wa MKUKUTA; na usimamizi wa mashirika na taasisi za umma.

4

9. Mheshimiwa Spika, mwisho nitawasilisha bajeti ya mwaka 2014/15 kwa mafungu saba ya wizara ya fedha ambayo ni fungu 7, 10, 13, 21, 22, 23 na fungu 50 pamoja na fungu 45 la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA 2013/14 NA MALENGO YA MWAKA 2014/15

10. Mheshimiwa Spika, uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa Mpango na Bajeti ya Wizara umezingatia malengo ya Mpango Mkakati wa Wizara wa mwaka 2012/13 - 2016/17 ambao utaiwezesha Wizara kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025; Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano 2011/12 - 2015/16; Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA II); Malengo ya Maendeleo ya Milenia 2015; Mkakati wa Pamoja wa Misaada Tanzania (MPAMITA) pamoja na Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma – PFMRP. Aidha, Mpango na Bajeti ulizingatia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2010 pamoja na Mfumo wa Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa (Big Results Now – BRN).

11. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara ilipanga kutekeleza yafuatayo: kuongeza mapato ya ndani kufikia uwiano wa Pato la Taifa wa asilimia 20.9 kwa mwaka 2013/14 ikilinganishwa na asilimia 17.7 kwa mwaka 2012/13; kukamilisha Ripoti za Utafiti wa Mfumo Bora wa Kodi wa Serikali ya Jamhuri ya

5

Muungano wa Tanzania; kuandaa na kusimamia utekelezaji wa bajeti ya Serikali; kusimamia utekelezaji wa MKUKUTA-II; kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa watekelezaji wa miradi hiyo; kukamilisha Sera ya Mali ya Umma; kufanya tathmini ya usimamizi na utekelezaji wa malipo ya mishahara ya watumishi wa umma; kusimamia utekelezaji wa mipango kazi ya ukaguzi na uzingatiwaji wa miongozo ya ukaguzi katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, na Mamlaka ya Serikali za Mitaa; kuratibu na kusimamia upatikanaji wa misaada na mikopo nafuu kutoka Nchi Wahisani, Mashirika na Asasi za Fedha za Kimataifa; kuidhinisha miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP); na kukamilisha Sera ya Taifa ya Ununuzi wa Umma.

12. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, Wizara pia ilipanga kukamilisha miradi ya MCA-T na kukabidhi miradi iliyokamilika kwa taasisi husika; kusimamia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya nne (PFMRP IV); kufanya uhakiki wa Wastaafu waliopo katika Daftari la Pensheni la Hazina; kuunganisha Hazina Ndogo na Sekretarieti za Mikoa 24 katika mfumo wa malipo kwa njia ya elektroniki kupitia Benki Kuu ya Tanzania (Tanzania Inter- Bank Settlement System - TISS); kuimarisha utendaji kazi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina; na kuandaa na kuhuisha kanuni na miongozo ya utekelezaji wa Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi.

6

Mfumo wa Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa

13. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, kupitia Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa, Wizara ya Fedha katika maabara ya utafutaji wa rasilimali fedha iliwekewa malengo yafuatayo: kuongeza mapato mapya ya kodi ya shilingi trilioni 1.16; kuongeza mapato mapya yasiyo ya kodi ya shilingi bilioni 96.7; kudhibiti matumizi; na kutafuta fedha za utekelezaji wa miradi ya Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa katika sekta zinazotekeleza miradi hiyo.

14. Mheshimiwa Spika, hadi mwezi Aprili 2014, ukusanyaji wa mapato kutoka vyanzo vilivyoibuliwa chini ya BRN umefikia shilingi bilioni 338 sawa na asilimia 29.14 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.16. Matokeo yasiyoridhisha yalisababishwa na baadhi ya mapendekezo ya BRN kutokutekelezwa katika mwaka 2013/14. Mapendekezo hayo ni kubadilisha mfumo wa ushuru wa bidhaa zisizo za petroli kutoka specific kwenda advalorem (makisio shilingi bilioni 386) na kuanzisha kodi ya zuio ya asilimia tano kwenye bidhaa zinazotoka nje ya nchi (makisio shilingi bilioni 225.6). Kwa vile ukusanyaji wa mapato ndio msingi wa kufanikiwa kwa BRN, Serikali inachambua vyanzo mbadala vya kufidia mapato haya ili kuhakikisha lengo kuu la kuongeza mapato kwa shilingi trilioni 3.48 linafikiwa ifikapo mwaka 2015/16.

7

Mwenendo wa Uchumi

15. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara kupitia Benki Kuu iliendelea na jukumu la kuandaa, kusimamia na kutathmini utekelezaji wa sera ya fedha inayolenga kuwa na kiwango kidogo cha mfumuko wa bei kwa ajili ya kuhakikisha gharama za maisha haziongezeki. Kutokana na juhudi hizi, mfumuko wa bei umeshuka kutoka wastani wa asilimia 16 mwaka 2012 hadi kufikia wastani wa asilimia 7.9 mwaka 2013. Katika kipindi hiki uchumi umeendelea kuimarika huku ukuaji halisi wa Pato la Taifa ukiongezeka kwa asilimia 7.0 katika kipindi cha mwaka 2013 ikilinganishwa na asilimia 6.9 katika mwaka 2012. Shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kiasi kikubwa ni pamoja na mawasiliano asilimia 22.8, huduma za kifedha asilimia 12.2, ujenzi asilimia 8.6, na uuzaji bidhaa wa jumla na rejareja asilimia 8.3. Katika mwaka 2014/15, Wizara kupitia Benki Kuu itaendelea kushirikiana na wadau wote katika kuhakikisha kwamba lengo la msingi la utulivu wa bei na ukuaji wa uchumi linadumishwa.

Uandaaji na Usimamizi wa Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali

16. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara imeratibu uandaaji wa Mwongozo wa Mpango na Bajeti kwa kipindi cha 2014/15 – 2016/17 kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na kusambaza kwa wadau mwezi Desemba kama

8

ilivyopangwa. Aidha, Wizara imeandaa na kuchapisha vitabu vya bajeti ya Serikali vya mwaka 2014/15 (Volume I, II, III na IV) kama vilivyowasilishwa Bungeni kwa ajili ya mjadala wa Bunge la Bajeti la mwaka 2014/15 unaoendelea; kitabu cha tafsiri rahisi ya bajeti ya Serikali (Citizen’s Budget) kwa mwaka 2013/14; na Kitabu cha Budget Background and Medium Term Framework – 2013/14 – 2015/16.

17. Mheshimiwa Spika, Serikali inakusudia kuanza kutumia mfumo wa Programu katika uandaaji, uidhinishaji na utekelezaji wa Bajeti. Mfumo huu utasaidia Serikali kugawa rasilimali kwa kuzingatia matokeo na kuweka viashiria vya kufikia malengo. Katika hatua za awali za maandalizi ya utekelezaji wa mfumo huu katika mwaka 2013/14, Wizara ilitenga fedha kwa ajili ya mafunzo kwa wataalam wa Wizara nane za mfano. Maandalizi haya ya kimkakati na kimfumo yataendelea katika mwaka 2014/15. Wizara zilizotengwa kwa majaribio na ambazo tayari zimefanyiwa mafunzo ni Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Wizara ya Fedha. Wizara hizi kwa sasa zinaendelea na zoezi la kuandaa programu na viashiria vya kupima utekelezaji kabla ya mfumo kuanza kutumika.

18. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu kikao kazi cha wataalamu wa wizara, mikoa na halmashauri kuhusu mfumo wa ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Bajeti. Katika kipindi hicho,

9

Wizara pia ilifanya kikao kazi kilichohusisha washiriki kutoka wizara, idara za Serikali zinazojitegemea, mikoa na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa lengo la kutathmini uandaaji na uwasilishwaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/13 na kufanya mkutano wa mwaka wa wadau ambao ulijumuisha Washirika wa Maendeleo kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa Bajeti ya Serikali.

19. Mheshimiwa Spika, katika kusimamia na kudhibiti utekelezaji wa bajeti ya Serikali ikiwemo kufuatilia matumizi ya fedha za umma, Wizara ilifanya ufuatiliaji na ukaguzi wa matumizi ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya maendeleo kwa miradi ya ASDP na DASIP ikihusisha wizara nne, mikoa sita na halmashauri 33. Aidha, ufuatiliaji na ukaguzi ulifanyika kwa mapato na matumizi ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) na kwa fedha zilizotolewa kuhudumia vituo 16 vya Makazi ya Wazee katika mikoa 14 nchini.

20. Mheshimiwa Spika, katika ukaguzi huo, Wizara ilibaini kuwapo kwa upungufu na changamoto katika maeneo haya ikiwa ni pamoja na: fedha kutowafikia walengwa kwa wakati kama ilivyopangwa; udhaifu kwenye udhibiti wa ndani wa matumizi na hivyo kusababisha kuwapo kwa huduma duni; na miradi kutokamilika kwa wakati na kuwepo kwa bakaa ya fedha za maendeleo. Aidha, zimekuwepo changamoto za kubadilika mara kwa mara bei ya kununulia nafaka na gharama za usafirishaji, hivyo kuathiri malengo yaliyopangwa ikiwemo kusababisha madeni. Wizara imewasiliana na wahusika na kutoa nyaraka za maelekezo ya kuhakikisha kwamba udhibiti wa ndani

10

wa matumizi unaimarishwa katika ngazi zote za usimamizi na inapobidi hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.

21. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara inatarajia kutekeleza yafuatayo: kupitia mfumo wa uwasilishaji wa bajeti za wizara, idara za Serikali, mikoa na halmashauri na kuhakikisha kuwa sera na mipango ya kitaifa na ile ya kisekta vyote vimezingatiwa ipasavyo katika Bajeti ya Serikali na kutengewa fedha; kufanya tathmini ya utekelezaji wa Bajeti ya Serikali, kuendelea kuboresha mfumo wa mpangilio wa Bajeti ya Serikali kwa kuzingatia programu mbalimbali; kuimarisha mifumo ya kompyuta ya uandaaji bajeti ili kukidhi mahitaji ya taarifa mbalimbali zinazohitajika; kuendelea kujenga uwezo wa wizara, idara za Serikali, mikoa na halmashauri katika uandaaji wa Bajeti ya Muda wa Kati, usimamiaji wake na utoaji taarifa za utekelezaji ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji na tathmini kwa wakati; kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ili kuhakikisha uwazi na uwajibikaji unazingatiwa; na kufuatilia matumizi ya fedha za umma zikiwemo fedha za mishahara, matumizi mengineyo na fedha za miradi.

Usimamizi wa Misaada na Mikopo

22. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara ilifanikisha kusainiwa kwa mikataba 18 kwa ajili ya misaada na mikopo nafuu yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 958.027 kutoka kwa Washirika wa Maendeleo. Aidha, Wizara imeendelea kuratibu ukamilishaji wa Mwongozo mpya wa Ushirikiano wa

11

Maendeleo - Development Cooperation Framework ambao utachukua nafasi ya Mkakati wa Pamoja wa Misaada Tanzania (MPAMITA). Mwongozo huu una lengo la kusimamia ushirikiano wa maendeleo baina ya Serikali na Wadau wa Maendeleo na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana wakati wa utekelezaji wa MPAMITA. Lengo la ujumla ni kupatikana ufanisi katika misaada kutoka kwa Washirika wa maendeleo na kubainisha wajibu wa kila mdau wa maendeleo wakiwemo raia, wabunge, asasi zisizo za kiserikali na sekta ya habari.

23. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara imepanga kufanya yafuatayo: kuzindua Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo na kuandaa mpango kazi wake pamoja na kuhamasisha matumizi yake kwa Washirika wa Maendeleo, Wizara, Idara Zinazojitegemea, Serikali za Mitaa, Taasisi Binafsi na Waheshimiwa Wabunge; kutathmini utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali inayotekelezwa kwa fedha toka Washirika wa Maendeleo kwa nia ya kuhakikisha kwamba thamani ya fedha inapatikana katika miradi hiyo; kushiriki kwenye majadiliano na Jumuiya za kikanda na kimataifa; na kuendelea kutafuta fedha za misaada na mikopo nafuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na Misaada ya Kiufundi kutoka kwa Mashirika ya Kimataifa na nchi wahisani.

12

Ulipaji wa Deni la Taifa

24. Mheshimiwa Spika, Deni la Taifa limeendelea kusimamiwa na Sheria ya Madeni ya mwaka 1974 na marekebisho yake ya mwaka 2004. Wizara imeendelea kutoa kipaumbele katika ulipaji wa madeni kwa wakati ili kuepuka malimbikizo ya riba. Katika kipindi cha Julai, 2013 hadi Aprili, 2014 malipo ya deni la ndani yalifikia shilingi bilioni 1,694.53 ambapo kati ya malipo hayo riba ni shilingi bilioni 581.20 na Mtaji (principal rollover) ni shilingi bilioni 1,113.33. Aidha, deni la nje limelipwa kwa kiasi cha shilingi bilioni 340.22, kati ya kiasi hicho malipo ya riba ni shilingi bilioni 201.52 na deni halisi - principal ni shilingi bilioni 138.70.

25. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara itaendelea kulipa madeni ya ndani na nje kwa wakati ikiwa ni pamoja na kulipa kwa wakati madeni mbalimbali ambayo serikali imeingia mikataba (Contractual Liabilities) na madai ya dharura (Contingent Liabilities) pindi yanapotokea.

Usimamizi wa Matumizi ya Fedha za Umma

26. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kujenga uwezo wa usimamizi wa matumizi ya fedha za umma kwa kudhamini mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi 313 wa kada ya uhasibu, ugavi na kompyuta kutoka kwenye wizara, idara za serikali, sekretariati za mikoa, manispaa, halmashauri za miji na wilaya waliopo vyuoni na watumishi 218 walipewa mafunzo ya muda mfupi kwa lengo la kuongeza ufanisi katika usimamizi wa matumizi ya fedha za umma. Aidha,

13

Wizara imeendelea kusambaza Mfumo wa Malipo wa Kielektroniki -TISS mikoani ambapo hadi sasa jumla ya mikoa 20 imeunganishwa katika mtandao huo. Mikoa iliyounganishwa kwenye mtandao huo ni Iringa, Morogoro, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa, Ruvuma, Lindi, Simiyu, Mwanza, Kagera, Geita, Mara, Mtwara, Kigoma, Shinyanga, Njombe, Dar es Salaam na Katavi. Vile vile, mikoa mipya ya Geita, Simiyu, Katavi na Njombe imeunganishwa kwenye mtandao wa malipo wa Serikali (Intergrated Financial Management System).

27. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na mpango wa kutekeleza mfumo wa uandaaji wa taarifa za hesabu kwa kuzingatia Viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Taarifa za Hesabu katika Sekta ya Umma -IPSAS Accrual Basis ambapo hesabu za majumuisho za mwaka 2012/13 zimeandaliwa kwa kutumia mfumo huo kwa mara ya kwanza na kuwasilishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa wakati.

28. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, pamoja na mambo mengine, Wizara itaendelea kuboresha usimamizi wa fedha za umma kwa kufanya yafuatayo: kuendelea kutoa udhamini wa masomo ya muda mrefu na mfupi kwa wahasibu, wakaguzi, maafisa ugavi na wataalamu wa kompyuta kutoka Serikali Kuu na serikali za mitaa; kuweka mitambo katika hazina ndogo zote ili kuwezesha sekretariati za mikoa na hazina ndogo kufanya malipo kwa kutumia mifumo ya malipo ya kielektroniki -TISS/EFT;

14

kuendelea kutoa mafunzo ya TISS/EFT kwa wahasibu na watumishi wa kada zingine ili kuimarisha mfumo wa malipo; na kuanza ujenzi wa jengo la ofisi ya Hazina Ndogo Arusha.

29. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15 ili kuinua kiwango cha fani ya uhasibu sambamba na kuimarisha usimamizi wa fedha za umma Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano wa Wahasibu Wakuu wa Serikali wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika – ESAAG.

Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma – Public Finance Management Reform Programme (PFMRP)

30. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma imekamilisha utafiti wa mfumo wa kupeleka fedha kwenye Serikali za Mitaa, mpango wa utekelezaji wa utafiti huo umeandaliwa na utekelezaji wake utaanza mwaka wa fedha 2014/15. Aidha, utafiti juu ya mifumo ya fedha inayotumiwa na Serikali kwa lengo la kuiunganisha mifumo hiyo ili kuboresha usimamizi wake umekamilika. Vile vile, Wahasibu 522 kutoka Wizara mbalimbali, hazina ndogo na sekretarieti za mikoa walipata mafunzo juu ya Viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Taarifa za Hesabu katika Sekta ya Umma na watumishi wengine 34 ambao wanasimamia programu hii kutoka katika wizara na taasisi walipata mafunzo ya kusimamia Mabadiliko na Kuandaa

15

Mipango Mkakati -Change Management and Strategic Planning. Mafunzo haya yalilenga kuwajengea uwezo wa kuandaa mipango na bajeti inayolenga katika kutekeleza maboresho ya usimamizi wa fedha za umma.

31. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara itaendelea kuboresha usimamizi wa fedha za umma kwa kuendelea na utekelezaji wa Awamu ya Nne ya Programu ya PFMRP kwa kufanya yafuatayo: kupitia na kuboresha mifumo ya kifedha na kuangalia njia bora ya kuiunganisha baada ya utafiti kukamilika; na kuwajengea uwezo wakaguzi wa ndani katika wizara, idara, wakala za Serikali na halmashauri za Serikali za Mitaa juu ya ukaguzi wa mifumo ya fedha, usimamizi na ukaguzi wa vihatarishi, ukaguzi wa bajeti na mishahara, na ukaguzi wa miradi.

Sera ya Ununuzi wa Umma

32. Mheshimiwa Spika, katika kusimamia Sekta ya Ununuzi wa Umma nchini, Wizara imeendelea kutekeleza yafuatayo: kuandaa Sera ya Taifa ya Ununuzi wa Umma; kuandaa mapendekezo ya muundo wa Vitengo vya Usimamizi wa Ununuzi na Ugavi Serikalini; na kufanya tathmini ya mahitaji ya mafunzo kwa maafisa ununuzi na ugavi walioko katika Mamlaka za Serikali za Mitaa; na kuendelea kuhuisha taarifa za maafisa ununuzi na ugavi Serikalini, ambapo taarifa za maafisa 332 katika mikoa ya Shinyanga, Kagera, Mwanza na Mara zimehakikiwa na kuingizwa katika daftari la maafisa ununuzi na ugavi.

16

33. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara imepanga kufanya yafuatayo: kuandaa Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Ununuzi wa Umma na kusimamia utekelezaji wa Sera hiyo; kuhuisha muundo wa vitengo vya usimamizi wa ununuzi na ugavi serikalini; kuipitia Sheria ya Ununuzi wa Umma Na.7 ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013; kukamilisha tathmini ya mahitaji ya mafunzo kwa maafisa ununuzi na ugavi Serikalini; na kufanya tathmini juu ya ufanisi wa ununuzi wa umma nchini.

Udhibiti wa Ununuzi wa Umma

34. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma imetoa mafunzo kuhusu sheria, kanuni na taratibu za ununuzi kwa taasisi za umma 32 ambapo watumishi 747 walihudhuria mafunzo hayo. Aidha, Mamlaka ilitoa mafunzo kuhusu mfumo wa upokeaji na usimamizi wa taarifa za ununuzi nchini katika vituo vinne vya Morogoro, Arusha, Mwanza na Mbeya ambapo jumla ya washiriki 330 kutoka taasisi 191 walishiriki. Vile vile, Mamlaka imeendelea kusimamia mfumo wa upokeaji na usimamizi wa taarifa za ununuzi nchini ambapo katika kipindi hicho, taasisi 191 ziliunganishwa na kupatiwa mafunzo ya kutumia mfumo huo na hivyo kufanya jumla ya taasisi zilizounganishwa na kupatiwa mafunzo kufikia 364, sawa na asilimia 80 ya taasisi zote.

17

35. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma imefanya ukaguzi kuhusu utoaji wa zabuni na utekelezaji wa mikataba itokanayo na ununuzi wa umma katika Taasisi 120 zikiwemo wizara na idara zinazojitegemea 32, mashirika ya umma 46 na serikali za mitaa 42. Ukaguzi huu uilihusisha mikataba 5,867 yenye thamani ya shilingi bilioni 1,985.427 ikiwemo miradi 207 ya ujenzi yenye thamani ya shilingi bilioni 777.2. Ripoti ya ukaguzi inaonesha wastani wa uzingatiwaji wa sheria ya ununuzi ulikuwa ni asilimia 64 ambayo ni chini ya lengo la asilimia 80. Maeneo yaliyobainika kuwa na udhaifu mkubwa ni katika usimamizi wa mikataba na utunzaji wa nyaraka za ununuzi.

36. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara imepanga kutekeleza yafuatayo: kuandaa mpango kazi wa usimamizi wa utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2011; kuelimisha wadau mbalimbali kuhusu Sheria mpya na kanuni zake; kuendelea na maandalizi ya kuanzisha mfumo wa ununuzi kwa njia ya kielektronic (e-procurement system); kufungua ofisi za kanda Dodoma, Mbeya na Mwanza; kushirikiana na TAMISEMI ili kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye vitengo vya ununuzi vya halmashauri mbalimbali; kufanya kazi na Asasi za Kiraia na Wanahabari ili kuongeza uelewa wa masuala ya Ununuzi wa Umma kwa wananchi; na kuendelea kusimamia ununuzi katika sekta ya Umma.

18

Huduma ya Ununuzi Serikalini

37. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini imetekeleza yafuatayo: kuongeza vifaa vya huduma mtambuka kutoka 86 vilivyokuwepo hadi 181; kuendelea na ujenzi wa Ofisi na ghala katika mkoa wa Manyara; kuendelea na ujenzi wa kituo cha mafuta mkoa wa Dodoma; na kununua magari mawili makubwa yenye uwezo wa kubeba lita 45,000 za mafuta kila moja kwa ajili ya kusafirisha mafuta toka kwa wazabuni kwenda mikoani. Aidha, Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini, imeanza kufunga Mfumo wa Udhibiti na Usimamizi wa Mafuta ya Magari ambao utaanza kwa majaribio Agosti, 2014 katika mkoa wa Dar es Salaam ili kudhibiti matumizi ya mafuta katika magari ya Serikali.

38. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini imepanga kutekeleza yafuatayo: kukamilisha kazi ya kufunga Mfumo wa Udhibiti na Usimamizi wa Mafuta ya Magari katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma, Iringa na Mbeya; kuanza kazi za Ujenzi wa Ofisi katika mikoa ya Njombe na Mara; kukamilisha ujenzi wa visima vya mafuta katika mikoa ya Geita, Katavi na Wilaya ya Ileje; na kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta kufikia wastani wa lita 50,000 katika vituo vya mikoa ya Arusha, Mwanza, Kigoma, Mtwara, Lindi, Tabora, Pwani, Tanga na Ruvuma. Aidha, Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini itahuisha muundo wake ili kuweza kutoa huduma ngazi ya wilaya na

19

kuanza kutekeleza utaratibu wa ununuzi wa magari kwa pamoja.

Rufaa za Zabuni za Umma

39. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma imepokea jumla ya mashauri 35, kati ya hayo mashauri matatu yaliondolewa na walalamikaji kabla ya kusikilizwa; mashauri 17 walalamikaji walishinda; mashauri 11 walalamikaji walishindwa; mashauri mawili yalifutwa kufuatana na sheria; shauri moja halikutolewa uamuzi kutokana na ukomo wa muda wa kulisikiliza; na shauri moja lipo kwenye hatua ya kusikilizwa. Aidha, katika mwaka 2014/15, Mamlaka itaendelea kusikiliza na kutolea maamuzi malalamiko na rufaa katika Ununuzi wa Umma na kuelimisha umma na wadau juu ya kuwasilisha pingamizi za zabuni kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2011.

Usimamizi wa Mali ya Serikali

40. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara iliendelea kuandaa Sera ya Mali ya Umma. Lengo la sera hii ni kusimamia na kutoa miongozo ya udhibiti wa mali ya umma. Aidha, Wizara ilifanya uthamini wa mali ya Serikali katika mikoa mitano na wizara mbili, hivyo kufanya wizara, idara zinazojitegemea na wakala wa Serikali zilizofanyiwa uthamini kufikia 42. Katika kipindi hicho, usimikaji wa mfumo wa uhakiki wa mali ya umma ulikamilika. Vile vile, Wizara iliendelea na zoezi la kuondosha mali

20

chakavu katika wizara na idara za Serikali ambapo jumla ya shilingi bilioni 1.58 zilikusanywa kutokana na mauzo ya vifaa hivyo na shilingi milioni 12.83 kutokana na utoaji wa leseni za udalali.

41. Mheshimiwa Spika, Wizara ilifanya uhakiki wa mali ya Serikali katika wizara, idara zinazojitegemea na wakala za Serikali kwa lengo la kudhibiti matumizi ya mali katika taasisi hizo. Aidha, Wizara imefanya uhakiki maalum katika Bohari Kuu ya Madawa ambapo ushauri ulitolewa wa namna ya kupunguza hasara inayotokana na madawa, vifaa tiba na vitendanishi kuisha muda wake wa matumizi kabla ya kutumika.

42. Mheshimiwa Spika, katika mwaka, 2014/15, Wizara imepanga kukamilisha Sera ya Mali ya Umma na kuisambaza kwa wadau kwa ajili ya kupata maoni kabla ya kuanza utekelezaji wake. Aidha, Wizara imepanga kufanya uthamini wa mali katika mikoa saba na taarifa zake kuingizwa kwenye Daftari la Mali ya Serikali. Vile vile, Wizara itaendelea kuondosha mali chakavu, mali zilizokwisha muda wake na vifaa sinzia kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Fedha za Umma; kushughulikia taarifa za ajali na potevu za mali ya Serikali; na kuendelea kuchambua, kufanya majadiliano na wadai na kulipa madai ya fidia na kifuta machozi yanayotokana na amri ya Mahakama. Kadhalika, Wizara itaendelea na uhakiki wa mali katika wizara, idara zinazojitegememea na wakala za Serikali.

Mpango wa Millenium Challenge Account – Tanzania (MCA-T)

21

43. Mheshimiwa Spika, Programu ya Millenium Challenge Account Tanzania iliendelea na ukamilishaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji, nishati ya umeme na maji. Miradi yote ya barabara imekamilika isipokuwa sehemu ya Laela- Sumbawanga katika barabara ya Tunduma- Sumbwanga ambayo inatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka 2014. Miradi ya umeme na maji imekamilika na ipo katika kipindi cha uangalizi. Aidha, kutokana na utekelezaji wa kuridhisha, Tanzania imekidhi vigezo na hivyo itanufaika na awamu ya pili ya msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC). Katika awamu ya pili, miradi itakayofadhiliwa ni ya umeme na barabara za vijijini Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Ukaguzi wa Ndani

44. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara imetekeleza yafuatayo: kutoa Mwongozo wa Kamati za Ukaguzi katika Sekta ya Umma kwa lengo la kuhakikisha utendaji wenye tija kwa Kamati zote za Ukaguzi; kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa ndani 458, wajumbe wa Kamati za Ukaguzi na wadau wa ukaguzi wa ndani wapatao 567; kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo 11; ukaguzi wa orodha ya malipo ya mishahara; na kuhakiki madai mbalimbali yaliyowasilishwa wizarani kabla ya kulipwa.

22

45. Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza juhudi za Serikali za kudhibiti ubora wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, Wizara imenunua vifaa vya kuhakiki ubora wa miundombinu. Vifaa hivyo vitatumika katika ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Halmashauri za Serikali za Mitaa katika kuhakikisha kuwa miradi na miundombinu inayotekelezwa inakuwa na ubora unaokidhi viwango na hatimaye kupata thamani ya fedha. Hatua hii itaenda sambamba na kuwajengea uwezo wakaguzi wa ndani Serikalini katika kufanya ukaguzi wa kiufundi kwa miradi inayotekelezwa katika taasisi zao.

46. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara itaendelea kusimamia kada ya ukaguzi wa ndani na kamati za ukaguzi; kufanya ukaguzi wa Mfumo wa ulipaji Mishahara Serikalini; kuhakiki madai mbalimbali ya Serikali kabla ya kuyalipa; na kufuatilia utekelezaji wa miongozo mbalimbali iliyotolewa. Aidha, Wizara inatarajia kutoa miongozo ifuatayo: Mwongozo wa Usimamizi wa Viashiria Vya Udanganyifu; Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani; Mwongozo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Usimamizi wa Vihatarishi; Mwongozo wa Ukaguzi wa Ununuzi; na Mwongozo wa Ukaguzi wa Mikataba. Vile vile, wizara kwa kushirikiana na Taasisi za Serikali itaendelea kuimarisha ofisi za Mkaguzi Mkuu wa ndani kwa lengo la kusimamia matumizi ya fedha.

Ukaguzi wa Hesabu za Serikali

23

47. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imetekeleza kazi zake kwa mujibu wa sheria. Ofisi imeendelea kuwa mshirika katika Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa katika kukagua taasisi za Umoja wa Mataifa. Aidha, Ofisi imeendesha mafunzo kwa Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali na Kamati ya Bajeti kwa lengo la kuzijengea uwezo wa kuimarisha uwajibikaji na utawala bora. Vile vile, ukaguzi wa mapato na matumizi ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu unaendelea.

48. Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuondoa wakaguzi katika majengo ya wakaguliwa, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imekodi majengo ya ofisi katika mikoa ya Mwanza, Tabora, Tanga, Iringa, Kagera na Geita. Aidha, ujenzi wa ofisi katika mkoa wa Dodoma unaendelea ukiwa katika hatua za mwisho. Vile vile, Ofisi imeendelea na uunganishaji wa ofisi zake zilizoko mikoani na makao makuu kwa njia ya mtandao mpana. Kwa mwaka huu ofisi 4 zimeunganishwa na hivyo kufanya ofisi zilizounganishwa kufikia 14.

49. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/15, Ofisi inatarajia kufanya yafuatayo: kukagua mafungu yote 49 ya Wizara na Idara za serikali, hesabu za Mikoa yote 25 ya Tanzania Bara, Hesabu za Halmashauri zote 161 za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji, Mashirika ya Umma 177, Balozi zote 32 zilizoko nje ya nchi na Wakala 33 za Serikali pamoja na kufanya ukaguzi wa thamani ya fedha katika maeneo sita; kuendelea na ukaguzi wa mapato na matumizi ya vyama vyote vya siasa; kuanza ukaguzi katika sekta ya gesi na mafuta pamoja na

24

ukaguzi wa miradi mikubwa inayoendeshwa kwa ubia wa sekta ya Umma na Sekta binafsi; kuendelea kushiriki kikamilifu katika jukumu la kukagua taasisi za Umoja wa Mataifa sanjari na wanachama wengine wanaounda Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa.

50. Mheshimiwa Spika, mambo mengine yatakayotekelezwa katika mwaka 2014/15, ni pamoja na: kuendelea na zoezi la kuwaondoa wakaguzi katika maeneo ya wakaguliwa katika wizara zote na katika mikoa 6 iliyobaki; kuendelea kuzijengea uwezo kwa njia ya mafunzo Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali na Kamati ya Bajeti katika maeneo ya kuelewa kwa undani taarifa za ukaguzi wa hesabu zinazoandaliwa na wakaguliwa; kukamilisha ujenzi wa ofisi katika mkoa wa Rukwa pamoja na kuanza ujenzi wa ofisi katika mikoa ya Mara na Iringa; na kutoa mafunzo kwa watumishi ili kuimarisha uwezo wao katika kutumia mfumo wa TeamMate ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika ukaguzi wa kisasa.

Uratibu wa Utekelezaji wa MKUKUTA

51. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu utekelezaji wa MKUKUTA II kwa kufanya ufuatiliaji, tafiti, na tathmini na kuandaa taarifa ya utekelezaji na hali ya Umaskini nchini ili kuwezesha maamuzi ya kisera, kibajeti na kiutekelezaji. Kazi ya uandaaji wa Taarifa ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA II imekamilika na kuwekwa katika tovuti ya Wizara. Aidha, Wizara inaendelea kukamilisha Taarifa ya

25

Maendeleo ya Malengo ya Milenia. Taarifa ya awali inaonesha kuwa umaskini wa mahitaji ya msingi kwa Tanzania Bara ni asilimia 28.2 ambapo kwa Dar es Salaam ni asilimia 4.2, maeneo mengine ya mjini ni asilimia 21.7 na maeneo ya vijijini ni asilimia 33.3. Umaskini wa chakula ni asilimia 9.7 ambapo kwa Dar es Salaam ni asilimia 1.0, maeneo mengine ya mjini ni asilimia 8.7 na maeneo ya vijijini ni asilimia 11.3.

52. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara imepanga kutekeleza yafuatayo: kukusanya na kuchambua taarifa mbalimbali kutoka katika Wizara, Idara na Wakala za Serikali ili kuandaa Taarifa ya mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA II; kuandaa taarifa ya mwisho ya kutathimini utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia; kufanya mapitio ya MKUKUTA II; kukamilisha Mpango wa Utekelezaji wa Kinga ya Jamii pamoja na kuainisha viashiria vya upimaji juhudi za kinga ya jamii; na kuratibu mkutano wa kitaifa wa kujadili sera za kupambana na Umaskini nchini. Pia Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaandaa mapendekezo ya hatua zitakazofuata baada MKUKUTA II kufikia kikomo mwezi Juni, 2015.

53. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mradi wa SELF II imeendelea kutoa mikopo kwa wajasiriamali ambapo hadi kufikia Aprili 2014, mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 8.6 ilikopeshwa kwa wajasiriamali 4,943 kupitia Asasi ndogo 103. Kati ya waliokopeshwa, wanawake ni 2,040 sawa na asilimia 41 na wanaume ni 2,903 sawa na asilimia 59. Kwa wastani, urejeshwaji wa Mikopo ya Mradi wa SELF umeendelea kuwa wa ufanisi

26

mzuri katika kiwango cha asilimia 90 hivyo kuwezesha fedha za mkopo kuzunguka na kuwafikia wananchi wengi zaidi.

54. Mheshimiwa Spika, SELF II imetoa mafunzo kwa watendaji 280 wa Asasi 115 zinazokopesha wajasiriamali wadogo. Aidha, mafunzo yametolewa kwa wajasiriamali wadogo 1,670 katika taaluma ya uendeshaji miradi ya biashara. Vile vile, Maofisa Ushirika 81 kutoka mikoa ya kanda za Kaskazini na Ziwa walipatiwa mafunzo ya utoaji mikopo. Kadhalika, Mradi umeendelea kuelimisha umma kupitia vituo vya televisheni vya TBC, ZBC na redio za jamii. Katika mwaka 2014/15, Mradi wa SELF utaendelea na majukumu yake ya kutoa huduma za mikopo kwa wajasiriamali wadogo na kuimarisha huduma za kifedha kwa njia ya kujenga uwezo wa Asasi zinazokopesha wajasiriamali wadogo.

Sheria na Miswada ya Fedha

55. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilifanya marekebisho ya Sheria mbalimbali za Fedha kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2013 -The Finance Act, 2013. Lengo la marekebisho hayo ni kuweka usimamizi mzuri wa kodi na fedha za umma. Aidha, Sheria mbalimbali zilizopitishwa na Bunge ni pamoja na Sheria ya Mfuko wa Akiba wa GEPF wa Mafao ya Wastaafu ya mwaka 2013 -The GEPF Retirement Benefit Fund Act, 2013 na marekebisho ya Sheria ya Ushuru wa Bidhaa ya mwaka 2013 (The

27

Excise (Management and Tariff) (Amendment) Act, 2013) yaliyopitishwa na Bunge katika Mkutano wa 13 mwezi Desemba, 2013 yaliyolenga kuondoa kodi ya ushuru wa bidhaa kwenye Sim Card.

56. Mheshimiwa Spika, Wizara pia iliandaa Kanuni mbalimbali ili kuwezesha usimamizi na utekelezaji wa Sheria za fedha. Kanuni hizo ni pamoja na Kanuni za Kodi ya Mapato kuhusu Gharama za Kuhamisha -Transfer Pricing Regulations, 2013, Kanuni za Sheria ya Ununuzi wa Umma, 2013 - Public Procurement Regulations, 2013, Kanuni za Uanzishwaji wa Baraza la Usuluhishi wa Bima, 2013 -The Insurance Ombudsman Regulation, 2013, Kanuni za Uanzishwaji wa chombo cha kushughulikia Rufaa za masuala ya Bima, 2013 -The Insurance Appeals Tribunal Regulations, 2013 na Kanuni za Bima Ndogo – The Micro-Insurance Regulations, 2013.

57. Mheshimiwa Spika, katika mkutano wa Bunge la Bajeti unaoendelea Wizara inatarajia kuwasilisha Muswada wa kutunga Sheria mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani - Value Added Tax -VAT na Sheria ya Usimamizi wa Kodi - Tax Administration Act.

58. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara itakamilisha maandalizi ya kufanyia marekebisho Sheria ya Msajili wa Hazina - Treasury Registrar Act, Sheria ya Takwimu (Statistics Act) na Sheria ya Fedha za Umma -Public Finance Act. Aidha, Wizara ipo katika maandalizi ya kuwezesha kutungwa kwa Sheria ya Kodi ya Hoteli -Hotels Tax Act na kufanya

28

marekebisho ya Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana za Serikali - Government Loans, Grants and Guarantees Act.

Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi – PPP

59. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kupokea na kuchambua maandiko ya miradi inayokusudiwa kutekelezwa kwa utaratibu wa ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Katika mwaka 2013/14, Wizara imepokea na kuchambua miradi minne ya PPP. Katika uchambuzi wa miradi imebainika kwamba kuna upungufu katika upembuzi yakinifu pamoja na ukosefu wa Wataalam wa kufanya upembuzi huo. Aidha, Wizara imeshiriki kutoa mapendekezo ya kurekebisha Sheria ya Ubia Na. 18 ya mwaka 2010 pamoja na kanuni zake kwa lengo la kuweka usimamizi mzuri wa ubia.

60. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15 Wizara imetenga fedha za kuanzisha Mfuko wa Kuwezesha Utekelezaji wa Miradi ya Ubia -PPP Facilitation Fund.

Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi

61. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara kupitia Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu imepokea na kuchambua taarifa 46 za miamala shuku inayohusu fedha haramu na ufadhili wa ugaidi na taarifa 14 za kiintelijensia

29

zimewasilishwa kwenye vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria. Aidha, mafunzo ya kudhibiti fedha haramu na ufadhili wa ugaidi yametolewa kwa watoa taarifa 135 na washiriki 86 kutoka katika vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu na Mali Athirika. Vile vile, mafunzo hayo yametolewa kwa washiriki 49 kutoka Mamlaka za Udhibiti.

62. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara kupitia Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu itatekeleza yafuatayo: kupokea na kuchambua taarifa za miamala shuku inayohusu utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi; kutoa mafunzo kwa vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria na kwa watoa taarifa; kutoa miongozo ya kudhibiti fedha haramu na ufadhili wa ugaidi kwa watoa taarifa; kuratibu zoezi la kutathmini mianya na viashiria vya fedha haramu na ufadhili wa ugaidi katika sekta mbalimbali nchini; na kuendelea na hatua za kujiunga na Umoja wa Kupambana na Biashara ya Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi Duniani - EGMONT Group of Financial Intelligence Units.

Tume ya Pamoja ya Fedha

63. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara kupitia Tume ya Pamoja ya Fedha imekamilisha Stadi ya Kubainisha Mfumo Bora wa Kodi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na kuendelea na

30

Uchambuzi wa Uhusiano wa Mwenendo wa Uchumi na Mapato ya Muungano.

64. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara kupitia Tume ya Pamoja ya Fedha inatarajia kukamilisha Stadi ya Kubainisha Mwenendo wa Uchumi na Mapato ya Muungano wa Tanzania, na kufanya Stadi ya Uwekezaji katika Mambo ya Muungano. Aidha, Tume inatarajia kuhuisha Takwimu mbalimbali za Stadi zilizofanywa na Tume.

Habari, Elimu na Mawasiliano kwa Umma

65. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kwamba Wadau mbalimbali wanapata taarifa zinazohusu kazi na majukumu ya Wizara, Wizara imetoa elimu kwa umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Aidha, Wizara imeandaa machapisho na vipeperushi kwa ajili ya kuelezea mafanikio, changamoto na njia zilizotumika katika kukabiliana na changamoto hizo.

66. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara itaendelea kuandaa taarifa kuhusu utekelezaji wa majukumu yake na kuelimisha umma kupitia vyombo vya habari, maonesho, machapisho na vipeperushi. Aidha, Wizara itakamilisha Mkakati wa Mawasiliano.

Masuala ya Watumishi

67. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kujenga uwezo wake ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Hatua hizo ni

31

pamoja na: kupeleka watumishi katika mafunzo ya muda mfupi na mrefu, kuajiri watumishi 10, kuthibitisha watumishi 21 kazini, kupandisha vyeo watumishi 131, kuboresha mazingira ya kazi kwa kukarabati baadhi ya ofisi na kununua vifaa vya ofisi. Aidha, Wizara imeendelea kutoa huduma stahiki kwa Watumishi wa Wizara wanaoishi na virusi vya UKIMWI na kutoa elimu ya afya kwa wafanyakazi.

68. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara inatarajia kuajiri watumishi 257 wa kada mbalimbali; kupandisha vyeo watumishi 490; na kuthibitisha kazini watumishi 10. Aidha, Wizara inatarajia kuwapatia watumishi 642 mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao, kutoa elimu kuhusu magonjwa sugu na kutoa huduma stahiki kwa watumishi wa wizara wanaoishi na virusi vya UKIMWI.

Usimamizi wa Mashirika na Taasisi za Umma

69. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imechambua na kutangaza katika Gazeti la Serikali mashirika 10 ambayo yanatakiwa kuchangia asilimia 10 ya mapato ghafi katika Mfuko Mkuu wa Serikali. Hadi kufikia Aprili 2014, kiasi cha shilingi bilioni 25.0 kimekusanywa ikiwa ni asilimia 69.4 ya makadirio ya kukusanya shilingi bilioni 36 kwa mwaka 2013/14.

32

Aidha, katika kutekeleza zoezi la kuingia mikataba ya utendaji na Bodi za mashirika ya umma, Wizara inakamilisha majadiliano na Bodi za mashirika ya umma. Vile vile, zoezi la kumpata Msajili wa Hazina limefikia hatua za mwisho. Matarajio ni kwamba uteuzi utafanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha.

70. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara inatarajia kutekeleza yafuatayo: kusimamia utendaji wa Bodi za Wakurugenzi wa mashirika na taasisi za umma na kuingia mikataba ya utendaji na Bodi za mashirika ya umma; kusimamia mikakati ya kurekebisha mashirika ya umma na kufanya tathmini na ufuatiliaji wa Mashirika ya Umma yaliyobinafsishwa; na kuimarisha usimamizi wa mashirika na taasisi za umma ili kuongeza mapato ya Serikali.

71. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara kupitia Shirika Hodhi la Mali za Umma (CHC) imeendelea na zoezi la ubinafsishaji na urekebishaji wa mashirika ya Umma. Wizara inaendelea na zoezi la tathmini ya utendaji wa mashirika mengine yaliyobinafsishwa kwa lengo la kufahamu kama makubaliano ya mikataba ya mauzo yanazingatiwa na kuchukua hatua stahiki.

Mafao ya Wastaafu na Mirathi

72. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuboresha kumbukumbu za Wastaafu, kulipa mafao na michango

33

ya kisheria kwa wakati. Hadi Aprili 2014, kumbukumbu za wastaafu 142,014 zimehifadhiwa kwenye mfumo wa kompyuta - SAPERION na shilingi bilioni 220.79 sawa na asilimia 87 ya makadirio kimelipwa kama mafao ya wastaafu wanaolipwa Pensheni na Hazina. Aidha, Wizara imefanya uhakiki wa wastaafu walio kwenye Daftari la Pensheni la Hazina katika mikoa tisa. Vile vile, shilingi bilioni 522.86 sawa na asilimia 76 ya makadirio ya mwaka kimelipwa kama michango ya mwajiri kwa watumishi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa wanaochangia kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na michango ya Bima ya Afya.

73. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusimamia na kuratibu shughuli za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma - PSPF, Mfuko wa Pensheni wa PPF na Mfuko wa Mafao ya Kustaafu - GEPF. Utekelezaji wa Mifuko hiyo kwa mwaka 2013/14 ulikuwa kama ifuatavyo:

Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma - PSPF

74. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2014, Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma ulikusanya shilingi bilioni 492.29 ambapo kati ya hizo michango ya wanachama ni shilingi bilioni 402.24 na mapato yatokanayo na vitega uchumi ni shilingi bilioni 90.05. Aidha, shilingi bilioni 490.95 zilitumika kulipa mafao ikiwa ni pamoja na mafao ya kiinua mgongo na pensheni za kila mwezi. Katika mwaka 2014/15, Mfuko unatarajia kukusanya jumla ya shilingi bilioni 798.12 kutoka vyanzo mbalimbali.

34

Mfuko wa Mafao ya Kustaafu - GEPF

75. Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Mafao ya Kustaafu wa GEPF ambao awali ulikuwa ukijulikana kama Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini, umebadili mfumo wa malipo ya mafao kutoka akiba na kwenda kwenye mfumo wa pensheni. Mabadiliko haya yamefanywa kwa mujibu wa Sheria Na. 8 ya mwaka 2013 iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hadi Aprili 2014, Mfuko umeweza kusajili jumla ya wanachama 10,289 ambapo wanachama 8,138 ni kutoka sekta isiyo rasmi. Aidha, michango ya wanachama ilifikia kiasi cha shilingi bilioni 31.68 sawa na asilimia 79.95 ya lengo la kukusanya jumla ya shilingi bilioni 39.62 ifikapo Juni 2014. Vile vile, mapato yatokanayo na vitega uchumi yamefikia shilingi bilioni 17.86 ambayo ni sawa na asilimia 84 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 21.26 kufikia Juni 2014. Thamani ya Mfuko hadi mwezi Aprili 2014 imekua na kufikia shilingi bilioni 239.56.

76. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Mfuko utaendelea na jitihada zake za kupanua wigo wa wanachama na hivyo kusajili wanachama zaidi katika sekta zote kwa maana ya sekta rasmi na sekta isiyo rasmi. Mfuko unatarajia kusajili jumla ya wanachama 23,190 na kukusanya michango yenye thamani ya shilingi bilioni 47.54. Aidha, mapato yanayotokana na vitega uchumi yanatarajiwa kuongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 23.99. Thamani ya Mfuko inategemea kukua hadi kufikia shilingi bilioni 310 ifikapo Juni, 2015.

35

Mfuko wa Pensheni wa PPF

77. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013, Mfuko wa Pensheni wa PPF ulikusanya shilingi bilioni 278.57 ikiwa ni michango ya wanachama ambayo ni ongezeko la asilimia 18 ikilinganishwa na shilingi bilioni 235.89 zilizokusanywa mwaka 2012. Aidha, idadi ya wanachama wanaochangia katika Mfuko imeongezeka kufikia wanachama 247,418 kutoka wanachama 203,981 mwaka 2012. Vile vile, mapato yatokanayo na uwekezaji yaliongezeka kufikia shilingi bilioni 305.2 kutoka shilingi bilioni 111.15 mwaka 2012 ikiwa ni ongezeko la asilimia 174.5. Kadhalika, thamani ya mfuko imeongezeka kufikia shilingi trilioni 1.49 ikiwa ni ongezeko la asilimia 36.5 ikilinganishwa na thamani ya mfuko ya shilingi trilioni 1.092 ilivyokuwa mwaka 2012.

78. Mheshimiwa Spika, Thamani ya Mfuko inategemea kukua hadi kufikia shilingi trilioni 1.729 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2014. Aidha, mapato ya uwekezaji yanatarajiwa kufikia shilingi bilioni 180.64. Vile vile, Mfuko unategemea kuandikisha jumla ya wanachama 80,000 kutoka katika sekta ya Umma na binafsi.

Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA

79. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2014, mapato halisi ya kodi yalifikia shilingi bilioni 7,771.5 sawa na asilimia 75 ya lengo la mwaka la kukusanya shilingi bilioni 10,395.4. Kodi zilizochangia zaidi ni

36

pamoja na Kodi ya Ongezeko la Thamani, Kodi ya Kampuni na Kodi ya Mapato ya Ajira ambazo kwa pamoja zilichangia zaidi ya asilimia 80 ya mapato hayo.

80. Mheshimiwa Spika, licha ya hatua mbali mbali ambazo zimechukuliwa katika kipindi cha mwaka 2013/14, kumekuwa na changamoto katika kufikia lengo la makusanyo ya mapato. Sababu zilizochangia kutofikia malengo ni pamoja na: mapato pungufu ya Kodi ya Kampuni kuliko ilivyotarajiwa kutoka kwenye baadhi ya kampuni za madini; kushuka kwa makusanyo hususan Kodi ya Zuio kutokana na kupungua kwa makusanyo kwenye shughuli za utafiti wa gesi na mafuta. Sababu nyingine ni pamoja na kufutwa kwa Tozo ya Kadi za Simu SIMcard levy; na makusanyo hafifu kutoka kwenye Ushuru wa Bidhaa wa Huduma za Uhawilisho wa Fedha (Money Transfers). Kwa upande wa Forodha sababu zilizochangia kutofikiwa kwa lengo la makusanyo ni ukuaji mdogo wa uingizwaji wa bidhaa kutoka nje, na ongezeko la kuingiza bidhaa kupitia njia zisizo rasmi (panya roads) na bandari bubu.

81. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kudhibiti ukwepaji kodi, wizara kupitia TRA inachukua hatua kadhaa za kudhibiti upotevu wa mapato kupitia bandari bubu na panya roads, kwa kufanya upelelezi ili kuzigundua njia hizo na kuzidhibiti kwa kutumia Kikosi Kazi cha Kuzuia Magendo (Flexible Anti-Smuggling Team). Aidha, elimu kwa wafanyabiashara na wananchi wanaozunguka eneo la Pwani imeendelea kutolewa, ushirikiano na vyombo vingine vya udhibiti yaani Polisi

37

Uhamiaji na Usalama wa Taifa umeanzishwa; na kufanya doria katika maeneo hayo.

82. Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuimarisha makusanyo ya kodi, Mamlaka inaendelea kuimarisha matumizi ya Mashine za Kieletroniki za kutoa Risiti (Electronic Fiscal Devices-EFDs) ambapo kwa sasa inakamilisha zoezi la kuwaingiza wafanyabiashara wote wanaostahili kuanza kutumia mashine hizo, kuanzisha Mfumo wa Uthamini wa Mizigo ya Forodha Tanzania Customs Integrated System-TANCIS ambao umeanza kutumika mwezi Aprili 2014 pamoja matumizi ya mfumo wa kuthamini magari chakavu; na, kuanzisha Kitengo cha Kodi ya Kampuni za Kimataifa International Tax Unit kwa lengo la kubaini na kudhibiti mianya ya kupotea kwa kodi inayolipwa na kampuni za kimataifa zilizowekeza nchini.

83. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania imeanza kutekeleza makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuweka mazingira ya kuanzishwa kwa Mfumo wa Himaya Moja ya Forodha (Single Customs Territory - SCT) kuanzia Januari, 2014. Ili kuhakikisha kwamba mizigo ya nchi jirani haiuzwi nchini kinyume na utaratibu wa forodha, mfumo wa ki-eletroniki wa ufuatiliaji wa mizigo inayosafirishwa utatumika. Kupitia mfumo huu, mizigo na ama vyombo vya usafirishaji hufungwa lakili ya ki-eletroniki (electronic seal) na kifaa cha mawasilaino ambavyo huunganishwa na mfumo mkuu ili kuonesha

38

mwenendo mzima wa usafiri hadi mzigo husika utakapovuka mpaka wa nchi. Aidha, mbinu nyingine za udhibiti saidizi kama doria, usuluhishi wa taarifa (reconciliation) na ukaguzi zitatumika ili kuongeza udhibiti.

Rufaa za Kodi

84. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Bodi ya Rufaa za Kodi, imepokea jumla ya rufaa 129 na maombi 37, na imesikiliza na kutolea maamuzi rufaa 116 na maombi 28. Aidha, Bodi ipo katika hatua ya kuchapisha Ripoti ya Maamuzi ya Rufaa za Kodi zilizoamuliwa kuanzia mwaka 2009 - 2010. Kwa upande wa Baraza la Rufaa za Kodi, jumla ya rufaa 34 na maombi 4 yamepokelewa ambapo rufaa 41 na maombi 9 yamesikilizwa na kutolewa maamuzi. Idadi hii inajumuisha rufaa na maombi ambayo hayakusikilizwa mwaka 2012/13.

85. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara kupitia Bodi ya Rufaa na Baraza la Rufaa za Kodi itaendelea kupokea, kusikiliza na kutolea maamuzi rufaa za kodi; kutoa elimu kwa walipa kodi juu ya taratibu za kukata rufaa za kodi; na kutoa mafunzo kwa wajumbe wa Bodi na Baraza juu ya taratibu za kutatua migogoro ya kodi itokanayo na sheria za Kodi zinazosimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Aidha, Bodi ya Rufaa na Baraza la Rufaa za Kodi linatarajia kuchapisha Ripoti ya Maamuzi ya Rufaa

39

za Kodi zinazojumuisha maamuzi yaliyotolewa mwaka 2011 hadi 2012 kwa ajili ya rejea kwa wadau wake.

Huduma za Kibenki

Benki Kuu ya Tanzania

86. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Benki Kuu imeendelea kusimamia Sekta ya Kibenki ambapo kati ya kipindi cha Machi 2013 na Machi 2014, idadi ya benki na taasisi za fedha imeongezeka kutoka 51 na matawi 585 hadi 53 na matawi 625 kote nchini. Jumla ya mali ya sekta ya kibenki imekua kutoka shilingi trilioni 17.9 hadi shilingi trilioni 21.1. Kiwango cha mitaji kilifikia wastani wa asilimia 18.5 ikilinganishwa na kiwango cha asilimia 10 kinachotakiwa kwa mujibu wa sheria. Aidha, Mfumo wa Taarifa za Wakopaji Credit Reference Bureau unaendelea vyema, ambapo hadi sasa kampuni mbili zimepewa leseni ambazo ni: kampuni ya Creditinfo Tanzania Limited iliyoanza kazi Juni 2013, na kampuni ya Dun & Bradstreet Credit Bureau (T) Limited iliyoanza kazi Septemba 2013. Kampuni nyingine kwa jina la Transunion, nayo hivi karibuni imepewa leseni ya muda na inajiandaa kuanza kufanya kazi.

87. Mheshimiwa Spika, Kampuni hizi kwa sasa zinaandaa taarifa za wateja kutoka kwenye kumbukumbu ambazo zinahifadhiwa Benki Kuu. Taarifa hizi bado zinafanyiwa uhakiki kabla ya kuanza kutumika rasmi. Mara baada ya data bank hiyo

40

kukamilika, makampuni haya ya Credit Reference yataanza kufanya kazi hiyo kikamilifu na kwa usahihi. Benki Kuu inaendelea kuyahimiza mabenki ambayo bado hayajawasilisha taarifa kufanya hivyo.

88. Mheshimiwa Spika, Tarehe 30 Novemba 2013, Marais wa Afrika Mashariki walitia sahihi Itifaki ya Umoja wa Fedha ya Afrika Mashariki. Tukio hili, ndilo limeanzisha safari yetu ya kwenda kwenye hatua ya kuwa na sarafu moja ifikapo mwaka 2024. Chini ya Itifaki hii, tumekubaliana vigezo ambavyo tutatakiwa tufikie kabla ya kuingia kwenye umoja huo na road map ya miaka 10 ambayo itaanza kutekelezwa mara tu baada ya nchi zote kuridhia utekelezaji wake. Katika mpango huo, mambo muhimu ni; kukamilisha utekelezaji wa Umoja wa forodha na Itifaki ya soko la pamoja; kuoanisha mifumo ya kifedh, sera za ubadilishaji wa fedha za kigeni, sera za bajeti, na mifumo ya malipo; uhuisha mifumo ya takwimu na; kuhuisha sheria zote zinazohusiana na uanzishwaji wa umoja wa kifedha

Benki ya Maendeleo TIB - TIB Development Bank

89. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, TIB Development Bank (zamani Benki ya Rasilimali) iliendelea na marekebisho ya ndani ambapo shughuli za

41

Benki zimegawanywa katika kampuni mbili ambazo ni TIB Development Bank Limited inayohusika na shughuli za maendeleo na TIB Corporate Finance Limited inayohusika na shughuli za biashara.

90. Mheshimiwa Spika, katika mwaka ulioishia Desemba 2013, Benki ya Maendeleo TIB ilipata faida (kabla ya kodi) ya shilingi bilioni 11.9 ikiwa ni ongezeko la asilimia 78 toka shilingi bilioni 6.7 zilizopatikana mwaka ulioishia Desemba 2012. Aidha, waraka mizania wa benki ulifikia shilingi bilioni 408.7 ikilinganishwa na shilingi bilioni 338.4 Desemba 2012; Mikopo iliongezeka kufikia shilingi bilioni 307.0 toka shilingi bilioni 242.9 Desemba 2012.

91. Mheshimiwa Spika, Dirisha la Kilimo katika Benki ya Maendeleo TIB liliendelea kutoa mikopo kwa wakopaji mbalimbali kwa riba nafuu. Tangu kuanza kwa Dirisha mwaka 2010 hadi kufikia Aprili 2014, maombi yenye thamani ya shilingi bilioni 58.8 yaliidhinishwa. Kati ya hizo, shilingi bilioni 33.6 zilikopeshwa kwa kampuni za wakulima wadogo na wa kati, shilingi bilioni 8.7 zilienda kwa taasisi ndogo za fedha zinazokopesha wakulima wadogo na wa kati; na shilingi bilioni 16.5 zilikopeshwa kwa vikundi vya kuweka na kukopa (SACCOS).

Benki ya Maendeleo ya Kilimo - TADB

92. Mheshimiwa Spika, kufuatia uamuzi wa Serikali kuanzisha Benki ya Kilimo, Wizara imetekeleza yafuatayo: kuzindua Bodi ya Wakurugenzi wa Benki;

42

kukamilisha zoezi la upatikanaji wa Mtendaji Mkuu na Wakuu wa Idara; kuandaa Muundo wa Benki na Muundo wa Utumishi; kuandaa majukumu ya wafanyakazi; kuandaa rasimu ya Mpango wa Biashara; na kupatikana kwa ofisi za Benki. Mwaka 2014/15, Benki ya Maendeleo ya Kilimo inatarajia kupata leseni ya biashara, kuajiri wafanyakazi na kuanza kutoa huduma.

Twiga Bancorp

93. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Twiga Bancorp imeendelea kutoa huduma kwa kutumia matawi makubwa matano na madogo matano. Hadi kufikia Aprili 2014, mikopo ya shilingi bilioni 41.9 ilitolewa kwa wateja mbalimbali. Uwekezaji kwenye Dhamana za Serikali na Amana katika Benki zingine ulikuwa shilingi bilioni 3.6 na mapato yaliyokusanywa na Taasisi yalifikia ya shilingi bilioni 3.86.

94. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15 Wizara itaendelea kuboresha utendaji wa Taasisi kwa kuimarisha uongozi. Aidha, Taasisi itaongeza wigo wa huduma kwa kuanzisha huduma mbalimbali kama vile Max Malipo, Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money na biashara kwa uwakala. Vile vile, Taasisi inatarajia kufungua tawi jipya Kigamboni.

Benki ya Posta – TPB

95. Mheshimiwa Spika, katika kupanua wigo wa biashara na kupeleka huduma za kibenki vijijini, Benki ya Posta kupitia ofisi za Shirika la Posta Tanzania

43

imeziunganisha ofisi nane za Tunduma, Makambako, Peramiho, Masasi, Njombe, Nachingwea, Kilwa na Kahama katika mtandao wa TEHAMA na hivyo kuongeza idadi ya ofisi za Shirika la Posta ambazo zinatoa huduma za kibenki kufikia 17. Aidha, huduma kwa wateja zilitolewa kwa kutumia mashine 185 za ATM.

96. Mheshimiwa Spika, amana za wateja ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 138.86 mwaka 2012 hadi kufikia shilingi bilioni 170.03 mwaka 2013 sawa na ongezeko la asilimia 22.4. Aidha, uwekezaji katika dhamana za Serikali uliongezeka kutoka shilingi bilioni 39.67 hadi kufikia shilingi bilioni 45.73 katika kipindi hicho sawa na ongezeko la asilimia 19.8. Aidha, thamani ya mikopo inayotolewa kwa wateja iliongezeka kutoka shilingi bilioni 100.89 hadi kufikia shilingi bilioni 119.73 ikiwa ni ukuaji wa asilimia 18.7. Vile vile, faida kabla ya kodi imeongezeka kutoka shilingi bilioni 5.67 hadi kufikia shilingi bilioni 6.99 sawa na ongezeko la asilimia 23.4.

97. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014, TPB inatarajia kufikia malengo yafuatayo: kukuza rasilimali za benki hadi kufikia shilingi bilioni 237.10; kuongeza idadi ya wateja wapya 300,000; kuongeza amana za wateja kufikia shilingi bilioni 200.10; kuongeza mikopo ya wateja kufikia shilingi bilioni 47.16; kupata faida kabla ya kodi ya shilingi bilioni 8; na kuendelea na taratibu za kurekebisha sheria iliyoianzisha Benki ili kuisajili chini ya Sheria ya Kampuni.

44

Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Kifedha

98. Mheshimiwa Spika, Wizara imeanza kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Kifedha - National Microfinance Policy, 2000 ili kuondoa mapungufu ya kisheria yaliyojitokeza katika utekelezaji wake kwa lengo la kuzingatia mabadiliko ya kiuchumi na kijamii pamoja na kuweka mazingira mazuri katika ukuaji wa sekta hiyo. Aidha, katika mwaka 2014/15, Wizara itakamilisha maandalizi ya Sera ya Taifa ya Taasisi Ndogo za Huduma za fedha pamoja na kutunga Sheria ya Taasisi ndogo za huduma za kifedha - Microfinance Act.

Huduma za Bima

Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima – TIRA

99. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima imekamilisha na kutoa Mkakati wa Kuendeleza Bima ya Watu wa Kipato cha Chini - National Micro Insurance Strategy 2014-2017. Aidha, hadi kufikia Aprili 2014, kampuni 30, madalali 100 na mawakala 500 wa bima walisajiliwa. Vile vile, mauzo ya bima yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 406.7 mwaka 2012/13 hadi kufikia shilingi bilioni 481.7 sawa na ongezeko la asilimia 18.5.

100. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, TIRA inatarajia kutekeleza yafuatayo: kuendelea na maandalizi ya kufungua ofisi nyingine za kanda;

45

kuendelea na utaratibu wa uoanishaji sheria na kanuni za soko la bima katika eneo la Afrika Mashariki na lile la nchi za SADC; kuendelea na tafiti za bima ya kilimo, mifugo, pamoja na bima za watu wa kipato cha chini; na kukamilisha taratibu za kuanzisha bima ya Takaful.

Shirika la Bima la Taifa – NIC

101. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara ilikamilisha urekebishaji wa Shirika la Bima la Taifa na usimikaji wa mfumo wa TEHAMA kwa lengo la kuongeza ufanisi. Utendaji wa Shirika kibiashara uliendelea kuimarika ambapo mapato ya bima yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 27.38 mwaka 2012, hadi kufikia shilingi bilioni 31.53 mwaka 2013, ongezeko hilo ni sawa na asilimia 15. Mapato haya yalitokana na makusanyo ya bima za mtawanyo, vitega uchumi na mapato mengine.

102. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Desemba 2013, NIC ililipa madai ya wateja ya shilingi bilioni 8.31. Malipo hayo yalilipwa kwa wateja wa bima za maisha kiasi cha shilingi bilioni 5.71 na wateja wa bima za kawaida kiasi cha shilingi bilioni 2.60.

103. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/15, Wizara itaendelea na mkakati wa kuligawa Shirika katika kampuni mbili, ambayo ni Kampuni ya Bima za Maisha na Kampuni ya Bima za Kawaida. Aidha, Shirika litaendelea na mkakati wa kujitangaza zaidi na

46

kuongeza biashara kwa kubuni bima mpya zinazokidhi mahitaji ya wananchi.

Masoko ya Mitaji na Dhamana

Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana

104. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana imeendelea kusimamia Soko la Hisa la Dar es Salaam, kampuni za udalali na ushauri wa uwekezaji, mipango ya uwekezaji wa pamoja na kampuni zilizoorodheshwa kwenye Soko la Hisa . Aidha, Mamlaka imetekeleza yafuatayo: kuzindua Soko la Kukuza Kampuni na Ujasiriamali ambapo Benki ya Maendeleo iliorodhesha hisa zake; na kuendelea na maandalizi ya uanzishwaji wa soko la Hatifungani za Manispaa.

105. Mheshimiwa Spika, katika kutimiza azma ya Serikali ya kuhakikisha kampuni za Mawasiliano, Gesi na Madini zinaorodhesha hisa zake kwenye soko la Hisa la Dar es Salaam, Wizara kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana kwa kushirikiana na wadau iliandaa taratibu zinazotakiwa kuzingatiwa. Aidha, Mamlaka iliendelea kuelimisha umma kuhusu masoko ya mitaji na uwekezaji kwa kupitia warsha, matangazo katika vyombo vya habari, vipeperushi na machapisho.

106. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana imepanga kutekeleza yafuatayo: kukamilisha maandalizi kwa ajili ya uzinduzi wa Soko la Bidhaa; kuzindua mfumo wa uwekezaji kwa kutumia mitandao

47

ya simu za mikononi (M-akiba) kwa wawekezaji wadogo; kutayarisha taratibu za kisheria na usimamizi wa bidhaa na huduma mpya zinazotarajiwa kuingizwa sokoni zikiwemo hatifungani za halmashauri; kukamilisha uandaaji wa Mpango Mkuu wa Kitaifa wa Maendeleo ya Masoko ya Mitaji na; kuanzisha misingi ya kusimamia masoko kwa kuzingatia uzito wa athari. Aidha, Mamlaka itaendelea kuboresha programu ya elimu kwa umma ili kuboresha na kupanua ushiriki wa wananchi katika masoko ya mitaji.

107. Mheshimiwa Spika, Serikali iko katika hatua za mwisho za kupata taasisi mbili zitakazoendesha zoezi la tathmini ya kupima uwezo wa nchi wa kukopa na kulipa madeni yake. Mwezi Februari 2014, Wizara iliziandikia kampuni za Fitch, Moody’s Investment Services na Standard and poors kuwasilisha fomu zao za mikataba kwa hatua za uchambuzi. Tayari kampuni ya Fitch na Moody’s zimewasilisha fomu za mikataba kupitia kwa mshauri mwelekezi Citi Group. Aidha, kuchelewa kwa zoezi hili kulitokana na kampuni hizi za upimaji (Rating Agencies) kutokukubaliana na aina ya fomu za mikataba zinazoandaliwa na serikali pamoja na kuleta nyongeza ya gharama nje ya makubaliano yaliyosainiwa awali.

Soko la Hisa Dar es Salaam

108. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Soko la Hisa Dar es Salaam liliorodhesha Hatifungani za Serikali zenye thamani ya shilingi bilioni 690 ambazo ni asilimia 83 ya makadirio ya mwaka. Kwa upande wa hisa za kampuni, Soko liliorodhesha hisa za Benki ya

48

Maendeleo zenye thamani ya shilingi bilioni 4.5 na hisa za ziada na upendeleo za kampuni ya TOL Gases Ltd zenye thamani ya shilingi bilioni 4.5. Aidha, Kampuni ya Swala Oil and Gas (T) Ltd (Australia), Mwanza Community Bank ya mkoani Mwanza na Uchumi Supermarket (Kenya) ziliwasilisha maombi ya kuorodheshwa. Maombi haya yako katika hatua mbalimbali za kuidhinishwa.

109. Mheshimiwa Spika, Thamani ya soko imeongezeka kutoka shilingi trilioni 14.10 Julai 2013 hadi shilingi trilioni 18.06 Aprili 2014, ambayo ni sawa na asilimia 28. Mafanikio haya yametokana na ongezeko la bei ya hisa za kampuni zilizoorodheshwa pamoja na kuorodheshwa kwa kampuni mpya sokoni. Aidha, idadi ya wawekezaji iliongezeka kutoka 180,458 mwezi Julai 2013 hadi 192,419 mwezi Aprili 2014.

110. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2013 hadi Aprili 2014 hisa zenye thamani ya shilingi bilioni 245 ziliuzwa na kununuliwa. Aidha, hatifungani za Serikali zenye thamani ya shilingi bilioni 286 ziliuzwa. Kwa ujumla mwenendo wa shughuli za Soko katika kipindi kilichoishia Aprili 2014 ulikuwa wa kuridhisha na viashiria vya mwenendo wa soko vinaonesha mwelekeo chanya.

111. Mheshimiwa Spika, shughuli nyingine zilizotekelezwa na Soko la Hisa Dar es Salaam ni pamoja na: uboreshaji wa Mfumo wa Mnada kwa kuweka Mfumo Mpana – Wide Area Network

49

unaowawezesha madalali kuuza na kununua hisa wakiwa mahali popote nchini. Aidha, Soko la Hisa Dar es Salaam limekamilisha ukarabati wa jengo la Ofisi Mbadala Wakati wa Majanga – Disaster Recovery Site na jengo hilo limeanza kutumika.

112. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Soko la Hisa Dar es Salaam linatarajia kutekeleza yafuatayo: kuendelea kuhamasisha na kuelimisha kampuni umuhimu wa kujiorodhesha Sokoni; kurahisisha shughuli za minada kwa kutumia simu na intaneti; kuboresha mfumo wa kuuza na kununua hisa sokoni; na kuendelea na juhudi mbalimbali zinazolenga kuongeza ufahamu wa masuala ya masoko ya mitaji kwa umma.

Dhamana ya Uwekezaji Tanzania – UTT

113. Mheshimiwa Spika, Dhamana ya Uwekezaji Tanzania imebadilisha muundo wake na kuanzisha taasisi ndogo tatu ambazo ni: Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT Project and Infrastructure Development Plc), Taasisi ya Utoaji Mikopo (UTT Microfinance Institution – UTT MFI), na Taasisi ya Usimamizi wa Rasilimali za Uwekezaji na Huduma Kwa Wawekezaji (UTT Asset Management and Investor Services - UTT AMIS). Hadi kufikia Aprili, 2014 mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 4.3 imetolewa na UTT MFI kwa wananchi 5,785, wanawake wakiwa 4,744 na wanaume 1,041.

50

114. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, UTT MFI inatarajia kuanzisha aina mpya ya mikopo ili kukidhi mahitaji mbalimbali ya wananchi. Mikopo hiyo ni: mikopo kwa ajili ya wafanyabiashara na wakandarasi; mikopo kwa ajili ya huduma za afya; mikopo kwa ajili ya kilimo na viwanda vidogo vidogo; mikopo kwa wakala wa huduma za fedha; na mikopo ya matengenezo ya nyumba.

115. Mheshimiwa Spika, UTT AMIS inasimamia mifuko mitano ya uwekezaji wa pamoja ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Jikimu na Mfuko wa Ukwasi. Katika kipindi cha Julai 2013 hadi Aprili, 2014, thamani ya mifuko hiyo iliongezeka kutoka shilingi bilioni 119.03 hadi shilingi bilioni 167.37 sawa na ongezeko la asilimia 40.62. Ongezeko hili lilitokana na mauzo ya vipande pamoja na ongezeko la thamani za rasilimali za Dhamana ya Uwekezaji. Katika mwaka 2014/15, UTT AMIS imepanga kuanzisha mfuko wa uwekezaji wa pamoja katika majumba (Real Estate Investment Trust – REIT).

Taasisi za Kitaalam na Huduma Nyinginezo

Ofisi ya Taifa ya Takwimu

116. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetekeleza yafuatayo: kutayarisha takwimu za mfumuko wa bei kila mwezi; kutayarisha na kusambaza Takwimu za Pato la Taifa kwa Robo ya Kwanza na ya pili ya mwaka 2013;

51

kutayarisha Takwimu za Pato la Taifa kwa mwaka 2013 kwa bei za mwaka 2001; na kukamilisha matokeo ya awali ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Nchini wa Mwaka 2012. Aidha, Ofisi ya Taifa ya Takwimu imefanya uchambuzi wa taarifa mbalimbali za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 na kutoa Chapisho la Kwanza la Mgawanyo wa Watu kwa Umri na Jinsia katika Ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya, Kata na Shehia; Chapisho la Pili lenye Taarifa za Msingi za Mgawanyo wa Watu Kiumri na Kijinsia. Vile vile, Chapisho la Tatu lenye Taarifa za Msingi za Kidemografia, Kijamii na Kiuchumi kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar limekamilika.

117. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Ofisi ya Taifa ya Takwimu itaendelea kuboresha takwimu rasmi za kiuchumi na kijamii na kutoa machapisho mbalimbali kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012. Aidha, Ofisi itaendelea kuboresha takwimu za Pato la Taifa kwa kurekebisha mwaka wa kizio wa bei za 2001 kwenda 2007 ikiwa ni moja ya hatua za kuboresha takwimu za kiuchumi na kijamii ili zilingane na hali halisi ya maendeleo ya uchumi. Vile vile, Ofisi ya Taifa ya Takwimu itaendelea kufanya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014; Utafiti wa Ajira na Bei wa Mwaka 2014; Sensa ya Viwanda ya Mwaka 2014; Utafiti wa Kilimo wa mwaka 2014/15; na kuendelea na maandalizi ya Sheria mpya ya Takwimu.

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu

52

118. Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2014, Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu imeendesha mafunzo ya kitaaluma na kuhudhuriwa na jumla ya washiriki 2,242. Aidha, Bodi imekamilisha silabi mpya ya mitihani ambapo mitihani ya kwanza inatarajiwa kufanyika Novemba, 2014. Vile vile, wahitimu 228 wamesajiliwa kama watunza vitabu; Wahasibu wahitimu wanaopatiwa uzoefu wa kazi 2,631; Wahasibu waliosajiliwa ngazi ya CPA 1,270; Wahasibu waliosajiliwa kama Wakaguzi wa Hesabu katika ngazi ya CPA-PP 492; Kampuni za Ukaguzi wa Hesabu zilizosajiliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu 170; na Kampuni za Uhasibu zilizosajiliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu 19. Vile vile, Bodi imeendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa Kituo cha Taaluma ya Uhasibu eneo la Bunju - Dar es Salaam unaotarajiwa kukamilika mwaka 2014/15.

Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi

119. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi imesajili wataalamu 2,404 katika ngazi mbalimbali kwa mujibu wa sheria. Aidha, Bodi imeendesha mafunzo ya kitaaluma yaliyolenga kuboresha uwezo wa utendaji unaozingatia maadili. Vile vile, Bodi imetahini jumla ya wanafunzi 2,455 ambapo wanafunzi 1,115 walifaulu hivyo kufanya idadi ya wahitimu kufikia 24,660. Bodi

53

pia imeendelea kutoa mafunzo ya vitendo kwa wahitimu kutoka vyuo vya elimu ya juu. Katika mwaka 2014/15, Bodi inatarajia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa kuboresha mitaala yake ili iendane na soko la ajira la Utandawazi.

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha

120. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha imeendelea kutekeleza majukumu yake ya kusimamia michezo ya kubahatisha ambapo hadi kufikia Aprili 2014, jumla ya kodi iliyokusanywa na Bodi ilifikia shilingi bilioni 10.78 sawa na ongezeko la asilimia 14.4. Aidha, Bodi ilichangia shilingi milioni 532.48 katika mfuko mkuu wa Serikali sawa na ongezeko la asilimia 0.85.

Taasisi za Mafunzo

Taasisi ya Uhasibu Arusha

121. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Taasisi ya Uhasibu Arusha imeendelea kutoa mafunzo

54

katika fani za uhasibu, ugavi, benki, Usimamizi wa Fedha, Usimamizi wa Rasilimali, Utawala wa Biashara, Teknolojia ya Habari na Sayansi ya Kompyuta na Masomo ya Kimkakati. Aidha, jumla ya wanafunzi 3,341 wamedahiliwa, ambapo kati yao wanaume ni 1,847 sawa na asilimia 55 na wanawake 1,494, sawa na asilimia 45.

122. Mheshimiwa Spika, Taasisi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Galgotias cha India imeanzisha mafunzo ya shahada za uzamili katika sayansi ya kompyuta ambazo ni Master in Software Engineering, Master in Information Security na Master in Computer Application. Aidha, Taasisi inaendesha E-learning Library ambayo imeonesha mafanikio makubwa na pia ipo katika hatua za awali za kuanzisha E-learning Center.

123. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2014/15, Taasisi inakusudia kuanzisha mafunzo katika: Shahada ya Uzamili ya Ununuzi na Ugavi, Shahada ya Mafunzo Mkakati -Bachelor in Strategic Studies, Shahada ya Sayansi ya Kijeshi - Bachelor in Military Science na Stashahada ya uzamili katika mafunzo ya bima -Postgraduate Diploma in Insurance.

Chuo cha Usimamizi wa Fedha

55

124. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Chuo cha Usimamizi wa Fedha kilidahili jumla ya wanafunzi 9,998 katika fani mbalimbali. Kati ya hao wanawake 3,532 sawa na asilimia 35 na wanaume 6,466 sawa na asilimia 65. Aidha, Chuo kimeanzisha Shahada za Uzamili katika fani za Uhasibu na Fedha, Fedha na Uwekezaji na Rasilimali Watu. Vile vile, Chuo kimeanzisha tawi katika Jiji la Mwanza ambapo masomo kwa wanafunzi wa ngazi ya Cheti na Stashahada katika fani ya Uhasibu na Benki yalianza kutolewa mwaka 2013.

Taasisi ya Uhasibu Tanzania

125. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Taasisi ya Uhasibu Tanzania ilidahili jumla ya wanafunzi 9,769 kati ya hao wanawake 4,776 sawa na asilimia 49 na wanaume 4,993 sawa na asilimia 51 Aidha, Taasisi ilianzisha kozi mbili mpya ambazo ni Uhasibu katika Sekta ya Umma -Public Sector Accounting na Masoko na Uhusiano wa Umma -Markerting and Public Relations katika ngazi za Cheti, Stashahada na Shahada. Vile vile, Taasisi imeanza ujenzi wa jengo la mihadhara katika Kampasi ya Mtwara lenye uwezo wa kuchukua wanachuo 500.

126. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Taasisi inatarajia kudahili wanafunzi 9,729, kufungua tawi jipya katika mji wa Kigoma na kuendelea na ujenzi wa jengo katika Kampasi ya Mtwara.

56

Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini

127. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Chuo kimedahili jumla ya wanafunzi 5,052 kati yao wanawake 2,360 sawa na asilimia 47 na wanaume 2,692 sawa na asilimia 53. Aidha, wanafunzi 1,846 walihitimu masomo katika kozi mbalimbali ambapo kati ya hao wanaume ni 1,037 sawa na asilimia 56 na wanawake walikuwa 809 sawa na asilimia 44. Vile vile, Chuo kimekamilisha ujenzi wa jengo la pili la taaluma. Kadhalika Chuo kimetayarisha taarifa za Hali ya Uchumi na Kijamii za Wilaya (District Socio-Economic Profiles) za Halmashauri za Bunda, Ulanga, Kahama, Geita na Manispaa ya Dodoma.

128. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Chuo kitatoa mafunzo ya muda mfupi ya kujenga uwezo kwa watendaji namna ya kupanga, kutekeleza na kusimamia mipango ya maendeleo kwenye sehemu zao za kazi.

Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika

129. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Chuo kilidahili wanafunzi 269 kati ya hao wanawake 108 sawa na asilimia 40 na wanaume 161 sawa na asilimia 60. Aidha, Chuo kimeanzisha Shahada ya Uzamili katika Takwimu Rasmi na tayari chuo

57

kimedahili wanafunzi 32 kutoka nchi za Ethiopia, Ghana, Nigeria, Swaziland na Tanzania.

CHANGAMOTO

130. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu yake, Wizara ilikabiliwa na changamoto zifuatazo:

i. Kuongeza mapato ya ndani ya Serikali ili kukidhi mahitaji ya matumizi ya maendeleo na ya kawaida;

ii. Mabadiliko ya hali ya uchumi na uongozi katika nchi za washirika wa maendeleo ambapo zimepelekea kushindwa kutimizwa kwa baadhi ya miadi;

iii. Uwezo wa kusimamia mikataba katika kutekeleza baadhi ya miradi na programu za maendeleo; na

iv. Upatikanaji wa mikopo ya kibiashara kwa wakati kunakotokana na kubadilika kwa masharti kutoka kwa wakopeshaji.

131. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto hizo, Wizara imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na:

i. Kubuni vyanzo vipya vya mapato na kudhibiti matumizi pamoja na kupunguza upotevu wa mapato;

ii. Kuboresha ushirikiano na washirika wa maendeleo yenye lengo la kuwa na uelewa sawa kuhusu masuala mbali mbali katika ushirikiano wetu;

iii. Kuendelea kuzijengea uwezo Wizara, Taasisi na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kusimamia

58

na kutekeleza mikataba ya miradi na programu za maendeleo;

iv. Kuendelea kutekeleza Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma - “Public Financial Management Reform Programme (PFMRP)”; na

Kushauri Wizara, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzingatia vipaumbele wakati wa kupanga na utekelezaji kulingana na bajeti iliyotengwa.

v. Kuanza mazungumzo mapema na wakopeshaji wa mikopo ya kibiashara.

Mapitio ya Mapato na Matumizi ya Mafungu ya Wizara kwa Mwaka 2013/14

132. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, majukumu ya Wizara yalitekelezwa katika mafungu saba ya kibajeti. Mafungu hayo ni Fungu 50 - Wizara ya Fedha; Fungu 23 - Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali; Fungu 22 - Deni la Taifa; Fungu 21 – HAZINA; Fungu 13 - Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu; Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha; na Fungu 7 – Ofisi ya Msajili wa Hazina. Aidha, Fungu 45 - Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ambayo inajitegemea linaombewa fedha Bungeni na Waziri wa Fedha kwa mujibu wa Sheria.

Fungu 50 – Wizara ya Fedha

133. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Fungu 50 ilitarajia kupata shilingi bilioni 126.48 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato yasiyo ya kodi ambavyo ni mauzo ya mali, uuzaji wa nyaraka za zabuni na mapato

59

kutoka katika Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali (Gawio, Michango na Marejesho ya mikopo). Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014, makusanyo yalifikia shilingi bilioni 66.79 sawa na asilimia 52.81 ya lengo. Kiwango hicho kinatarajiwa kuongezeka katika robo ya nne ya mwaka wa fedha baada ya Mashirika mengi kuandaa hesabu za mwaka na ukaguzi wa hesabu hizo kukamilishwa.

134. Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya Fungu 50 kwa mwaka 2013/14 yalikuwa shilingi bilioni 54.71 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 233.67 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014, matumizi ya kawaida yalifikia shilingi bilioni 36.60 sawa na asilimia 66.89 ya makadirio na matumizi ya maendeleo yalifikia shilingi bilioni 219.97 sawa na asilimia 94.14 ya makadirio.

Fungu 23 – Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali

135. Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya Fungu 23 kwa mwaka 2013/14 yalikuwa shilingi bilioni 80.83 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 4.76 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2013, matumizi ya kawaida yalifikia shilingi bilioni 45.63 sawa na asilimia 56.45 ya makadirio na matumizi ya maendeleo yalifikia shilingi bilioni 1.22.

60

Fungu 22 - Deni la Taifa

Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya Fungu 22 kwa mwaka 2013/14 yalikuwa shilingi bilioni 3,319.01. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014 matumizi ya fungu hili yalifikia shilingi bilioni 2,795. 43 sawa na asilimia 84.22 ya makadirio.

Fungu 21- HAZINA

136. Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya kawaida ya Fungu 21 kwa mwaka 2013/14 yalikuwa shilingi bilioni 1,367.29 na matumizi ya maendeleo shilingi bilioni 38.15 . Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014, matumizi ya kawaida yalifikia shilingi bilioni 420.28 sawa na asilimia 30.74 ya makadirio, na matumizi ya maendeleo yalifikia shilingi bilioni 19.78 sawa na asilimia 51.85 ya makadirio.

Fungu 13 – Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu

137. Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya Fungu 13 kwa mwaka 2013/14 yalikuwa shilingi bilioni 1.94 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 0.39 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014, matumizi ya kawaida yalifikia shilingi bilioni 0.91 sawa na asilimia 46.90 ya makadirio, na matumizi ya maendeleo yalifikia shilingi bilioni 0.07 sawa na asilimia 17.95 ya makadirio.

61

Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha

138. Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya kawaida kwa Fungu hili yalikuwa shillingi bilioni 2.06, hadi kufikia Aprili, 2014 matumizi yalifikia shilingi bilioni 1.04 sawa na asilimia 49.76 ya makadirio.

Fungu 7 – Ofisi ya Msajili wa Hazina

139. Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya Fungu 7 kwa mwaka 2013/14 yalikuwa shilingi bilioni 38.08 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 1.66 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014, matumizi ya kawaida yalifikia shilingi bilioni 33.06 sawa na asilimia 86.8 ya makadirio, na matumizi ya maendeleo yalifikia shilingi bilioni 0.62 sawa na asilimia 37.35 ya makadirio.

Fungu 45 - Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

140. Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya Fungu 45 kwa mwaka 2013/14 yalikuwa shilingi bilioni 57.4 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 21.45 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014, matumizi ya kawaida yalifikia shilingi bilioni 43.11 sawa na asilimia 75.1 ya makadirio, na matumizi ya maendeleo yalifikia shilingi bilioni 2.97 sawa na asilimia 13.84 ya makadirio.

62

MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2014/15

Mapato

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara ya Fedha Fungu 50 inakadiria kukusanya mapato yasiyo ya kodi yapatayo shilingi 126,188,104,000 (bilioni 126.19

Maombi ya Fedha

Fungu 50 – Wizara ya Fedha.

141. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwa mwaka wa fedha 2014/15, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:

(a) Matumizi ya kawaida Shilingi 66,239,790,000 (bilioni 66.23). Kati ya hizo mishahara ni shilingi shilingi 5,620,668,000 (bilioni 5.62) na matumizi mengineyo shilingi 60,619,122,000 (bilioni 60.61).

(b) Miradi ya Maendeleo Shilingi 29,803,232,000 (bilioni 29.71).Kati ya hizo:

(i) Fedha za Ndani - Shilingi 19,350,000,000 (bilioni 19.35).

(ii) Fedha za Nje - Shilingi 10,453,232,000 (bilioni 10.45).

Fungu 23 – Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali:

63

142. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwa mwaka wa fedha 2014/15, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:

(a) Matumizi ya kawaida - Shilingi 82,170,024,000 (bilioni 82.17). Kati ya hizo mishahara shilingi 5,012,762,000 (bilioni 5.01) na matumizi mengineyo shilingi 77,157,262,000 (bilioni 77.16).

(b) Miradi ya Maendeleo – Shilingi 7,950,000,000 (bilioni 7.95) Kati ya hizo:

(i) Fedha za Ndani -Shilingi 4,800,000,000 (bilioni 4.80).

(ii) Fedha za Nje -Shilingi 3,150,000,000 (bilioni 3.15).

Fungu 22- Deni la Taifa

143. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwa mwaka wa fedha 2014/15, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha Shilingi 4,354,865,076,000 (bilioni 4,354.86). Kati ya hizo mishahara ni shilingi 10,341,136,000 (bilioni 10.34), Deni la Taifa shilingi 3,650,612,000,000 (bilioni 3,650.61) na matumizi mengineyo ni shilingi 693,911,940,000 (bilioni 693.91).

Fungu 21 - HAZINA

144. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwa mwaka wa fedha 2014/15, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:

64

(a) Matumizi ya kawaida Shilingi 790,325,216,000 (bilioni 790.32). Kati ya hizo mishahara ni shilingi 4,015,511,000 (bilioni 4.01) na matumizi mengineyo shilingi 786,309,705,000 (bilioni 786.31) ambazo ni kwa ajili ya matumizi ya Idara na Taasisi zilizo chini ya Fungu hili, nyongeza ya mishahara ya Watumishi wa Serikali na matumizi maalum.

(b) Miradi ya maendeleo ni shilingi 57,417,015,000 (bilioni 57.42). Kati ya hizo;

(i) Fedha za Ndani- Shilingi 17,000,000,000 (bilioni 17.0)

(ii) Fedha za Nje- Shilingi 40,417,015,000 (bilioni 40.42)

Fungu 13 – Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu:

145. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwa mwaka wa fedha 2014/15, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:

(a) Matumizi ya kawaida - Shilingi 2,000,000,000 (bilioni 2.0).

(b) Miradi ya Maendeleo, fedha za nje Shilingi 195,000,000 (bilioni 0.19).

Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha:

146. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwa mwaka wa fedha 2014/15, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha Shilingi 2,318,661,000 (bilioni

65

2.32) kwa matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo, shilingi 318,661,000 (bilioni 0.32) ni kwa ajili ya mishahara na shilingi 2,000,000,000 (bilioni 2.0) ni matumizi mengineyo.

Fungu 7 – Ofisi ya Msajili wa Hazina:

147. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwa mwaka wa fedha 2014/15, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:

(a) Matumizi ya kawaida - Shilingi 88,455,278,000 (bilioni 88.45). Kati ya hizo shilingi 670,328,000 (bilioni 0.67) ni kwa ajili ya mishahara na shilingi 87,784,950,000 (bilioni 87.78) ni matumizi mengineyo.

(b) Miradi ya Maendeleo – Shilingi 1,943,000,000 (bilioni 1.94) Kati ya hizo:

(i) Fedha za Ndani –Shilingi 650,000,000 (bilioni 0.65).

(ii) Fedha za Nje -Shilingi 1,293,000,000 (bilioni 1.29).

Fungu 45 - Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

148. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwa mwaka wa fedha 2013/14, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:

(a) Matumizi ya kawaida shilingi 69,843,825,000 (bilioni 69.84). Kati ya hizo mishahara ni shilingi

66

10,408,402,000 (bilioni 10.41) na matumizi mengineyo shilingi 59,435,423,000 (bilioni 59.43).

(b) Miradi ya maendeleo shilingi 13,011,432,000 (bilioni 13.01), kati ya hizo:

(i) Fedha za ndani shilingi 8,000,000,000 (bilioni 8.0).

(ii) Fedha za nje shilingi 5,011,432,000 (bilioni 5.01).

HITIMISHO

149. Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani za dhati kwa Wakuu wa Idara na Vitengo, Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha wakiongozwa na Katibu Mkuu Dkt. Servacius B. Likwelile na Naibu Makatibu Wakuu Ndugu Elizabeth J. Nyambibo, Prof. Adolf F. Mkenda na Ndugu Doroth S. Mwanyika kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kutekeleza majukumu ya Wizara. Vile vile, napenda kuwashukuru Wakuu wa Taasisi na Wakala wa Serikali chini ya Wizara kwa michango yao katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

150. Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza. Hotuba hii pia inapatikana katika tovuti ya Wizara (www.mof.go.tz)

151. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja

No comments:

Post a Comment