MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Wednesday, January 3, 2018

TRA YARAHISISHA USAJILI WA WALIPAKODI



Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Elijah Mwandumbya akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea kituo maalum kilichoteuliwa na mamlaka hiyo kilichopo Chanika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kampeni ya  usajili wa walipakodi.



Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni ya  usajili wa walipakodi inayofanyika nchi nzima kwa lengo la kuongeza idadi ya walipakodi, kupanua wigo wa ulipaji kodi na kuongeza mapato ya Serikali.



 Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (kulia)  Regina Urio akimhudumia mfanyabiashara aliyefika katika kituo maalum kilichoteuliwa na mamlaka hiyo kilichopo Chanika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusajili na kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).  



TRA YARAHISISHA USAJILI WA WALIPAKODI.



Na: Veronica Kazimoto,
Dar es Salaam.

Wafanyabiashara wanaostahili kulipa kodi kwa njia ya makadirio, watalipa robo ya kwanza ndani ya siku tisini (90) kuanzia siku waliyosajiliwa tofauti na utaratibu uliokuwepo wa kulipa kodi hiyo kabla mfanyabishara hajaanza kufanya biashara husika.
Hayo yamesema leo na Kamishna wa Kodi za Ndani Elijah Mwandumbya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) alipotembelea kituo maalum kilichoteuliwa na mamlaka hiyo kilichopo Chanika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kampeni ya  usajili wa walipakodi.
Kamishna Mwandumbya amesema kuwa, hapo awali wafanyabiashara walitakiwa kulipa robo mwaka ya kwanza mara baada ya kusajili na kupata Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) suala lililosababisha baadhi ya watu kushindwa kulipa kutokana na msingi mdogo wa biashara zao.
"Niseme tu kwamba, TRA tumeamua kuboresha huduma zetu kwa kuhakikisha kuwa, walipakodi wapya wanalipa makadirio yao ndani ya miezi mitatu tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo mfanyabiashara alitakiwa kulipa kabla ya kuanza biashara yake", alisema Mwandumbya.






No comments:

Post a Comment