KAMATI ya
kusimamia Tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2012 zinazotolewa na Chama
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imepokea mapendekezo ya majina
ya wanamichezo kutoka vyama mbalimbali kwa ajili ya kuwania tuzo hizo kwa kila
mchezo.
Majina ya
wanamichezo hao yamependekezwa na vyama husika, isipokuwa mpira wa miguu kwa
wanaume pamoja na mpira wa kikapu, ambapo majina yameteuliwa na kamati kwa
kushirikiana na baadhi ya wahariri wa habari za michezo na wadau wa michezo
husika, ingawa awali vyama hivyo viliombwa kuwasilisha majina lakini
havikutekeleza ombi hilo hivyo kamati ikaamua kutafuta utaratibu mwingine wa
kupata majina.
Pia vyama viwili
vya michezo ya paralimpiki na baiskeli
bado majina hayajaifikia kamati yetu kutokana na sababu mbalimbali na tayari wameahidi
watawasilisha majina hayo kabla ya Mei 12 mwaka huu. Chama cha Mpira wa Wavu
pia kimeshindwa kuwasilisha majina.
Hatua ya mwisho
ambayo itafanyika baada ya kupokea mapendekezo hayo kwenye kila mchezo, Kamati
ya Tuzo za Taswa itafanya uchambuzi kupitisha majina hayo kulingana na sifa
ambazo vyama husika vimeleta kwa kila mwanamichezo na kuona kama wanastahili
kupewa tuzo kulingana na vigezo vya kamati na TASWA.
Awali TASWA
ilipanga tuzo hizo zifanyike Aprili 27 mwaka huu, lakini imeshindikana kutokana
na sababu mbalimbali zilizokuwa nje ya uwezo wa Kamati ya Tuzo pamoja na chama
kwa ujumla na sasa sherehe zitafanyika mwanzoni mwa mwezi Juni katika tarehe
itakayotangazwa baada ya kukubaliana na wadhamini, ambapo mazungumzo
yanatarajiwa kukamilika kabla ya Mei 15 mwaka huu.
Tunavishukuru
vyama vyote vilivyotupa ushirikiano kwa hatua ya awali kwa kutupatia
mapendekezo yao pamoja na kutaja sifa kwa kila mchezaji waliyewasilisha jina
lake nasi tunaahidi tutapitia kwa umakini mapendekezo hayo, lakini uamuzi wa
kamati ndiyo utakaokuwa wa mwisho.
TASWA itatoa tuzo
kwa kila mchezo ambao kamati yetu ambayo
Katibu wake ndiye pia Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando itajiridhisha
wanastahili, ambapo baadaye washindi wa kila mchezo watawania Tuzo ya
Mwanamichezo Bora wa Tanzania kwa Mwaka 2012.Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa
Tanzania kwa mwaka 2011 ilienda kwa Shomari Kapombe. Washindi wengine kwa miaka
ya karibuni ni Mwanaidi Hassan (2010 na 2009), Mary Naali (2008), Martin Sulle
(2007) na Samson Ramadhan (2006).
Majina ya
wanaowania kwa mwaka 2012:
MPIRA WA
MAGONGO-WANAUME
1 Sylvester
Kigodi
2. Casto
Mayuma
3. Gurtej
Bilu Singh
4. Vendri
Bhamra
5. Elias Samala
Gofu ya Kulipwa
1 Hassani Kadio
2 Yassin Salehe
3 Fadhili Nkya
4 Salimu Mwanyenza
5 Rajabu Iddy
GOFU YA RIDHAA WANAWAKE:
1:MADINA
IDDI
2:ANGEL
EATON
3.
HAWA WANYECHE
4.AYNE
MAGOMBE
GOFU
YA RIDHAA WANAUME
Jimmy Mollel
|
Frank Roman
|
Nuru Mollel
|
Martin MacDonald
|
John Said
|
|
NGUMI ZA RIDHAA-WANAUME
- Ismail Isack Galiatano
- Said Hofu
- Selemani Kidunda.
- Victor Njaiti
- Mohamed Chibumbui.
NGUMI ZA
RIDHAA WANAWAKE:-
1. Sara Andrew
2. Irene Kimaro
3. Easter Kimbe.
4. Mather George
5. Mariam Nyerere.
Ngumi za Kulipwa
1.
Francis Miyeyusho
2.
Ramadhan
Shauri
3.
Thomas
Mashali
4.
Said
Mbelwa
5.
Francis
Cheka
JUDO-TANZANIA BARA-WANAUME
1) AHMED MAGOGO
2) ADREW THOMAS MLUGU
3) GEOPHREY EDWARD MTAWA
4) GERVAS LEONARD CHILIPWELI
5) ABUU SELEMANI MCHETEKO
6)
ABUUBAKAR
NZIGE
JUDO
TANZANIA BARA WANAWAKE
1. MATRIDA .H. TEMBA
2. AMINA MOHAMED
JUDO ZANZIBAR-WANAUME
1. MOHAMMED KHAMIS JUMA
2. MASOUD AMOUR KOMBO
3. MBAROUK SULEIMANI SULEIMAN
JUDO ZANZIBAR-WANAWAKE
1.
GRACE ALPHONCE
2.
LAYLATI MOHAMMED
TENISI-WANAWAKE
[1]
Rehema Athumani
[2] Vailety Petar
[3]
Mkunde iddi
[4]
Edna John
[5]
Zuhura Baraka
TENISI Wanaume
[1]
Omary Abdalah
[2]
Yassini Shabani
[3]
Hassan Kasimu
[4]
Kiango Kipingu
[5]
Lebric Jacobu
MPIRA WA MIKONO-WANAUME
Faraji Shaibu
|
Nyuki ZANZIBAR
|
Hemedi Salehe
|
JKT
|
Abinery Kusena
|
JKT
|
Ally Khamis
|
Ngome
|
Hassani Yusufu
|
Magereza
|
MPIRA WA MIKONO-WANAWAKE
Catherine Mapua
|
Ngome
|
Dorisi Mangara
|
Magereza
|
Zakia Mohamed
|
Ngome
|
Happy Mahinya
|
JKT
|
Mary Kimiti
|
Magereza
|
RIADHA-WANAWAKE
1.Zakia Mrisho
2. Mary Naali
3.Jacklin
Sakilu
4.Sarah Ramadhani
5.Anjelin Tsere
5.Anjelin Tsere
6.
Sara Maja
RIADHA-WANAUME
1. Dickson Marwa
2. Faustine
Musa
3. Augstino Sule
4. Bazil John
5. Samson Ramadhan
KRIKETI-WANAUME
1. Abhik Patwa.
2.
Benson
Mwita.
3.
Sefu
Khalifa.
4.
Issa
Kikasi.
5. Riziki Kiseto
KRIKETI-WANAWAKE
Monica Pascal.
Mwanaiddi Ibrahim.
Hadija Nasibu
Esther Wales
Mwanaidi Ammy
SOKA-WANAWAKE
FATUMA MUSTAPHA
ASHA
RASHID
MWANAHAMISI
OMARY
SOPHIA
MWASIKILI
ESTER
CHABRUMA
SOKA-WANAUME
JOHN
BOCCO-AZAM
KELVIN
YONDANI-YANGA
SHOMARI
KAPOMBE-SIMBA
MCHA
KHAMISI-AZAM
MBWANA
SAMATTA-TP MAZEMBE
Thomas
Ulimwengu-TP Mazembe
WACHEZAJI
WA NJE WANAOCHEZA TANZANIA
EMMANUEL
OKWI-SIMBA(SASA ETOILE DU SAHEL)-SOKA
KIPRE
TCHETCHE-AZAM-SOKA
HARUNA
NIYONZIMA-YANGA-SOKA
HAMISI
KIIZA-YANGA-SOKA
MARY
WAYA-FILBERT BAYI –NETIBOLI (ALIKUWA KOCHA MCHEZAJI)
KIKAPU-WANAWAKE
Faraja Malaki- Jeshi
Evodia Kazinja-JKT Stars
Sajida Ahmed-Don Bosco
Rehema Kilomba-Donbosco
Tukusubira David-Vijana Queens
KIKAPU-WANAUME
Mussa
Chacha-Savio
Lusajo
Samuel Mwakipunda-Oilers
Salim Mchemba-ABC
Filbert
Mwaipungu-ABC
Steven
Atanasio-ABC
NETIBOLI
Lilian
Sylidion-Filbert Bayi
Mwanaidi
Hassan-JKT
Irene
Elias Kanile-Filbert Bayi
Jacqueline
Sikozi-Filbert Bayi
Faraja
Malaki-Jeshi Stars
WACHEZAJI BORA CHIPUKIZI
Salum
Abubakari-Azam-soka
Frank
Domayo-Yanga-soka
Edward
Cristopher-Simba-soka
Emmanuel
Malya-Tenisi Gymkhana Arusha
Tambwe
Juma-Kriketi
WATANZANIA
WANAOCHEZA NJE
Mbwana Samatta-TP
Mazembe
Ivo Mapunda-Gor Mahia
Hasheem Thabeet-Oklahoma
Thomas
Ulimwengu-TP Mazembe
Soud Abdulrazak-Uganda
(kikapu)
Mohammed Abdallah
‘dulah’-Uganda (kikapu)
No comments:
Post a Comment