Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) linaandaa utaratibu utakaowawezesha washabiki kwenda
jijini Harare, Zimbabwe kushuhudia mechi ya Taifa Stars.
Mechi hiyo ya
marudiano ya Kombe la Afrika kwa ajili ya fainali zitakazochezwa Morocco
mwakani itafanyika Jumapili (Juni 1 mwaka huu) jijini Harare.
Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilishinda mechi ya kwanza
iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0.
Usafiri huo utakuwa
wa basi ambapo washabiki wanatarajiwa kuondoka siku ya Ijumaa na kuwasili
Jumapili mchana jijini Harare ambapo watashuhudia mechi na kuanza safari ya
kurejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo.
Washabiki
wanatakiwa kuwa na hati za kusafiria (pasipoti), nauli ya kwenda na kurudi
itakuwa sh. 300,000.
USAJILI WA
WACHEZAJI KUANZA JUNI 15
Usajili wa
wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2014/2015) unaanza Juni 15 hadi Agosti
3 mwaka huu wakati kipindi cha kutangaza wachezaji walioachwa au kusitishiwa
mikataba ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu.
Kipindi cha kwanza
cha uhamisho wa wachezaji ni kuanzia Juni 15 mwaka huu hadi Julai 30 mwaka huu.
Kupitia majina na kutangaza pingamizi ni kati ya Agosti 4 na 11 mwaka huu.
Kuthibitisha usajili hatua ya awali ni Agosti 12 hadi 14 mwaka huu.
Usajili hatua ya pili
utakuwa kati ya Agosti 14 na 29 mwaka huu. Kupitia na kutangaza majina ya
pingamizi hatua ya pili ya usajili ni kuanzia Agosti 30 hadi Septemba 4 mwaka
huu. Uthibitisho wa usajili hatua ya pili ni Septemba 5 na 6 mwaka huu.
Kwa upande wa Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza Agosti 24 mwaka huu, na ratiba
inatarajiwa kutoka mwezi mmoja kabla (Julai 24 mwaka huu).
No comments:
Post a Comment