MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Thursday, January 4, 2018

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU ASHIRIKI WARSHA YA MASUALA YA MIFUMO YA TEHAMA


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora (kushoto) akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Miundombinu ya TEHAMA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Baltazari Kibola wakati wa warshaa kuhusu Mifumo ya TEHAMA na Takwimu inavyotegemeana Kiutendaji

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akiweka sahihi katika kitabu cha wageni katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) aliposhiriki Warsha ya Masuala ya Mifumo ya (TEHAMA)


Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  Mohamed Pawaga akizungumza jambo alipotembelewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora katika ofisi yake Mjini Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Miundombinu ya TEHAMA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Baltazari Kibola akiwasilisha mada kwenye warsha ya masuala ya Mifumo ya TEHAMA


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akitoa ufafanuzi wa masuala ya mifumo ya TEHAMA wakati wa Warsha iliyolenga juu ya Mifumo ya TEHAMA na Takwimu inavyotegemeana Kiutendaji yaliyofanyika  katika ukumbi wa mikutano wa TAMISEMI Dodoma .


Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Obey Assery akichangia hoja wakati wa warsha fupi kuhusu Mifumo ya TEHAMA na Takwimu inavyotegemeana Kiutendaji iliyoandaliwa na TAMISEMI


Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  Mohamed Pawaga akieleza umuhimu wa matumizi ya Mifumo ya TEHAMA na Takwimu kwa wajumbe wa warsha iliyoandaliwa na Ofisi hiyo Dodoma.


Baadhi ya washiriki wa Warsha wakifuatilia uwasilishaji kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Miundombinu ya TEHAMA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Baltazari Kibola wakati wa mafunzo ya masuala ya TEHAMA

Daktari Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Boniface Nguhuni akijibu hoja wakati wa Warsha ya Masuala ya Mifumo ya TEHAMA


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya masuala ya Mifumo ya TEHAMA kwa Kaimu Mkurugenzi wa masuala ya Miundombinu ya TEHAMA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Baltazari Kibola wakati wa warsha ya masuala ya Mifumo ya TEHAMA iliyofanyika Dodoma.

No comments:

Post a Comment