MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Wednesday, November 30, 2011

Songas wakabidhi vyumba viwili vya madarasa na madawati 50 kwa Shule ya msingi Kinyelezi Dar es Salaam

 Wanafunzi wa Kinyelezi wakiimba wakati wa kukabidhiwa vyumbsa viwili vys madarasa
 Wanafunzi wa Shule ya msingi Kinyelezi Dar es Salaam wakiimba baada ya kukabidhiwa vyumba viwili vya madarasa na madawati 50 na Kampuni ya Songas
 Usafiri wa haraka wa Bongo kwa kutumia Pikipiki maarufu Bodaboda
 Waandishi wa habari wapigapicha wakigombea kupiga picha Jerry Muro baada ya Mahakama kuona hana kosa katika kesi iliyokuwa inamkabili
Jerry Muro baada ya kuachiwa katika Mahakama ya Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana akiwa na Mkewe

Thursday, November 24, 2011

FAINALI UHAI CUP YASOGEZWA

Mechi ya fainali ya michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Kombe la Uhai (Uhai Cup) kwa klabu za Ligi Kuu sasa itachezwa kesho (Novemba 26 mwaka huu) saa 3.00 asubuhi kwenye Uwanja wa Karume.

Awali fainali hiyo kati ya Simba ambayo iliingia hatua hiyo kwa kuitandika Toto Africans mabao 4-1 na Azam iliyofuzu kwa kuizamisha Serengeti Boys (timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17) mabao 3-0 ilikuwa ichezwe leo (Novemba 25 mwaka huu) saa 9.00 kwenye uwanja huo.

Mabadiliko hayo yamefanyika ili kutoa nafasi kwa mashabiki kushuhudia mechi za michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza leo (Novemba 25 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa. Kila siku kwenye michuano ya Chalenji zinachezwa mechi mbili; ya kwanza saa 8.00 mchana na nyingine saa 10.00 jioni.

Michuano ya Kombe la Uhai inadhaminiwa na Kampuni ya S.S. Bakhresa kupitia maji Uhai ambapo bingwa atapata sh. milioni 1.5, mshindi wa pili sh. milioni moja wakati wa tatu atapata sh. 500,000. Mbali ya fedha hizo, bingwa atapata medali za dhahabu, makamu bingwa medali za fedha na mshindi wa tatu medali za shaba.
Mchezaji bora sh. 400,000, mfungaji bora (sh. 300,000), kipa bora (sh. 300,000) na timu yenye nidhamu sh. 300,000.

VIINGILIO MICHUANO YA KOMBE LA CHALENJI

Viingilio kwa mechi za hatua ya makundi kwa michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza leo (Novemba 25 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam vitakuwa kama ifuatavyo;

Kwa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo ni zaidi ya 30,000 kiingilio kitakuwa sh. 1,000 wakati viti vya rangi ya chungwa ambavyo ni zaidi ya 10,000 kiingilio kitakuwa sh. 3,000. VIP C na B ambayo jumla ya viti vyake ni 8,000 kiingilio kitakuwa sh. 5,000 wakati VIP A yenye viti 700 kiingilio ni sh. 10,000

TENGA ACHAGULIWA TENA CECAFA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Tenga amechaguliwa leo (Novemba 24 mwaka huu) bila kupingwa baada ya mpinzani wake Fadoul Hussein wa Djibouti kutotokea kwenye uchaguzi.

Kutokana na hali hiyo, mjumbe kutoka Uganda alitoa hoja ya Tenga kupitishwa bila kupingwa, hoja ambayo iliungwa mkono na Kenya, Tanzania, Uganda, Sudan, Zanzibar, Ethiopia, Burundi na Eritrea.

Jumla ya nchi wanachama zilizopiga kura katika uchaguzi uliofanyika hoteli ya New Africa ni kumi na moja, na kila moja ilikuwa na kura moja tu.

Kwa upande wa nafasi nne za wajumbe wa Kamati ya Utendaji kulikuwa na wagombea wanane. Waliopita katika raundi ya kwanza na kura zao kwenye mabano ni Abdiqani Saeed Arab wa Somalia (8), Tariq Atta Salih wa Sudan (8) na Raoul Gisanura wa Rwanda (8).

Wengine katika raundi ya kwanza na kura walizopata kwenye mabano ni Sahilu Wolde wa Ethiopia (4), Justus Mugisha wa Uganda (4), Tesfaye Gebreyesus wa Eritrea (4), Hafidh Ali Tahir wa Zanzibar (2) na
Abubakar Nkejimana wa Burundi (3).
Mjumbe aliyefanikiwa kushinda katika raundi ya pili na kuingia kwenye Kamati ya Utendaji ni Wolde wa Ethiopia aliyepata kura tano dhidi ya nne za Mugisha na mbili za Gebreyesus.

ZIMBABWE YAZIBA NAFASI YA NAMIBIA
Timu ya Taifa ya Zimbabwe (Might Warriors) imeteuliwa na CECAFA kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza Novemba 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam kuziba nafasi ya Namibia iliyojitoa.

Zimbabwe itawasili Novemba 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam na itakuwa kundi A pamoja na timu za Tanzania Bara, Rwanda na Djibouti.

KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS

Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Charles Boniface Mkwasa ametaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 20 kwa ajili ya michuano hiyo inayoanza kesho.



Wachezaji waliobaki kati ya 28 waliokuwa wameitwa awali ni Juma Kaseja (Simba), Shabani Kado (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Godfrey Taita (Yanga), Juma Jabu (Simba), Ibrahim Mwaipopo (Azam) na Juma Nyoso (Simba), Said Murad (Azam), Erasto Nyoni (Azam) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Nurdin Bakari (Yanga), Haruna Moshi (Simba) na Mwinyi Kazimoto (Simba).

Wengine ni Said Maulid (Angola), Musa Mgosi (DC Motema Pembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC), Mrisho Ngassa (Azam), Ramadhan Chombo (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Rashid Yusuf (Coastal Union).

Watanzania wawili kucheza ligi daraja la pili Sweden

Wachezaji wawili wa kitanzania, Joseph Kaniki (Golota) na William John wamefanikiwa kujiunga na timu ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF) nchini Sweden, baada ya kufanikiwa kupita katika majaribio( Trials). Majaribio hayo yalijumuisha wachezaji zaidi ya thelathini ambapo wachezaji watano walichaguliwa kujiunga na klabu hiyo ya ligi daraja la pili KonyaSpor

Asante kotoko in Dar

TIMU ya soka ya Kumasi Asante kotoko ya Ghana inatarajiwa kuwasili nchini Desemba 9 tayari kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya kombaini ya timu za Yanga na Simba siku ya Desemba 11 kwenye uwanja wa Taifa.
Mchezo huo ni sehemu ya kukamilisha maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Future Century Limited, Helen Masanja.
Masanja alisema kuwa timu hiyo itafikia Zanzibar na baadaye kuja jijini Dar es Salaam kwenye hotel ya Lamada tayari kwa mchezo huo ambao umedhaminiwa na PPF, Kenya Airways, Vanedrick Tanzania Limited, Lamada Hotel na Vanne Fashion Tabata.
Alisema kuwa wanatarajia kuwa na burudani ya aina yake kwani tayari kombaini ya timu ya Yanga na Simba itaundwa na wachezaji nyota wanaocheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu.
Aliongeza kuwa   makocha wawili, mkongwe, Abdallah “King  Mputa” Kibaden na Fred “ Minziro” Felix ndiyo watakuwa wakuu wa benchi la ufundi la timu hiyo ambayo itaundwa na wachezaji 20 watakaotangazwa hapo baadaye. Wengine katika benchi la ufundi na meneja, Boniface Pawasa na daktari wa timu, Juma Sufiani.
Alifafanua kuwa uteuzi wa timu hiyo hautajali uraia wa wachezaji hivyo kama wachezaji kutoka nchi za nje ambao wanachezea timu hizo watateuliwa, basi watacheza mchezo huo.
Masanja alisema kuwa Yanga na Simba zimekubaliana na kuweka historia kwa mara ya kwanza tangu timu hizo zitengane mwaka 1935. Alisema kuwa historia inaonyesha kuwa timu hizo zilikuwa pamoja kuanzia mwa 1922.
Mwenyekiti wa Yanga Lyod Nchunga alisema kuwa mechi hiyo itaondoa tofauti iliyopo baina ya mashabiki wa Simba na wale wa Yanga hasa zinapotokea timu hizo zinacheza mechi za kimataifa ambapo imekuwa ni kawaida mashabiki wa timu hizo kushangilia timu pinzania.
Wakati Nchunga akisema hayo, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema kuwa muungano huo utaleta tija kwa timu hizo ambapo mashabiki wa Simba na Yanga siku hiyo watakuwa kitu kimoja kwa ajili ya kuishangilia timu yao tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Alisema kuwa huu ndiyo mwanzo wa kuanza kushirikiana katika mechi za kimataifa na kuwataka mashabiki kufika kwa wingi na kutoa sapoti kubwa kwao.

Wednesday, November 23, 2011

kikao cha Nec CCM

Baadhi ya wajumbe wa Nec CCM wakiwa katika Kikao hicho cha siku mbili kilichoanza mjini Dodoma jana

Monday, November 21, 2011

Tamasha

Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA),Joseph Mbilinyi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu shoo ijulikanyo Anti Virus wakati Itakayotumbuizwa katika Tamasha litalaofanyika  Nov. 26 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi,(kushoto) ni Msanii  Fred Malaki (a,k,a- MKOLONI) n a Mwanadada Zainab Lipangile a.k.a  ZAY –B, Katika tamasha hilo Wasanii mbalimbali watatumbuiza.

Wednesday, November 16, 2011

Michuano ya Cecafa

NAMIBIA YAINGIA MICHUANO YA CHALENJI

Namibia itashiriki michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza Novemba 25 mwaka huu ikiwa timu mwalikwa baada ya Eritrea kujitoa. Hivyo Namibia inaingia moja kwa moja katika kundi A ambalo lina mabingwa watetezi Tanzania Bara, Rwanda na Djibouti.

Pia ratiba ya mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia ya Tusker imetangazwa rasmi leo (Novemba 16 mwaka huu) ambapo mechi zote zitachezwa Dar es Salaam baada ya Mkoa wa Mwanza kushindwa kutimiza masharti iliyopewa ili nayo iwe kituo cha michuano hiyo.

Mechi mbili zitachezwa kwa siku Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam isipokuwa Novemba 26 mwaka huu ambapo kutafanyika uzinduzi rasmi saa 10 jioni kwa mechi kati ya Tanzania Bara na Rwanda.

Novemba 25 mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Burundi na Somalia (saa 8 mchana) na Uganda na Zanzibar itakayoanza saa 10 jioni. (Ratiba yote ya mashindano imeambatanishwa)

MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI
Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro), Charles Boniface Mkwasa kesho (Novemba 17 mwaka huu) saa 6 mchana atakuwa na mkutano na waandishi wa habari.

Mkutano huo utafanyika ofisi za TFF ambapo pamoja na mambo mengine atatangaza kikosi kitakachotetea Kombe la Chalenji.

Sunday, November 13, 2011

VURUGU ZA MBEYABAADA YA KUPIGWA BOMU LA MACHOZI WAGONJWA WAKIMBIA, MADAKTARI WAWILI NA WAUGUZI WATANO WAZIRAI


Vitanda vilivyokuwa vikitumiwa na wangonjwa katika Zahanati ya Ipinda, iliyopo Mwanjelwa jijini Mbeya vikiwa wazi baada ya wagonjwa kukimbia mara baada ya bomu la machozi lililopingwa na Jeshi la polisi kutua ndani ya Wadi.





 Mgonjwa aliyekuwa akitibiwa Zahanati hapo akiwa amezirai baada ya bomu la machozi lililopingwa na Jeshi la polisi kutua ndani ya Wadi.







Mganga Mkuu wa zahanati ya Ipinda jijini Mbeya Dk. Lute Kibopile ambaye pia ni mmiliki wa zahanati hiyo akionesha Bomu la machozi lililopigwa na Jeshi la polisi na kuingia ndani ya Wadi

 Mganga Mkuu wa zahanati ya Ipinda jijini Mbeya Dk. Lute Kibopile ambaye pia ni mmiliki wa zahanati hiyo akielezea jinsi bomu la machozi lilivyopingwa



Muuguzi akionesha eneo ambalo bomu la machozi lilipotua katika Zahanati ya Ipinda, eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya

Mtaalamu wa masuala ya maabara katika Hospitali ya UHAI BAPTIST Dk Ngangele Lisukile akiwa ameshika kigae kilichodondoka mara baada ya bomu la machozi lililopingwa hospitalini hapo majira ya saa 5:30 asubuhi.  PICHA ZOTE NA: www.mbeyayetu.blogspot.com

Friday, November 11, 2011

machinga na FFU wapambana na jijini Mbeya


Wamachinga wakiwa tayali kwa ajili ya Kupambana na FFU wakati wa tukio hilo


Wamachinga Mbali mbali wakikimbia katika eneo la tukio wakati wa machafuko hayo yamepamba moto





Watu Mbali Mbali wakiwa wanakimbia ili kujiokoa na Hatari katika eneo hilo picha zote kwa niaba ya Latest news

Jk akizugumza na wanahabari baada ya kufungua Mkutano wa kazi

Rais Dkt Jakaya Kikwete akiwafafanulia wanahabari kuhusiana na Mkutano wa Kazi (Business Meeting) uliojadili Mpango wa Uwekezaji Katika Sekta ya Kilimo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta hiyo wakiwemo mabalozi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa, mawaziri na viongozi serikalini pamoja na wadau wa sekta ya umma. Mkutano huu wa siku mbili umefanyika Ubungo Plaza jijini Dar

Thursday, November 10, 2011

Bunge laendelea mjini Dodoma

Wabunge wakihudhuria Kikao cha Bunge mjini Dodoma

Pinda akutana na viongozi wa Songas Dodoma

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa na viongozi wa Songas alipokutana nao Dodoma

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA UWEKEZAJI WA KILIMO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa Mkutano wa Uwekezaji wa Chakula na Kilimo, ulioanza leo Novemba 10, 2011 kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.
Makau wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa Uwekezaji wa Chakula na kilimo, baada ya kuongoza mkutano huo leo Novemba 10, katika ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

MALEMA ATEMWA ANC

Chama tawala nchini Afrika Kusini, ANC kimefukuza kiongozi wa vijana Julius Malema kutoka cheo chake kwa muda wa miaka mitano.

Hii ni baada ya kamati ya nidhamu kumpata na hatia ya kuvunjia chama heshima.

Julius Malema ambaye hakuwepo kwenye makao makuu ya chama chake wakati hukumu hiyo ilipotolewa, amepewa siku 14 kukata rufaa ya uamuzi huo.

Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu Derek Hanekom, amesema kuwa tabia ya Malema imeishushia hadhi chama cha ANC na sio njia muafaka ya kuelezea hisia za kutoridhika na sera za chama.

Kamati hiyo imempata na hatia ya kuvuruga mkutano wa ANC, kukivunjia hadhi chama hicho kwa kudai mageuzi ya utawala nchini Botswana na kuchochea migawanyiko chamani.

Viongozi wengine wa umoja wa vijana, miongoni mwao msemaji Floyd Shivambu, pia wamefukuza kutoka kwa nyadhifa zao kwa muda wa miaka mitatu.

"Tabia ya Malema itaharibu uhusiano wa kimataifa wa chama chetu na kuvunjia heshima Afrika Kusini kwa jumla na sio vyema kuwa ivumiliwe" alisema Bw Hanekom.

Hata hivyo kamati hiyo haikumpata Malema na hatia kwenye kosa la kuchochea ubaguzi wa rangi.

Wadadisi wa siasa nchini Afrika Kusini wanasema uamuzi huu unaweza kuwa ushindi kwa Rais Jacob Zuma ambaye anakabiliwa na upinzani kutoka kundi linalopendelea sera za kutaifisha uchumi wa nchi hiyo, ikiwemo kunyakuwa ardhi za wazungu.

Malema anaushawishi mkubwa miongoni mwa vijana na watu masikini na wadadisi wanasema ikiwa hata kata rufaa huenda harakati zake zikawa changamoto kubwa kwa chama cha ANC.

SHEHENA YA BANGI MAHAKAMANI

Askari kanzu akifungua moja ya viroba vyenye bangi katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa morogoro kwa ajili ya vielelezo baada ya jeshi la polisi mkoa huo kukamata bangi hiyo eneo la Mindu ikisafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam ambakom kuna soko zuri la biahsra hiyo haramu mkoani hapa.

UTURUKI YAPIGWA NA TETEMEKO JINGINE

Waokoaji wakitafuta walionusurika katika jengo la hoteli mashariki mwa Uturuki jumatano.

Uturuki yakumbwa na tetemeko jingine la ukubwa wa 5.7 vipimo vya rikta.

Tetemeko la 5.7 kwenye vipimo vya rikta lilikumba eneo la mashariki mwa Uturuki Jumatano usiku na kuuwa watu wapatao watatu na kupromosha majengo yapatayo 20.

Dazeni ya watu inaaminika wamenaswa katika vifusi katika eneo la Van karibu na mpaka wa Iran.Watu wapatao 10 walionusurika wamefukuliwa chini ya majengo yalioanguka mpaka sasa.

Tetemeko hilo limetokea chini ya wiki 3 baada ya tetemeko linguine la ardhi kukumba Uturuki katika eneo hilo kuuwa watu wapatao 600 na maelfu kadhaa kupoteza makazi yao.

Wednesday, November 9, 2011

RAIS KIKWETE

Rais Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Joseph Pyne. mzungu aliyeshika namba 3 katika shindano la wasanii wa muziki la Bongostar Search 2010 wakati walipokutana katika Ziara ya Prince Charles Mtoto wa Malkia wa Uingereza Queen Elizaberth II , Prince Charles alikuwa nchini kwa ziara ya Kiserikali ya siku nne ambayo ilimalizika jana.

HAFLA YA KUMUAGA BALOZI WA ULAYA

Spika wa Bunge akimpa Balozi Clarke zawadi ya saa ya ukutani yenye jengo la Bunge la Tanzania.
Balozi Clarke(kulia) pia alikutana na kujadili masuala kadhaa na Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (katikati). Kushoto ni mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Khalifa Khalifa.
Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Mussa Zungu Azzan, Bolozi wa Umoja wa Ulaya Tim Clarke, Mwenyekiti wa Kamati Mhe Edward Lowassa na Mjumbe wa Kamati Mhe. Khalifa S. Khalifa. Picha na Prosper Minja-Bunge

MHESHIMIWA MBOWE ALIPOAMUA KUJIPELEKA POLISI KWA HIYARI YAKE

Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe akiingia katika ofisi za mkoa za Jeshi la Polisi mkoni Arusha leo,aliyevaa nguo nyeusi ni Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema,Joyce Mukya akiwa amemsindikiza mwenyekiti wao kujisalimisha Polisi.
Mkuu wa Operation wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha,Saimon Pilo (kulia) akiwa amempokea Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe (katikati) katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kufanya nae Mazungumzo,wakati Mwenyekiti huyo alipofika Kituoni hapo Kujisalimisha leo asubuhi.

Sunday, November 6, 2011

RAIS KIKWETE ATEMBELEA KITENGO CHA FIGO HOSPITALI YA MUHIMBILI

Rais Jakaya Kikwete akimsalimu na kumpa pole mtoto Ali Abdul (13) kutoka Rufiji, mkoa wa Pwani, aliyetoka kufanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya damu iliyozibwa na madaktari bingwa toka India amabo wako nchini kusaidia kazi katika kitengo cha tiba ya figo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam. Kitengo hicho kimeundwa mahususi kusaidia watu wa matabaka yote kupat matibabu ya figo ikiwa ni moja ya jitihada za serikali kusaidia wananchi wake kupata matibabu hayo hapa hapa nchini na kwa gharama nafuu. Rais Kikwete ameonesha kufurahishwa na kuridhishwa na maendeleo ya kitengo hicho ambacho muda si mrefu ujao kitakuwa na uwezo wa kutibu wagonjwa wengi zaidi
Rais Jakaya Kikwete akiongea na madaktari bingwa hao toka India
Rais Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na madaktari bingwa toka India na wa Tanzania aliowatembelea katika kitengo cha tiba ya figo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam

UGIRIKI KUUNDA SERIKALI YA MSETO

Viongozi wa Ugiriki wameafikiana kuunda serikali mpya ya muungano wa kitaifa, ofisi ya rais imesema.
Makubaliano hayo yaliafikiwa katika mazungumzo yaliyoongozwa na rais Karolos Papoulias mjini Athens, kati ya Waziri Mkuu, George Papandreou na kiongozi wa upinzani, Antonis Samaras.
Waziri Mkuu George Papandreou amekubali kujiuzulu na atakaye mrithi atachaguliwa katika mazungumzo yatakayofanyika Jumatatu, taarifa kutoka kwa ofisi ya rais ilisema.
Serikali hiyo mpya ya muungano ndiyo itakayoongoza nchi hadi uchaguzi mkuu ujao, ambao huenda ukafanyika 19 Februari, wizara ya fedha ilisema.
Tangazo la kuundwa kwa serikali mpya linajiri baada ya wiki moja ya mgogoro kuhusu madeni ya Ugiriki.

masharti ya EU

Muungano wa Ulaya umesema kuwa hautatoa mkopo zaidi kwa Ugiriki hadi pale mpango wake mpya wa kupunguzia nchi hiyo madeni utakapokubaliwa.
Kumekuwa na shinikizo kali kutoka kwa jamii ya kimataifa kwa Ugiriki kutatua mzozo wake wa kisiasa ili kuzuia kuyumbisha masoko katika muungano huo.
Punde kiongozi mpya atakapotaganzwa, rais Papoulius atazialika vyama vya kisiasa kujiunga na serikali hiyo.
Bwana Papandreou amekuwa akijaribu kuunda serikali ya muungano kurithi inayoongozwa na chama chake cha Pasok, lakini kiongozi wa upinzani Bwana Samaras wa chama cha New Democratic Party alikataa kushauriana naye hadi pale angejiuzulu.

SIDI MGUMIA AKIWA IRAN

Mdau Sidi Mgumia akiwa na mshiriki mwenzake wa maonyesho kutoka Romania wakiwa nje ya jengo ambalo ndani yake kunapatikana aina mbalimbali za makapeti ambazo zimetengenezwa kwa umahiri wa hali ya juu, za kipeeke na ni moja ya vivutio vikubwa vya watalii pia ni kati ya utaalam ambao raia wa Iran wanajivunia sana.
Watu hivyo wengi walipenda awasainie vitabu vyao ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu alizowaachia wana Iran!!

MAKAMU WA RAIS KATIKA BALAZA LA EID El-HAJ

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa dini ya Kiislam kuomba dua baada ya swala ya Idd El Haj, iliyofanyika katika Msikiti wa aL Farouk Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akimpokea Rais Mstaafu wa Comoro, Mohammad Abdallah Sambi, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Msikiti wa Al Farouk, Kinondo ni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6, kushiriki katika swala ya Idd El Haj iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba na Baraza la Idd. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya Baraza la Eid El-Haj, baada ya swala ya Idd iliyofanyikaKitaifa kwenye Msikiti wa Al farouq Kinondoni jijiji Dar es Salaam leo Novemba 6. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

UJUMBE WA IDD AL HAJJ KWA WATU WOTE

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu
Hamdu zote ni za Mola Mlezi wa viumbe pia. Na rehema Zake Allah na salamu Zake zimshukie Bwana wa wanaadamu wote, Muhammad al Mustafa, na Aali zake wema na Masahaba wake wateule.
Hivi sasa msimu wa machipuo wa Hija uliojaa usafi, uraufu na unyofu wa kimaanawi pamoja na utukufu na heshima kutoka kwa Mwenyezi Mungu umewadia, huku nyoyo za waumini wenye shauku kubwa zikizunguka Alkaaba ya tawhidi na umoja mithili ya vipepeo. Makkah na Mina na Mash'ar na Arafa ni nyumbani kwa watu wenye bahati njema ambao wameitika mwito na mlingano wa Mwenyezi Mungu wa وَأَذِّن فِي النَّاسِ بِالْحَجِّ Na walinganie watu Hija... na wamepata fakhari ya kuingia kwenye ugeni wa Mwenyezi Mungu Mwingi wa maghufira, Mwingi wa ukarimu. Hapa ni katika ile Nyumba iliyobarikiwa (na Mwenyezi Mungu) na ni katika kitovu cha uongofu ambacho "Aya bainifu za Mwenyezi Mungu" zinang'ara ndani yake na kuwafunika kivuli cha amani watu wote walioko kwenye eneo hilo tukufu.
Zisafisheni nyoyo zenu kwa zamzamu ya unyofu, dhikri na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na macho ya ndani ya nafsi zenu yafungueni kwa ajili ya kuona Aya zilizo wazi za Mola wa Haki. Jipambeni kwa sifa za ikhlasi na kujisalimisha kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu, jambo ambalo ni ishara ya uja na unyenyekevu wa kweli. Zifufueni na ziwekeni hai katika nyoyo zenu mara kwa mara, kumbukumbu za Yule baba (Nabii Ibrahim AS) ambaye kutokana na ikhlasi, unyenyekevu na kujisalimisha kwake kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu, alimchukua Ismail wake na kumpeleka kwenye madhabahu (kwa ajili ya kumtoa kafara katika njia ya Mwenyezi Mungu). Ni kwa namna hiyo ndipo tutaweza kuijua njia ya wazi na inayong'aa ya kuweza kutufikisha kwa Mola Mlezi wetu, Mwingi wa utukufu. Piteni katika njia hiyo kwa hima ya imani thabiti na nia ya kweli-kweli.
Makamu ya Ibrahim ni moja ya ishara hizo bainifu za Mwenyezi Mungu. Mahali ulipo mguu wa Ibrahim AS pembeni mwa Alkaaba Tukufu ndiyo alama na nembo pekee ya Ibrahim. Mahala hapo alipokuwa akisimama (Nabii) Ibrahim (AS) ni mahala pa ikhlasi, kusamehe kila kitu na kujitolea kwake kikamilifu katika njia ya Mwenyezi Mungu, hapo palikuwa ni mahala kwa kuonyesha msimamo wake usiotetereka mbele ya matamanio ya nafsi na mapenzi ya baba kwa mwanawe na pia mbele ya nguvu za kufru na shirki na ubeberu wa Namrud wa zama zake.
Leo hii pia, mambo yote haya mawili yanamfungulia njia ya uongofu kila mmoja wetu katika umma wa Kiislamu. Hima, ushujaa na nia isiyotetereka ya kila mmoja wetu inaweza kutuongoza kwenye malengo yale yale ambayo Mitume wote wa Mwenyezi Mungu kuanzia Adam hadi Mtume wa Mwisho waliwalingania watu na kufanikiwa kuwaongoa baadhi yao kwenye saada na ufanisi wa duniani na Akhera.
Hii ni fursa nzuri na adhimu kwa umma wa Kiislamu na ni vyema kwa mahujaji kuzingatia masuala muhimu yanayohusiana na ulimwengu wa Kiislamu. Juu ya masuala yote hayo muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu, kuna hii harakati ya mapinduzi katika baadhi ya nchi muhimu za Kiislamu. Baina ya msimu wa Hija wa mwaka jana na msimu wa Hija wa mwaka huu kuna matukio yametokea katika ulimwengu wa Kiislamu ambayo yanaweza kubadilisha kikamilifu mustakbali wa umma wa Kiislamu na yametoa bishara njema ya kupatikana mustakbali bora uliojaa heshima na mendeleo ya kimaada ya kimaanawi kwa Waislamu. Huko Misri, Tunisia na Libya, mataghuti, madikteta na watawala vibaraka na waharibifu wameng'olewa kwenye viti vya utawala, na katika baadhi ya nchi nyingine pia mawimbi makubwa ya mapambano ya wanachi yanatishia kuangamiza majengo ya kifakhari ya tawala za kitaghuti na kidikteta.
Ukurasa huu mpya uliofunguka katika historia ya umma wetu unabainisha uhakika ambao kila kipengee chake ni ishara bainifu za Mwenyezi Mungu ambazo zinatupa masomo na mazingatio makubwa katika maisha yetu. Uhakika huo inabidi utumike katika mahesabu yote ya mataifa ya Kiislamu.
Mosi ni kwamba hivi sasa katika kitovu cha mataifa ambayo kwa makumi ya miaka yalikuwa chini ya udhibiti wa kisiasa wa mabeberu wa kigeni kumezuka kizazi cha vijana ambao kwa kujipamba na sifa ya kupigiwa mfano ya kujiamini wamekubali kuingia kwenye hatari na kukabiliana na madola ya kibeberu na kutia hima ya kuleta mapinduzi na kubadilisha hali iliyopo.
Jengine ni kwamba licha ya watawala za kisekula kudhibiti kila kitu na kupambana na mafundisho ya dini kwa siri na kwa dhahiri katika nchi hizo, lakini wananchi wamejitokeza kwa wingi mno katika medani ya mapambano wakaziongoza vizuri nyoyo na ndimi zao; na mithili ya chemchemu zinazofoka, mamilioni ya watu wakaingia katika medani hiyo kwa maneno na matendo na kuipa uhai na utukufu mikusanyiko yao na matendo yao. Minara ya adhana, maeneo ya kusalia, takbiri, nara na kaulimbiu za Kiislamu; yote hayo ni ushahidi wa wazi wa uhakika huo, na kwamba uchaguzi wa hivi karibuni nchini Tunisia nao ni uthibitisho usio na chembe ya shaka wa ukweli wa jambo hilo. Ni kitu kisicho na shaka kwamba uchaguzi huru katika nchi yoyote nyingine ya Kiislamu hautakuwa na matokeo mengine ghairi ya kama yale yaliyotokea Tunisia (ya ushindi wa Waislamu katika uchaguzi huo).
Jengine ni kuwa, katika matukio ya mwaka huu mmoja uliopita, imewathibitikia watu wote kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mwenye nguvu ametia nguvu katika azma na nia ya kweli ya mataifa ya wanaadamu kiasi kwamba, hakuna nguvu yoyote nyingine inayoweza kushinda nguvu hiyo ya wananchi. Wananchi wa taifa lolote lile wanaweza kubadilisha mustakbali wao kwa kutumia nguvu hiyo waliyopewa na Mwenyezi Mungu.
Jengine ni kwamba madola ya kibeberu yakiongozwa na Marekani, ambayo katika kipindi chote hiki cha makumi ya miaka wamekuwa wakizidhibiti mataifa ya Kiislamu kwa hila na mbinu mbali mbali kama za kisiasa na kiusalama, na kwa fikra zao, walidhani kuwa wamejifungulia jia kubwa lisilo na mpinzani yeyote kwa ajili ya kulidhibiti wanavyopenda eneo hili nyeti kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa, lakini hivi sasa madola hayo ya kibeberu yamekumbwa na mawimbi ya kwanza kabisa ya hasira na chuki za wananchi wa eneo hili. Inabidi kuwa na uhakika kwamba tawala zitakazoingia madarakani baada ya mapinduzi yanayoshuhudiwa katika mataifa ya Kiislamu, kamwe hazitakubaliana na milingano hiyo ya unyonyaji na ukandamizaji na kwamba jiografia ya kisiasa ya eneo hili itabadilishwa na wananchi kwa ajili ya kulinda heshima na uhuru wa mataifa ya eneo hili.
Jengine ni kuwa, tabia bandia na ya kinafiki ya madola ya Magharibi imezidi kufichuka mbele ya watu wa nchi za dunia. Nchi za Marekani na za Ulaya zilifanya juhudi zao zote kujaribu kuwalinda vibaraka wao katika nchi za Misri, Tunisia na Libya, lakini zilipoona haziwezi kupambana na maamuzi na nia thabiti ya wananchi, zilianza kuwachekea kinafiki wananchi wa nchi hizo na kujifanya ni marafiki wao.
Uhakika na ishara bainifu za Mwenyezi Mungu katika matukio ya mwaka mmoja uliopita katika eneo hili ni zaidi ya hayo ni si jambo zito kwa watu wenye mazingatio kuuona na kuutambua uhakika huo.
Lakini pamoja na hayo yote, leo hii umma mzima wa Kiislamu na hasa mataifa yaliyomo kwenye harakati za Mapinduzi, yanapaswa kuwa na mambo mawili makuu:
Mosi: Kuendelea na istikama na kusimama sawa sawa na kujiepusha vilivyo na kulegea azma na nia ya kweli iliyopo. Amri ya Mwenyezi Mungu iliyokuja katika Qur'ani Tukufu kwa Mtume Wake SAW ni kwamba:
فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ yaani: "Basi, simama sawa sawa kama ulivyoamrishwa, wewe na wale wanaoelekea kwa Mwenyezi Mungu pamoja nawe." Pia Mwenyezi Mungu anasema: فَلِذَلِكَ فَادْعُ وَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ yaani: "Basi kwa haya waite! Nawe simama sawa sawa kama ulivyoamrishwa..."  Na vile vile kupitia kwa Nabii Musa AS Qur'ani Tukufu inasema:

قَالَ مُوسَى لِقَوْمِهِ اسْتَعِينُوا بِاللَّهِ وَاصْبِرُواْ إِنَّ الأَرْضَ لِلَّهِ يُورِثُهَا مَن يَشَاء مِنْ عِبَادِهِ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ

Yaani: "Musa akawaambia watu wake: Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu, na subirini. Hakika ardhi ni ya Mwenyezi Mungu. Naye humrithisha amtakaye katika waja Wake. Na mwisho (mwema) ni wa wacha Mungu."
Dhihirisho kubwa la Taqwa hivi sasa kwa ajili ya mataifa yaliyosimama kwenye harakati ya mapinduzi ni kwamba wasisite wala kurudi nyuma katika harakati yao hiyo iliyojaa baraka na wala wasipumbazike na mafanikio waliyoyapata hadi sasa. Hii ni sehemu na hatua muhimu sana ya taqwa ambapo walio na taqwa hiyo huingia katika orodha ya wale watu ambao Mwenyezi Mungu amesema: "Na mwisho (mwema) ni wa wacha Mungu."
Pili: Ni kuwa macho na makini sana mbele ya hila za mabeberu wa kimataifa na madola ambayo yamepata pigo kutokana na harakati hizo za kimapinduzi. Mabeberu hawatakaa kimya, bali watatumia uwezo wao wote wa kisiasa, kiusalama na kifedha kupigania kurejesha ushawishi na nguvu zao katika nchi hizo. Silaha zinazotumiwa na mabeberu hao ni kutia tamaa, kutoa vitisho na kufanya hila na udanganyifu. Uzoefu mbali mbali unaonesha kuwa, wako baadhi ya shakhsia na watu muhimu katika jamii ambao hutekwa na silaha hizo na kuwafanya wamtumikie adui kwa kujua na kutojua kutokana na woga, tamaa na kughafilika. Jicho lililo macho la vijana, wasomi na maulamaa wa kidini linapaswa liwe makini mno katika suala hilo.
Hatari kubwa zaidi iliyopo ni uingiliaji na ushawishi wa kambi ya kufru na ubeberu katika mfumo mpya wa kisiasa wa nchi hizo. Maadui watafanya juhudi zao zote kujaribu kuzuia mifumo itakayokuja madarakani katika nchi hizo isiwe na sura ya Kiislamu na ya wananchi. Watu wote wenye uchungu na nchi hizo na wale wote wanaopigania heshima, utukufu na maendeleo ya nchi zao wanapaswa kufanya juhudi zao zote kuhakikisha kuwa mifumo mipya ya utawala itakayoingia madarakani katika nchi hizo inakuwa na sura ya Uislamu na ya wananchi. Katiba ina nafasi muhimu mno katika suala hilo. Kuweko umoja wa kitaifa, kutambuliwa rasmi makundi mengine ya kidini, kikabila na ya vizazi vingine ndilo litakalokuwa sharti la kupatikana ushindi mbali mbali katika siku za usoni.
Wananchi mashujaa na waliosimama imara na kufanya mapinduzi katika nchi za Misri, Tunisia, Libya na mataifa mengine yaliyoamka ya wananchi majasiri yanapaswa kujua kuwa njia pekee ya kuweza kuokoka na dhulma na kedi za Marekani na mabeberu wengine wa Magharibi ni kuimarisha nguvu zao na kuleta mlingano mzuri wa nguvu duniani kwa manufaa yao. Kama Waislamu wanataka kutatua masuala yao kwa njia bora mbele ya madola ya kibeberu ulimwenguni, basi wanapaswa kuifikia mipaka ya nadola makubwa duniani na hilo haliwezekani bila ya kuwepo ushirikiano, mapenzi, umoja na mshikamano kati ya nchi za Kiislamu. Na huo ndio wasia usiosahaulika aliotuachia Imam Khomeini (quddisa sirruh). Marekani na NATO kwa kisingizio cha kupambana na Gaddafi dikteta wamewashambulia kinyama wananchi wa Libya kwa miezi kadhaa. Gaddafi ni yule yule mtu ambaye kabla ya wananchi mashujaa wa Libya kusimama dhidi yake alikuwa rafiki wa karibu wa mabeberu na walikuwa wakimkumbatia na walikuwa wakipora utajiri wa Libya kupitia kwake kama ambavyo walikuwa wakimbusu mkono wake na wakisalimiana naye kwa shauku kubwa ili wapate kupora zaidi utajiri wa Libya, na baada ya wananchi kusimama dhidi yake, mabeberu hao hao wakamfanya Gaddafi kisingizio cha kuangamiza kikamilifu miundombinu yote ya Libya. Nchi gani duniani iliweza kuizuia NATO isifanye maafa na kuuawa watu kwa umati huko Libya? Kwa kweli kama meno na makucha ya madola makubwa hayatakatwa, basi hatari kama hizo zitaendelea kuzikabili nchi za Kiislamu na haiwezekani kujikomboa na uadui huo ila kwa kuundwa kambi yenye nguvu ya ulimwengu wa Kiislamu.
Leo hii Magharibi, Marekani na Uzayuni ni dhaifu zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Matatizo yao makubwa ya kiuchumi, kufeli kwao mtawalia huko Afghanistan na Iraq, upinzani mkubwa wa wananchi huko Marekani na katika nchi nyingine za Magharibi, upinzani ambao unaongezeka siku baada ya siku, mapambano na kuwa tayari wananchi wa Palestina na Lebanon kujitolea muhanga katika njia ya haki, mapambano ya kishujaa ya wananchi wa Yemen na Bahrain na katika nchi nyingine duniani zilizoko chini ya ushawishi na ubeberu wa Marekani, yote hayo yanabeba bishara kubwa nzuri kwa umma wa Kiislamu hususan nchi mpya za kimapinduzi. Wanaume na wanawake waumini katika kila kona ya ulimwengu wa Kiislamu na hasa hasa Misri, Tunisia na Libya wanapaswa kutumia kwa njia bora kabisa fursa hii iliyojitokeza ili kuunda kambi ya kimataifa ya Kiislamu yenye nguvu. Shakhsia muhimu na viongozi wa harakati za kimapinduzi wa nchi hizo wanapaswa kutawakali kwa Mwenyezi Mungu Mkubwa na kuwa na imani na ahadi ya nusra kutoka kwa Mwenyezi Mungu na wanapaswa kuupambe ukurasa mpya uliofunguka katika historia ya umma wa Kiislamu kwa fakhari zitakazokumbukwa milele na ambazo zitakuwa ni chemchemu ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kuandaa uwanja wa kushuhudiwa nusura Yake.

Wassalaamu Alaa Ibadillahis Swalihin,
Sayyid Ali Husaini Khamenei,
5/Aban/1390
29 Mfunguo Pili Dhilqaad 1432.

HAROUB AONDOLEWA TAIFA STARS

HAROUB AONDOLEWA TAIFA STARS
Beki wa kati wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Nadir Haroub ameondolewa katika kikosi hicho kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 mwaka huu jijini N’Djamena.
 
Haroub ameondolewa baada ya kuumia kifundo cha mguu wa kulia (right ankle) akiwa mazoezini jana asubuhi (Novemba 5 mwaka huu).
 
Kwa mujibu wa daktari wa Stars, Dk. Juma Mwankemwa, mchezaji huyo hakuvunjika isipokuwa amepata mshtuko mkubwa wa kifundo hicho ambapo itamchukua wiki mbili kupona sawa sawa.
 
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen amesema kutokana na hali hiyo Haroub hatakuwemo kwenye kikosi hicho kwa ajili ya mechi hiyo na ile ya marudiano ambayo itachezwa Novemba 15 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Poulsen amesema kwa muda uliobaki hataita mchezaji mwingine kwa ajili ya kuziba pengo la Haroub, hivyo kwa sasa atabaki na kikosi cha wachezaji 21 alionao kambini hoteli ya New Africa.
 
LESENI ZA UKOCHA ZA CAF DARAJA C
Kozi ya ukocha kwa ajili ya kupata leseni za daraja C kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itafanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanzia kesho (Novemba 7 mwaka huu) hadi Novemba 20 mwaka huu.
 
Makocha 30 ndiyo wanaoshiriki kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi wanne; Jan Poulsen kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Kasimawo Laloko (Nigeria) na Sunday Kayuni wanaotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Kim Poulsen kutoka Chama cha Mpira wa Miguu Denmark (DBU).
Washiriki wa kozi hiyo ni Abdul Nyumba, Absolom Mwakyonde, Ahmed Mumba, Christopher Eliakim, Dismas Haonga, Edward Hiza, Eliasa Thabit, Emmanuel Massawe, Fulgence Novatus, Gabriel Gunda, Gideon Kolongo, Haji Amir na Hassan Banyai.
 
Wengine ni Juma Mgunda, Jumanne Ntambi, Keneth Mkapa, Leonard Jima,  Maarufu Yassin, Maka Mwalwisi, Mecky Maxime, Mohamed Tajdin, Mussa Furutuni, Mussa Kamtande, Peter Mhina, Richard Kabudi, Sebastian Nkoma,  Stephen Matata, Tiba Mlesa, Wane Mkisi na Wilfred Kidau.
 
STARS KWENDA CHAD NOVEMBA 9
Taifa Stars itaondoka nchini Novemba 9 mwaka huu kwenda N’Djamena, Chad kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia itakayochezwa nchini humo Novemba 11 mwaka huu.
 
Msafara wa timu hiyo utakaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Eliud Mvella utaondoka saa 9 kamili alasiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi ambapo utawasili N’Djamena saa 1 jioni ambapo Tanzania itakuwa saa 3 usiku.
 
Timu itarejea nchini Novemba 12 mwaka huu kwa ndege ya Ethiopian Airlines na kwenda moja kwa moja kambini kujiandaa kwa mechi ya marudiano itakayochezwa Novemba 15 mwaka huu.

Saturday, November 5, 2011

AYATOLLAH KHAMENEI'S MESSAGE TO HAJJ PILGRIMS

All praise belongs to Allah, the Lord of the Worlds, and blessings and greetings be upon the Master of the creatures, Muhammad al-Mustafa and his immaculate family and his chosen companions.  The spiritual spring of Hajj has arrived with its freshness, purity and God-given grandeur and majesty, gathering again the faithful and eager hearts like butterflies encircling the Ka'bah of divine unity and Islamic solidarity. Camped at Makkah and Mina, Arafat and Mash'ar are the fortunate human beings who, having responded to the call of "proclaim the Hajj to all the people", are being honored with the hospitality of the clement and munificent Lord. Here is the blessed House and the source of guidance from which the manifest divine signs radiated and the canopy of safety was set up to cast its universal shade. Cleanse your hearts in the Zamzam of piety, humility and God's remembrance. Open the inner eye to the lights of the divine signs. Embrace the spirit of submission and dedication, which are the hallmarks of true servitude. Keep refreshing in your hearts the memory of that father who, in willing compliance, led his Ishmael to the scene of sacrifice, thus showing us the clear path of attaining the friendship of the Glorious Lord and the manner of traversing it with a resolve infused with faith and an intent imbued with sincerity.
The station of Abraham is one among these manifest signs. The footprint of Abraham by the side of Holy Ka'bah, peace be upon him, is only a symbol of the station of Abraham. The station of Abraham is his station of dedication and self-sacrifice, his fortitude and resistance to personal desires and fatherly feelings as well as against the domination of kufr, polytheism and Nimrod, the tyrant of the time.
Today these two paths of deliverance lie open before each of us, individuals belonging to the Muslim Ummah. Determination, courage and firmness of resolve on the part of each one of us, can advance us towards the same goals to which mankind has been invited by the divine messengers from Adam to the Seal of the Prophets, with the promise of dignity and felicity, in the world and the hereafter, for those who take this path.
It will be appropriate for the Hajj pilgrims at this great assembly of the Islamic Ummah to address the most important issues of the Islamic world. The uprisings and revolutions in some of the important Islamic countries are the most important among these issues. The events that have taken place in the Islamic world in the interval between the previous and the current Hajj pilgrimage can change the destiny of the Islamic Ummah, and they forebode a bright future accompanied with dignity and progress, material and spiritual. Dictators and corrupt taghut, allied with foreign powers, have been overthrown in Egypt, Tunisia and Libya, and the stormy waves of popular uprising in some other countries threaten to bring down the castles of wealth and power.
This new chapter in the history of our Ummah reveals certain truths which are all manifest divine signs and teach us vital lessons. These truths should be taken into account by Muslim nations in all their calculations.
First, a young generation has emerged from among these nations after decades of political subjugation to foreign powers, which with admirable self-confidence, is ready to face dangers, confront the dominant powers and is determined to change the status quo.
Second, despite the authority and efforts of secular rulers and their overt and covert measures to curtail the influence of religion in these countries, Islam - with its evident and impressive presence - has become the guiding principle of popular expression and sentiment. Like a spring effusing through popular discourse and behavior, it has given vitality and freshness to the rallies and activities of the millions. The mosques and minarets, Islamic slogans and calls of "Allahu Akbar", all are clear indications of this fact and the recent Tunisian elections provide decisive evidence for this claim. Without doubt, free elections in any Islamic country will rarely result in anything except what happened in Tunisia.
As revealed for all by this year's events, God Almighty has placed such a force in the resolve and determination of nations that no power whatsoever can withstand it. With this God-given power nations can change their destiny and partake of divine help.
Furthermore, during the last decades arrogant powers, led by the United States, had reduced the regional states to a condition of subjugation through their political and security tactics. They imagined that they had opened up an obstacle-free highway for their rising economic, cultural and political domination over this sensitive part of the world. But now they are the primary target of the disgust and hatred of the region's nations. Certainly, the regimes emerging from these revolutions will never submit to the disgraceful inequalities of the past, and the political geography of the region will be determined by the nations in pursuance of their dignity and complete independence.
In addition, the crafty nature of the hypocritical Western powers has become all too apparent for the people of these countries. The U.S. and Europe made their utmost efforts to retain their pawns in Egypt, Tunisia and Libya, each one in a particular way. But when their wishes had to bow to the resolve of the nations, they cast a friendly yet wily smile at the triumphant public.
There are other valuable facts and manifest divine signs embedded in the regional events of the past year, which are not hard to discern for reflective minds.
The entire Islamic Ummah and especially the revolutionary nations nevertheless stand in need of two basic elements:
First, continuation of resistance and avoidance of weakness in resolve. In the Qur'an, the divine summons to the greatest messenger, may God bless him and his family, are addressed in these words: "Be steadfast, just as you have been commanded-[you] and whoever has turned [to God] with you-and do not overstep the bounds (11:112)" and "Be steadfast, just as you have been commanded (42:15)." Prophet Moses, peace be upon him, is quoted as telling his people: ‘Turn to God for help and be patient. The earth indeed belongs to God, and He gives its inheritance to whomever He wishes of His servants, and the outcome will be in favor of the God-fearing.' (7:128)
At the present, the most significant manifestation of fearing God for the nations that have risen up is not to halt in their auspicious movement, and not to let themselves be diverted by the achievements of this phase. This is the important part of piety and fear of God whose possessors are rewarded with the favorable outcome.
Second, vigilance with regard to the plots and tricks of the arrogant international powers who have suffered a setback from these uprisings and revolutions. They will not sit by idly. They will re-enter the arena with all their political, financial and security power to re-establish their influence and control in these countries. Their tools are the carrot and stick and deceit. Experience has shown there are some among the elite who are susceptible to these tricks. Fear, greed or negligence prompt them to serve the enemy. The vigilant eyes of the youth, intellectuals and religious scholars should be closely watching.
The biggest danger posed by the camp of kufr and the arrogant powers lies in its intervention and influence over the structures of the new political systems in these countries. They will do their utmost to see that the new systems do not take on an Islamic and democratic identity. All the concerned people in these countries and all those who cherish their homeland's honor, dignity and progress should work to ensure the complete and perfect Islamic and democratic character of the emergent polity. In this regard, the role of the constitutions will be prominent. National unity and official recognition of sectarian, tribal and ethnic differences are a precondition of future success.
The valiant revolutionary nations of Egypt, Tunisia and Libya, as well as other awakened and combatant nations, should know that the sole means of deliverance from the oppression and guile of the United States and other Western hubristic powers is to establish a global balance of power conducive to their interests. The Muslims should put themselves on equal footing with the great world powers in order to be able to reach a serious solution for their problems with the world devourers. This cannot be achieved except with the cooperation, understanding and solidarity of Islamic countries. This was the unforgettable testament of the great Imam Khomeini.
For months, the United States and NATO dropped bombs on the heads of the Libyan people making Gaddafi, a vicious dictator, an excuse. Gaddafi was someone who was considered their close friend before the brave uprising of the Libyan people. They used to coddle him, steal the wealth of Libya through his hands and shake or kiss his hand in order to dupe him. Following the people's uprising, they made him an excuse to destroy the entire infrastructure of Libya. Which state could stop the tragic massacre of the Libyan people and destruction of the country at the hands of NATO? Until the claws and fangs of the bloodthirsty and barbaric Western powers are not broken, such dangers will remain conceivable for Islamic countries. Safety from such dangers is not possible except by turning the Islamic world into a powerful pole.
Today the West, the United States and Zionism are weaker than ever before. Economic troubles, successive failures in Afghanistan and Iraq, deep-running public protests in America and other Western countries whose scope is widening daily, the struggles and sacrifices of the people of Palestine and Lebanon, the daring popular uprisings in Yemen, Bahrain and some other countries under American influence-all these are significant portents for the Islamic Ummah, especially for the emergent revolutionary nations. Faithful men and women throughout the Islamic world, particularly in Egypt, Tunisia and Libya should make the most of this opportunity for the formation of an international Islamic power bloc. The vanguard and the elite of the uprisings should place their trust in Almighty God and with reliance on His promise of help, adorn the new chapter in the history of the Islamic Ummah with their lasting achievements, thus earning God's approval and fulfilling the prerequisites of His help.
May Peace be upon God's righteous servants!
Seyyed Ali Hossaini Khamenei
29 Dhul Qa'dah, 1432
5 Aban, 1390
27 October, 2011